Branch, kampuni inayoongoza duniani kwa utoaji mikopo kwa watu binafsi kwa njia ya simu za mikononi, imeelezea nia yake thabiti ya kuwafikishia huduma za kifedha za gharama nafuu mamilioni ya Wanzania popote pale walipo.
Tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2015, Branch tayari imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 73 na kuwafikia zaidi ya watu milioni moja na laki tano walipo sehemu mbali mbali.
Mikopo ainayotolewa na Branch kupitia App yao inaanzia kiasi cha shilingi 5,000 hadi shilingi 1,000,000.
Akiongea na wahariri wa vyombo vya Habari, msimamizi wa huduma kwa wateja kwa Tanzania Reuben Wanyamawi, alisema Branch imejipanga vyema kuwafikishia huduma za mikopo Watanzania popote pale walipo na muda wowote hivyo kuwezesha kutatua changamoto zao zinazohitaji fedha.
“Branch inayofuraha kuwahudumia Watanzania na mkakati wetu ni kuwafikia Watanzania wengi zaidi popote pale walipo na muda wowote. Ni jambo la kuvutia kuona kuwa idadi ya watu wanaotumia huduma zetu imekuwa ikiongezeka kila kukicha,” alisema
Reuben aliongeza, “Tunaamini kuwa kila mtu popote pale lipo anahitaji na anastahili huduma za kifedha. Kuongezeka kwa matumizi ya simu janja kunaongeza fursa kwa watu wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha,”
Kwa mujibu wa msimizi huyo wa huduma kwa wateja, inachukua dakika chache tu kwa mtu kuomba mkopo na kuupata kupitia App ya Branch. “Ukishathibitishwa, inachukua dakika chache tu kupata mkopo wako. Tunatumia taarifa zilizopo kwenye simu za wateja kufanya maamuzi ya kutoa mikopo. Kama ombi lako halijakubaliwa, usijali. Wakati mwingine huchukua mara kadhaa kuomba ndiyo mteja apate mkopo,” alisema
Katika kuhakisha wateja wanafurahia huduma zao alisema, Branch ina utaratibu wa rufaa ambapo kama mteja akimshawishi mteja mwingine kuchukua mkopo na akaulipa kwa wakati, mteja huyo atapata zawadi ya shilingi 7,000 na mteja mpya atapata zawadi ya shilingi 7,000 pia.
No comments:
Post a Comment