Mwenye tuzo anakuja, wenye kelele mmejipanga? Marioo ametangazwa kujiunga na line-up ya 4Plays, sherehe za miaka minne ya 1245, zitakazofanyika Oktoba 17, Superdome Arena, Masaki.
Baada ya kutwaa tuzo ya Best Male East Africa kwenye AFRIMMA 2026, Marioo anakuja na sababu nyingine ya mashabiki kusherehekea. Kutoka kumpongeza kwenye comments hadi kuimba naye mbele ya jukwaa, Superdome itachimbika!
Staa huyo anaungana na Young Jonn kutoka Nigeria kwenye line-up inayofanya kauli ya “nitaona kama nitakuja” kuwa ngumu kuitetea. Bongo Flava na Afrobeats zinakutana kwenye usiku mmoja wa kusherehekea miaka minne ya 1245.
Sherehe hizo zinaungwa mkono na Air Tanzania, Clouds Media, Johari Rotana, Heineken na Don Julio, kuongeza nguvu kwenye burudani hiyo inayosubiriwa kwa hamu.
Birthday ni ya 1245, lakini zawadi ni ya mashabiki! Nunua tiketi kupitia 4plays.1245tz.com au wasiliana kupitia 0748 211 245.
Oktoba 17, Dar es Salaam itasimama. Utakuwepo au itahadithiwa? Hii ni Chess sio Checkers

No comments:
Post a Comment