Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakitoa burudani ya ngoma za asili wakati wa kampuni ya Vodacom walipokwenda shuleni hapo kwa ajili ya kutoa misaada ya vifaa mbalimbali. |
Vodacom Tanzania Yakabidhi Vifaa kwa Shule ya WasichanaVodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Wasichana ya Bethsaida mjini Dar es Salaam ambavyo kampuni ilishinda katika mashindano ya makampuni ya Vodacom duniani.
Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis alisema, “Elimu ni msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga miasha bora.
Hii ni kweli zaidi kwa Watoto yatima ambao tegemeo lao ni elimu pekee.”Shule ya Wasichana ya Bethsaida ilichaguliwa kupokea msaada huu kwa kuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.
Mkurugenzi wa Vodacom pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni waliikabidhi shule hiyo viti 100, vitabu Zaidi ya 300 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua. Bi penessis alielezea Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom ilijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa wa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.
Msaada huu unaendana na malengo ya Vodacom Tanzania kuongeza ujumuishwaji katika elimu. Hivi karibuni, kampuni ya Vodacom ilizindua mpango wa kupanua wigo wa mfumo wa E-Fahamu kufikia nchi nzima. E-Fahamu ni huduma inayotoa mawaidha ya elimu yenye viwango vya kimataifa na vyenye kukidhi miongozo ya serikali juu ya elimu.
Kuhusu Vodacom Tanzania FoundationThe Vodacom Tanzania Foundation ni sehemu ya kampuni ya Vodacom Tanzania PLC yenye mamlaka ya kutoa huduma za kijamii zikiwa zinawalenga zaidi wanwake na vijana. Foundation inajumuisha utoaji wa hisani na kutumia uwezo utakanao na teknolojia kuleta suluhisho kwa mahitaji ya kijamii.Ikishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, Vodacom Tanzania Foundationimesaidia zaidi ya miradi 120 hadi sasa ikiwa imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 15 kuboresha Maisha ya watanzania.Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:
No comments:
Post a Comment