Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 5 July 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI MAONESHO YA 46 YA BIASHARA SABASABA

Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Joanitha Deogratias (wa pili kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo.

Afisa Mikopo wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Cornel Mlay (kulia), akizungumza na mmoja ya mteja alietembelea banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Katikati ni Afisa Uwendeshaji wa Benki hiyo, Godbright Mlay.

Afisa Uendeshaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Salha Singano (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa mmoja ya mteja alipotembelea Banda la benki hiyo kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo. Kushoto ni Afisa wa Kitengo cha ICT, Joseph Bukuru.

Meneja Uhusiano wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Shilla Senkoro (kushoto), akizungumza na mteja kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana benki hiyo.

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imeshiriki maonesho ya 46 ya B
iashara Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa katika kuongeza matawi kila mkoa na wilaya ili kusogeza huduma kwa wateja wake.

Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo wa benki hiyo Joanitha Deogratias alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na wale wakubwa pia mikopo kwa wastaafu kwa ajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo za kiuchumi.

Joanitha alisema katika kuboresha huduma TCB imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi. Alisema benki hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kutoa unafuu kwa wateja wake kutokana hali ya kiuchumina ikiwemo kutoa unafuu wa riba.

“Sisi kama benki ya Biashara Tanzania TCB tumefungua milango kwa wateja wetu wote waliokopa na ambao hawajakopa, tunataka kuwaendeleza wateja hasa kwa kusikiliza changamoto zao na tumeendelea kufungua matawi Karibia nchi nzima,” alisema.

Vilevile benki hiyo imechukua hatua ya kuwakumbusha na kuwahimiza Watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022.

No comments:

Post a Comment