Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926_270926_101026

Absa Banner_170926_270926_101026

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Tuesday, 13 October 2026

EQUITY BANK YARAHISISHA MALIPO YA SERIKALI KIDIJITALI KUPITIA EQUITY MOBILE APP

Equity Bank Tanzania imeendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kuwawezesha wateja kufanya malipo ya serikali kidijitali kupitia Equity Mobile App, kwa haraka na usalama popote walipo nchini.

Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kukamilisha malipo yao bila kulazimika kutembelea benki, hatua inayookoa muda na kuongeza urahisi katika matumizi ya huduma za kifedha.

Ili kufanya malipo, mteja anatakiwa kufungua Equity Mobile App, kubofya sehemu ya “Muamala”, kuchagua “Malipo ya Serikali” na kuingiza Control Number ili kukamilisha muamala.

Equity Bank inawahimiza wateja kupakua Equity Mobile App au kupiga *150*07# ili kufurahia huduma za kifedha zilizo rahisi, salama na zinazopatikana popote walipo.

Hatua hiyo inaendana na juhudi za benki hiyo za kuendeleza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za kifedha na kuwapa wateja urahisi zaidi wa kufanya miamala yao ya kila siku.

Soma habari zaidi za biashara, benki na fedha kupitia Kitomari Banking & Finance Blog.

Mitandao ya kijamii:

No comments:

Post a Comment