- Kampuni imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 108 hadi sasa na kuchangia kutengeneza ajira zaidi ya 2,100, huku ikiongoza kwa sehemu ya soko la intaneti ya faiba majumbani nchini Uganda na Tanzania.
- Savanna Telecom (Africa) Limited na mshirika wake FiberHome wanaendeleza dhamira ya pamoja ya kufanya huduma za intaneti ya kasi majumbani zipatikane kwa gharama nafuu barani Afrika.
CAPE TOWN, Afrika Kusini, Novemba 16, 2026: Wakati maandalizi yakiendelea kuelekea ufunguzi wa Maonesho ya Teknolojia ya Afrika (Africa Tech Festival – ATF), mkutano mkubwa zaidi wa sekta ya mawasiliano ya simu barani Afrika, utakaofanyika kuanzia Novemba 17 hadi 19 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Cape Town (Cape Town International Convention Centre), Savanna Telecom (Africa) Limited, kampuni mama yenye makao yake nchini Mauritius inayomiliki Savanna Fibre nchini Uganda, Tanzania na Kenya, imetangaza mafanikio makubwa katika shughuli zake pamoja na mpango kabambe wa kupanua miundombinu ya mawasiliano mwaka 2027.
Katika kipindi kifupi cha shughuli zake, Savanna imevuka idadi ya wateja 250,000 wanaotumia huduma ya intaneti ya kasi kupitia nyaya za nyuzinyuzi (fibre optic) majumbani nchini Uganda, Tanzania na Kenya. Mafanikio haya yamefikiwa kupitia miundombinu inayofikia zaidi ya makazi milioni moja katika maeneo ambayo huduma hiyo imefikishwa.
Ikiendeleza kasi hiyo ya ukuaji, kampuni imekamilisha usanifu wa kihandisi kwa ajili ya upanuzi zaidi wa miundombinu utakaowezesha huduma kufikia makazi mengine milioni moja ndani ya kipindi cha miezi 12 ya mwaka 2027. Mpango huo unawakilisha upanuzi mkubwa wa miundombinu ya mawasiliano katika Afrika Mashariki, huku sehemu kubwa ya uwekezaji huo ikielekezwa katika miji midogo na vitongoji ambavyo havijawahi kufikiwa na huduma za intaneti ya faiba kutoka kwa kampuni nyingine.
Kuweka Huduma za Intaneti Nafuu na Kupatikana kwa Wote Barani Afrika
Savanna ilianzishwa kwa imani moja kuu: upatikanaji wa intaneti unapaswa kuwa jambo la kawaida na la gharama nafuu kama kuwasha taa. Kwa muda mrefu, huduma za intaneti ya kasi barani Afrika zimejikita zaidi katika maeneo ya biashara mijini na vitongoji vinavyoishi watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha.
Savanna inalenga kuwafikia wananchi wengine ambao hawajafikiwa vya kutosha, wakiwemo wanafunzi wanaojisomea nyakati za usiku, wafanyabiashara wanaopokea malipo kupitia simu za mkononi, vituo vya afya vya vijijini vinavyopata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu walioko mijini, pamoja na kaya ambazo hazijawahi kuwa na huduma ya intaneti ya uhakika.

.jpeg)
.jpeg)






.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)





.jpeg)




.jpeg)
