Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_301026_111126

Stanbic Bank Banner_201026

Friday, 13 November 2026

BENKI YA AZANIA YATANGAZWA MDHAMINI MKUU WA MKUTANO MKUU WA 40 WA ALAT JIJINI MWANZA


Mwanza, Novemba 12, 2026 – Benki ya Azania PLC imetangazwa rasmi kuwa Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), utakaofanyika jijini Mwanza kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2026.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa ALAT na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Mhe. Constatine Sima, ameishukuru Benki ya Azania kwa kuunga mkono mkutano huo kupitia udhamini wake. Aidha, amewakaribisha wajumbe kutoka maeneo mbalimbali nchini kushiriki katika mkutano huo muhimu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Biashara za Serikali wa Benki ya Azania, Ndg. Samson Mahimbi, amesema udhamini huo ni sehemu ya dhamira ya benki hiyo ya kuunga mkono maendeleo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Ameeleza kuwa Benki ya Azania inalenga kuwa mshirika wa kimkakati wa Halmashauri kupitia utoaji wa suluhisho mbalimbali za kifedha zinazolenga kuboresha ufanisi wa shughuli za Serikali za Mitaa.

Suluhisho hizo ni pamoja na huduma za ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa fedha pamoja na ufadhili wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma na maisha ya wananchi.

Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Azania inalenga kuimarisha mahusiano yake na Halmashauri nchini na kuchangia juhudi za kukuza maendeleo endelevu ya jamii.

Mkutano Mkuu wa 40 wa ALAT unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha viongozi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, usimamizi na maendeleo ya mamlaka hizo nchini.

Benki ya Azania – Benki Inayozidi Matarajio!

No comments:

Post a Comment