Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926_270926

Absa Banner_170926_270926

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Thursday, 13 May 2021

DStv INAKULETEA KAIZER CHIEFS VS SIMBA FC LIVE

 

Ni mwendo wa bandika bandua kupitia #SokaLisilopimika pekee!

Tazama Kaizer Chiefs vs Simba FC kupitia chaneli 270.

WAKAZI WA KATAVI WAIPOKEA BENKI YA NBC KWA SHANGWE

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, Meneja wa Huduma za NBC Wakala, Robert Madaki, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya hiyo, Elibariki Masuke, na kulia ni Wakala wa ofisi hiyo Emmanuel Atimili.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, pamoja na Maofisa wengine kutoka Benki hiyo na Wakala wa Ofisi hiyo Emmanuel Atimili.

Taarifa kwa Umma Mei mwaka huu 2021 Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Benki ya NBC kwa kuzindua NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani kwa kuwepo kwa wakala mkuu huyo kutafungua fursa za kiuchumi, kuziendeleza pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara katika Mkoa huo.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo la NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera ameupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu ambapo watu zaidi ya elfu moja wamefungua akaunti katika tawi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Homera aliupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Katavi. Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. Komredi Homera pia aliusihi uongozi wa Benki ya NBC kutoa mikopo kwa wajasiriamli wa Katavi ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwa haraka.

Aidha Homera ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa msaada mifuko 300 ya saruji, Bati 60 sambasamba na ndoo 5 za rangi katika Cho Cha Afya huku benki hiyo ikiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa mawili katika chuo hicho.

Tuesday, 11 May 2021

DStv INAKULETEA MPALI KILA JUMATATU - ALHAMISI


Mpali inazidi kuwa 🔥🔥🔥

Tazama visa hivi vya Nguzu na familia yake kila siku ya Jumatatu - Alhamisi saa 12:00 jioni kupitia @maishamagicbongo, Chaneli 160.

Piga *150*53# kulipia kifurushi Bomba sh 19,900 tu.

#vyanyumbanihuanziadstv

KCB GROUP TO SPEND SH6BN IN BUYING RWANDAN, TANZANIAN BANKS

KCB Group CEO Joshua Oigara (right) Chairman Andrew Kairu (centre) and Group CFO Lawrence Kimathi during the release of the full-year results.

KCB Group will spend a total of Sh6 billion to acquire two banks in Rwanda and Tanzania from London-listed Atlas Mara limited.

The Nairobi Securities Exchange-listed firm had earlier estimated it would acquire a 62 percent stake in Banque Populaire du Rwanda Plc (BPR) and a 100 percent ownership in African Banking Corporation Tanzania Limited at a cost of $40 million (Sh4.2 billion).

The amount has increased after KCB sought to make a full buyout of the Rwandan bank by making an offer to its minority shareholders who hold a combined 38 percent stake.

“The group has made an offer to the remaining shareholders of BPR for the acquisition of the remaining stock at the same terms as Atlas Mara's to raise its ownership to 100 percent,” KCB says in its latest annual report.

“Once approved, the aggregate completion consideration that would be payable by KCB for acquisition of the combined assets is estimated at current values and exchange rates to be $56.9 million (Sh6 billion).”

Atlas Mara is selling its African banks to KCB and other lenders to raise funds to pay its creditors, some of whom have launched liquidation proceedings against the multinational that was the brainchild of former Barclays Plc’s chief executive Bob Diamond.

I&M BANK COMPLETES ACQUISITION OF UGANDAN LENDER


I&M Holdings Plc. has completed the acquisition of 90 percent shareholding in Uganda’s privately-owned lender Orient Bank Ltd (OBL) as part of its regional expansion plan.

In a statement Monday, I&M said the acquisition was completed on April 30, 2021 after the transaction received the necessary approvals from the Central Bank of Kenya, Bank of Uganda, Capital Markets Authority of Kenya and the Common Market for Eastern and Southern Africa (Comesa).

The agreement for the deal priced at Ush96.75 billion ($26.93 million) was made in July last year.

“I&M Group aspires to be Eastern Africa’s leading financial partner for growth. The acquisition of OBL will place I&M Bank in an advantageous position to capitalise on the growth in the Eastern African economies and thereby ultimately increasing shareholder value,” said Sarit Raja Shah, I&M’s Group Executive Director.

Continue Reading > > >

CLYDE & CO UPDATER - TANZANIA ISSUES NEW MINING RULES ON DISPUTE RESOLUTION


Tanzania recently issued new Mining (Disputes Resolution) Rules, directly impacting companies and individuals operating in the mining sector and revoking the previous rules in effect. In this article, we provide an overview of the new rules and the key implications to consider.

Background

The Mining (Disputes Resolution) Rules (the Rules) which are made under section 122 of the Mining Act Cap 123 Revised Edition 2019 (the Mining Act), were published in the Government Gazette dated 16 April 2021 and repeal the Mining (Disputes Resolution) Rules Government Notice No. 224 of 1999.

Application of the Rules

The Rules will directly affect persons engaged in prospecting or mining operations and any third parties but not the Government. This means that the Executive Secretary of the Mining Commission (the Commission) will have power to inquire into and decide disputes between the abovementioned persons. The law permits this power to be delegated to any officer of the Commission who holds - at a minimum - the rank of a director.

Section 119(1)(a)-(d) of the Mining Act provides that the Commission will decide disputes in connection with:
  • boundaries of areas subject to mineral rights;
  • claims by any persons entitled to erect, cut, construct or use any pump, line of pipes, flume, race, drain, dam or reservoir for mining purposes, or to have priority of water taken, diverted, used or delivered, as against any other person claiming the same;
  • assessment and payment of compensation in line with the Mining Act; and
  • any other matter which may be prescribed by law.

The Commission

The Commission is managed by the Executive Secretary who is the Chief Executive Officer. The Executive Secretary is appointed, for a term of five years, by the President of the United Republic of Tanzania to oversee the management of the Commission. After the five year tenure, the Executive Secretary will be eligible for re-appointment.

Monday, 10 May 2021

BENKI YA NMB YADHAMINI MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya thamani ya sh milioni 15 kutoka kwa Mhazini Mkuu wa Benki ya NMB, Azizi Chacha jana kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliyoanza jana uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri Elimu, Omari Kipanga na watatu ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo.

Dodoma - Benki ya NMB imekabidhi kitita cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya udhamini wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) yaliyofunguliwa rasmi jana Jijini Dodoma.

Akizungumza jana Mhazini Mkuu wa Beniki ya NMB, Azizi Chacha alisema benki hiyo imetoa fedha hizo ikiwa ni udhamini wa mashindano hayo yanayoandaliwa na Serikali kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Chacha alibainisha kuwa lengo la NMB kutoa fedha hizo ni kuisaidia Serikali katika kufanikisha mashindano hayo ya Kitaifa ambayo yamekuwa na malengo ya kuibua wabunifu wapya kila mwaka.

BENKI YA NBC YAZINDUA KLABU YA WAFANYABIASHARA MKOANI KIGOMA

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta (wapili kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi wakifurahia baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika wenye lengo la kuwakutanisha wateja wake wafanya biashara na wenye viwanda na wadau wengine. Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanayabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya NBC, Mussa Mwinyidaho pamojana Mteja wa Benki hiyo, Marietha Patrick.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta (wa sita kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa saba kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma baada ya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa huo uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Benki ya NBC imezindua klabu ya wafanyabiashara wa benki hiyo mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya mipango ya benki hiyo kusogeza huduma kwa wateja wake sambamba na kujenga mtandao ambao utawasaidia wafanyabiashara wateja wa benki hiyo kufanya biashara zao kwa tija.

Theobald Sabi ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC,Theobald Sabi akizungumz kwenye uzinduzi wa klabu hiyo ya wafanyabiashara kwa mkoa Kigoma alisema kuwa lengo kubwa la klabu hiyo kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kwenye sekta ya biashara kuzungumza kwa pamoja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao na kuzitatua.

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA MIFUKO 500 YA SARUJI MKOA WA KIGOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi (wanne kulia) akikabidhi msaada wa mifuko mia tano 500 ya saruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule mkoani humo. Mifuko hiyo ilipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchatta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Nd Thobias Adengenye. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma.

Benki ya Taifa ya Biashara imekabidhi mifuko 500 ya seruji kwa Mkoa wa Kigoma kusaidia juhudi za serikali za ujenzi wa madarasa mkoani humo. Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchata akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Thobias Andengeye pamoja na kuishukuru Benki ya NBC alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa kutokana na muamko wa wazazi wa Kigoma kupeleka watoto shule kufuatia maamuzi ya serikali kutoa elimu bure.

“Tunategemea wanafunzi wapatao 40,771 kuhitimu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 kuepelekea uhitaji wa madarasa ziaidi ya 1,010 huku mkoa wetu ukiwa na madarasa 405, hivyo mchango wa Benki ya NBC wa mifuko 500 ya saruji utaisaidia kusukuma malengo serikali yetu ya mkoa kukamilisha ujenzi wa madarasa zaidi ya 605.” Alisema Nd Mchata.

ABSA BANK TANZANIA CO-SPONSORS FINTECH & HEALTHTECH YOUTH ENTREPRENEURS IN THE INAUGURAL WAZO CHALLENGE TANZANIA DEMO DAY


Absa Bank Tanzania announced youth entrepreneurial winners of the Wazo Challenge Tanzania Demo Day. The program was managed and organized by Startup Réseau; an India-headquartered startup accelerator which kick-started its East Africa expansion with the inaugural edition of the "Wazo Challenge Tanzania", announced in February 2021.

Wazo Challenge Tanzania focussed on 5 thematic areas - Financial Services, Healthcare, Agriculture, Energy / Utility and Education. As a part of the program, Startup Réseau hosted a Venture Bootcamp, wherein 10 high-potential founders were selected for a 4-week venture mentorship and leadership development bootcamp, that was delivered by successful founders, industry leaders, domain experts and investors from Startup Réseau’s global network. The Venture Bootcamp also had a parallel track of “Office Hours” wherein 15 more startups from the application pool were mentored.

This one-month long venture development bootcamp operated from March - April 2021 having winners compete for a cash grant of USD 10,000 determined by the stage of startups, the founders’ vision, uniqueness, market opportunities and clarity of business model. The grant money was disbursed as Top-3 prizes of USD 5,000 (Kikoba App), USD 3,000 (Mipango App) and USD 2,000 (MedPack)

Saturday, 8 May 2021

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKABIDHI MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 220 MACHOCHWE

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Nurdin Babu, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Machochwe, Martha Marwa baada ya kuzindua kisima kilichochimbwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika kijiji hicho. Mradi huo una thamani ya Shilingi 220 milioni ambapo wakazi 12,000 watanufaika. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Nurdin Babu, akizungumza kwenye uzinduzi wa kisima kilichochimbwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika kijiji cha Machochwe. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Water Aid, Anna Mzinga na Mkurugenzi wa Mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha(kulia).
Viongozi wa kimila wa Machochwe Wilayani Serengeti (walioshika fimbo) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha mji chenye thamani ya shilingi milioni 220 kilichochimbwa kwa uafadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kinaweza kuhudumia watu 12,000.
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), John Wanyancha akizungumza wakati wa kukabidhi kisima katika kijiji cha Machochwe Mkoa Mara.

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi 220m/- katika Kijiji cha Machochwe kilichopo wilayani Serengeti Mkoani Mara ikiwa ni jitihada zake za kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji salama kwa wananchi wa eneo hilo.

Mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia watu 12,000, unahusisha uchimbaji wa kisima,ununuzi wa tanki la maji na pampu yenye uwezo wa kuvuta lita 7,500 kwa saa.

Akizungumza wakati wa kukabidi kisima hicho, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL John Wanyancha alisema kampuni hiyo kupitia mradi wa ‘Maji ni Uhai’ imesaidia uchimbaji wa visima vilivyosaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ikiwamo Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa zaidi ya watu milioni moja.

BENKI YA CRDB YAKUSANYA WADAU KUJADILI UVUMBUZI KATIKA SEKTA YA FEDHA

Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe akiongoza Kongamano lililoandaliwa kwa kushirikiana kati ya Benki ya CRDB na Vodacom Tanzania na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma. Hii ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).

Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada wa Benki ya CRDB Ndugu Mangire Kibada akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.


Dodoma, Mei 06, 2021 – Benki ya CRDB imefanya kongamano lililobeba mada ya “Ni kwa namna gani sekta ya fedha inapaswa kuenenda kwa mwaka 2021?” ukizingatia dunia inapita katika changamoto ya janga la COVID-19 liloshika kasi mwaka 2020. Kongamano hilo lilioandliwa kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom liliongozwa na Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliasisiwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Friday, 7 May 2021

NCBA BANK TANZANIA APPOINTS JULIUS KONYANI AS AN EXECUTIVE DIRECTOR


NCBA Bank Tanzania Limited has appointed Julius Konyani to the Board of Directors as an Executive Director following the redeployment of Gift Shoko to NCBA Bank Kenya as the Group Director, Regional Subsidiaries. This appointment has also been approved by Bank of Tanzania (BOT).

Konyani brings to the board over 17 years of extensive experience and expertise in Banking and Management having served in an array of leadership roles in banks locally, including CRDB Bank PLC, NMB Bank PLC, United Bank of Africa (T) LTD the Defunct Commercial Bank of Africa Tanzania among others.

Konyani is currently the NCBA Tanzania, Head of Retail and Business Banking where he has been instrumental in strengthening and growing its retail business following the merger of NIC and Commercial bank of Africa (CBA) in 2019. He was also the country project lead for the successful integration of the two banks which gave birth to NCBA effective July 2020.

BENKI YA NMB YABORESHA BIMA YA FARAJA, YATAMBULISHA BIMA YA VIKUNDI

Mkuu wa Kitengo cha Bima (Head of NMB Bancassurance Department) cha Benki ya NMB, Martine Massawe (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Bima ya Maisha. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Life (CEO), Amani Boma na kulia ni Meneja Mkuu wa Biashara ya Makampuni Sanlam, Nura Masood.

Kwa mara nyingine Benki ya NMB imedhihirisha kauli mbiu yake kuwa ipo karibu na wateja, imekuja na maboresho ya huduma zake za bima ili kuhakikisha Watanzania wanapata faraja wakati wa matatizo.

Benki hiyo inashirikana na kampuni mbili za bima, Metropolitan Life na Sanlam Life ambapo watakuwa na utaratibu wa kutoa bima za maisha na vikundi kwa wateja na wasio wa NMB, katika kuangalia matarajio ya wateja wao baadae ikitokea hatari katika maisha yao na hivyo kusaidia malengo ya wateja kufikiwa hata kama wao hawapo au wamepata ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Bima NMB, Martine Massawe alisema wameiboresha huduma ya bima ya NMB Faraja kwa kuongezea kiasi cha fedha kinachotolewa lakini pia kuongeza kpengele cha ulemavu wa kudumu atakaopata mteja pia atalipwa lakini pia wamekuja na hudma mpya ya bima kwa vikundi.

WANUFAIKA WA KILIMO - VIWANDA WATEMBELEA KIWANDA CHA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI MWANZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries, Mark Ocitti, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, wakati wanafunzi ambao ni wanufaika wa programu ya Kilimo-Viwanda kutoka Chuo cha kilimo cha Igabiro Wilayani Muleba, Mkoani Kagera walipotembelea kiwanda cha Mwanza kujionea uzalishaji wa bia. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Sadock Stefano.

Mpishi wa bia wa zamu (Shift Brewer) Christina Machaka akiwaeleza namna bia inavyopikwa kwenye mitungi maalum wanafunzi wa Chuo cha Kilimo lgabiro walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti Tawi la Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo kupitia wa programu ya Kilimo-Viwanda inayoendeshwa na Kampuni ya Serengeti.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo lgabiro cha Mkoani Kagera, Neema Michael, akizungumza jinsi alivyonuifa kwa kulipiwa ada na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia programu ya Kilimo-Viwanda, ambapo wanafunzi wa Chuo hicho walitembelea Kiwanda cha Mwanza. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries, Mark Ocitti na anayefuatia ni Mkuu wa Chuo hicho, Sadock Stephano.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo Igabiro kilichopo Muleba Mkoani Kagera ambao ni wanufaika wa programu ya ufadhili wa mosomo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti inayojulikana kama Kilimo-Viwanda wakiwa lkatika ziara ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mwanza.

Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imejidhatiti kuwapa wanafunzi nyenzo na mafunzo zaidi ya kivitendo kama njia mojawapo ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kilimo nchin Tanzania.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti katika tukio la kuwapongeza wananfunzi 17 waliopata nafasi za ufadhili kupitia programu hii kutoka chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture kilichopo mkoa wa Kagera. SBL imelenga kufanya haya kupitia program hii maarufu inayojulikana kama Kilimo Viwanda inayolenga kusaidia wanafunzi kutoka familia masikini ili waweze kusomea masomo ya kilimo kwenye ngazi ya diploma katika vyuo vya ndani.

Wednesday, 5 May 2021

BENKI YA NMB YAENDESHA DROO YA 'BONGE LA MPANGO'

Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akibofya kitufe kumpigia mmoja wa washindi kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.

Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbezi Louis, Nestory Mwombeki (kushoto) akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo tawini hapo. Wa pili kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo wakiwa kwenye hafla hiyo.

Tuesday, 4 May 2021

TAZAMA NUSU FAINALI ZA UEFA LIVE NDANI YA DStv

 

Ule muda uliokuwa ukisubiriwa sasa umewadia!

Nusu fainali za UEFA zitakazoamua timu zitakazoingia fainali.

Je wewe utabiri wako unautupia wapi...?

Piga *150*53# kulipia sasa kifurushi chako cha Compact Plus TShs 89,000 tu ili usikose mechi hizi.

#SokaLisiloPimika

Friday, 30 April 2021

AIRTEL AFRICA APPOINTS OLUSEGUN OGUNSANYA AS CEO


London and Lagos, 29 April 2021: Airtel Africa plc ("Airtel Africa", or the "Company"), a leading provider of telecommunications and mobile money services, with a presence in 14 countries across Africa, announces Olusegun “Segun” Ogunsanya, Managing Director and CEO Nigeria is to succeed Raghunath “Raghu” Mandava, as Managing Director and Chief Executive Officer following Raghu Mandava’s informing the Board of his intention to retire. Segun Ogunsanya will join the Board of Airtel Africa plc with effect from 1 October 2021.

Segun Ogunsanya joined Airtel Africa in 2012 as Managing Director and CEO Nigeria and has been responsible for the overall management of our operations in Nigeria, our largest market in Africa. Segun has more than 25 years’ business management experience in banking, consumer goods and telecoms. Before joining Airtel in 2012, Segun held leadership roles at Coca-Cola in Ghana, Nigeria, and Kenya (as MD and CEO). He has also been the Managing Director of Nigerian Bottling Company Ltd (Coca-Cola Hellenic owned) and Group head of retail banking operations at Ecobank Transnational Inc, covering 28 countries in Africa. He is an electronics engineer and also a chartered accountant.

NMB BANK PLC CONTINUES STEADY GROWTH MOMENTUM WITH STRONG Q1 2021 RESULTS

NMB Bank Chief Executive Officer, Ms. Ruth Zaipuna.
Tanzania’s Leading Bank, NMB Bank Plc continued its strong performance in Q1 2021. The Bank’s Profit before tax increased 34% YoY to TZS 93 billion, while Profit after tax is up 33% YoY to TZS 65 billion in the Quarter ended 31 March 2021.

The solid performance reflects continued revenue growth momentum, disciplined cost-optimization, and enhanced loan portfolio management.

Total revenue grew 16% YoY to TZS 224 billion from TZS 193 billion recorded in Q1 2020. The revenue growth was driven by increase in net interest income due to increase in both loans and advances and investment in government securities. In addition, the bank recorded 10% YoY growth in Non-funded income mainly due to increased customer activities on the bank’s digital platforms.

The Bank continues to demonstrate enhanced operational efficiency. The execution of cost-optimization initiatives continues to yield positive results, with cost-to-income ratio improving to 48% in Q1 2021 from 52% in Q1 2020, well below the regulatory threshold of 55%. The bank will continue to implement cost-optimization and operational efficiency initiatives in line with overall bank’s strategic ambitions while continuing to serve customers better.

BENKI YA NCBA TANZANIA YAMTEUA JULIUS KONYANI KUWA MKURUGENZI MTENDAJI KWENYE BODI YA WAKURUGENZI

Benki ya NCBA Tanzania imemteua Bwana Julius Konyani kuwa Mkurugenzi Mtendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi baada ya Gift Shoko kuhamishiwa Kenya kama Mkurugenzi wa Grupu pamoja na matawi ya benki hiyo Afrika Mashariki. Uteuzi huu umethibitishwa na Benki Kuu ya Tanania (BOT).

Konyani anashika nafasi hiyo mpya akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 17 kwa bodi ya benki hiyo akiwa amefanya kazi na kushika nyadhifa mbali mbali za kiuongozi na kiutawala kwenye benki kama CRDB Bank PLC, NMB PLC, United Bank of Africa (T) Limited.

Kabla ya uteuzi huo, Konyani alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Reja Reja na za Kibiashara za benki NCBA na amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza biashara za reja reja za benki hiyo kufuatia muunganiko kati ya NIC na Commercial Bank of Africa (CBA) mwaka 2019. Konyani aliongoza timu iliyoshughulikia muunganiko kati ya NIC na CBA ambao ulipelekea kuzaliwa kwa benki ya NCBA mwezi Julai mwaka 2020.

Tuesday, 27 April 2021

NMB BANK EYES ‘BODABODA’ RIDERS WITH TSHS 5 BILLION IN LOANS SCHEME

The Minister of State in the Prime Minister's Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled), Jenista Mhagama (right) and NMB Bank Plc, Chief Executive Officer, Ruth Zaipuna (centre) try one of the tricycles during an event at which the lender announced that it had set aside TShs 5 billion for lending to youth who work as 'Bodaboda' motor cycle 'taxi' drivers in Dar es Salaam over the weekend. Looking on is NMB Bank Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi.

Dar es Salaam - Bodaboda riders now have every reason to boost their incomes as NMB Bank Plc sets aside Sh5 billion for lending to them.The money, set aside the NMB Mastaboda loan initiative, is geared towards helping the youth who are engaged in the motorcycles business popularly known as ‘Bodaboda’ so that they can grow their businesses and contribute to the country’s economic growth.

Available data shows that Tanzania was home to over two million Bodaboda taxi riders who would benefit from the initiative and join the banked segment of the society.

The minister for State in the Prime Minister’s Office (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled), Ms Jenista Mhagama, graced the launch of the NMB Mastaboda loan initiative in Dar es Salaam at the weekend during the event that was also attended by about 300 ‘Bodaboda taxi’ riders.
To qualify for the loan, a Bodaboda rider will be required to open an account with NMB Bank Plc.

Apart from operating the account for three months consecutively and being a member of the of bodaboda riders’ associations, one will also be required to possess a National Identification card.

Speaking during the event, Ms Mhagama said the loan initiative was complimenting government efforts to empower youth so that they can actively participate in Tanzania’s economic growth efforts.

DStv INAKULETEA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM

 

Usikose kufuatilia mubashara Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ushuhudie chama hicho kikipata Mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kufariki dunia mwezi uliopita.

Ni mubashara ndani ya Plus TV – DStv, Chaneli 294 siku ya Ijumaa 30 Aprili 2021, kuanzia saa 3 asubuhi.

BENKI YA NMB YAZINDUA MIKOPO YA PIKIPIKI KUPITIA KAMPENI YA 'NMB MASTABODA - MILIKI CHOMBO'

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akizindua rasmi Mkopo wa NMB Mastaboda wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na wa pili kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki hiyo, Filbert Mponzi na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha madereva wa Pikipiki Dar es Salaam, Michael Massawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa kwanza kulia), Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe wakipiga makofi baada ya uzinduzi rasmi wa Mkopo wa Mastaboda kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakiwa kwenye Pikipiki ya Magurudumu Matatu (Bajaji) baada ya kuzindua Mkopo wa Mastaboda kwenye Hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akiwa amepanda Pikipiki (Bodaboda) baada ya kuzindua Mikopo maalumu kwa madereva bodaboda nchini. kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na kushoto ni Dereva wa Bodaboda wa eneo la Kimara Suka, Beatrice Massawe.

Benki ya NMB imezindua Kampeni ya NMB MastaBoda 'Miliki Chombo,' inayotoa mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kwa watoa huduma wa Sekta ya Usafirishaji 'Bodaboda na Bajaj', ambako imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 5 za kufanikisha mikopo hiyo kwa mwaka wa kwanza.

Uzinduzi wa NMB MastaBoda Loan umefanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, ambaye awali Oktoba 2019, aliiomba NMB kufikiria namna ya kuwawezesha vijana wanaohudumu katika Sekta hiyo kote nchini.

Akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki yake ililipa uzito ombi la Waziri Mhagama na kwa nia ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuipatia suluhu changamoto ya ajira, ikaona ianzishe mikopo hiyo kwa maslahi mapana ya ustawi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

"Tumetenga kiasi cha Sh. Bilioni 5 kwa ajili ya NMB MastaBoda Loan katika mwaka huu wa kwanza na kukiwa na mwitikio mzuri miongoni mwa wakopaji, basi hatutosita kuongeza kiasi hicho ili kuwafikia walio wengi kote nchini. Wakopaji watakuwa na 'QR Code' za kupokelea malipo yao na kuingizwa moja kwa moja katika akaunti zao za NMB.

Monday, 26 April 2021

BENKI YA NMB YAKABIDHI ZAWADI KWA MSHINDI WA KAMPENI YA BONGE LA MPANGO

Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (katikati) akimkabidhi mshindi zawadi ya pikipiki ya magurudumu matatu - Paulina Moshi, mkazi wa mtaa wa ujenzi Halmashauri ya Mbulu Mkoani Manyara. NMB ilimkabidhi mshindi huyo wa kampeni ya Bonge la Mpango inayoendeshwa nchi nzima kwa wateja wanaofungua au kuweka fedha kwenye akaunti zao za NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Mbulu, Rogate Iranga.
Mshindi wa Bonge la Mpango, Paulina Moshi Mkazi wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara (mwenye tisheti yenye rangi ya chungwa) akishangilia pamoja na familia yake mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki ya magurudumu matatu kwenya hafla iliyofanyika Tawi la NMB Mbulu.


Mshindi wa kampeni ya Bonge la Mpango, Paulina Moshi akifurahia pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kuifikisha pikipiki hiyo aliyoshinda hadi nyumbani kwake.

Friday, 23 April 2021

DStv INAKULETEA VICHEKESHO KUPITIA CHANNEL 294

 


Kaa tayari, tunakuja kurekebisha mbavu zako moja kwa moja kupitia runinga yako LIVE on @dstvtanzania channel 294, @plustvtz.

@watubaki wanakuja kuongeza nuru na furaha ya kupokea mzigo wa mwisho wa mwezi, ni April 30 kuanzia saa 2:30 za usiku, Kaa Tayari.

Hakikisha unapiga *150*53# kulipia kifurushi Bomba TShs 19,900 tu kutazama vichekesho hivi.

#Watubaki

#ZaidiNaZaidi

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPELEKA WANAFUNZI WA KILIMO SHAMBANI KUJIFUNZA KWA VITENDO

Meneja wa shamba la Siverlands lililopo Ifunda Mkoani Iringa, WayneTraves (aliyechuchumaa) akiwaelekeza jambo kuhusu udongo wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda pamoja na wafanyakazi wa SBL ikiwamo Mkurugenzi Mtendaji, Mark Ocitti (aliyevaa kofia) walipotembelea shamba hilo.
Wanafunzi Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni ya Bia ya Serengeti unaojulikana kama Kilimo Viwanda wakijifunza kwa vitendo juu ya ukulima wa kisasa walipotembelea shamba la Silverlands lilipo Ifunda Mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda katika muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara katika shamba la Silverlands lililopo Ifunda Mkoani Iringa. Wengine kwenye picha ni wafanyakazi wa shamba hilo na wafanyakazi wa SBL.

Wanafunzi wanufaika wa mpango wa ufadhili wa masomo ya kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) maarufu kama Kilimo Viwanda kutoka katika chuo cha Mt. Maria Goretti wamepata fursa ya kuembelea shamba la Silverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa na kujinza ukulima wa kisasa.

Wanafunzi hao ambao waliambatana na waalimu wao waliungana na baadhi ya wafanyakazi wa SBL akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mark Ocitti, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma John Wanyancha na wafanyakazi wengine.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kampuni ya SBL imedhamiria kuendelea kutengeneza maisha bora kwa vijana na wakulima nchini kupitia programu yake ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi wanaotoka familia masikini kwenye vyuo vinavyofundisha kilimo.

WASHINDI GRANDE FINALE NMB MASTABATA WAKABIDHIWA TIKETI, ZAWADI ZAO

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi zawadi mshindi wa droo kuu ya MastaBata 'Si Kikawaida' Ally Abukari Ally ambaye ameshinda zawadi mbalimbali zikiwemo TV kubwa ya kisasa, friji kubwa na vifaa vingine vingi vyenye thamani ya sh milioni 7. Wengine ni maofisa waandamizi wa benki hiyo wakishuhudia tukio hilo. Sindano la MastaBata 'Si Kikawaida' lililenga kuhamasisha matumizi ya kadi kwenye manunuzi badala ya fedha taslimu. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi – Philbert Casmir (mwisho kushoto), Donatus Richard Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam (mwisho kulia) na Manfred Kayala Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi (anayemfuatia Meneja wa Kanda).

Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi tiketi ya ndege mshindi wa droo kuu ya MastaBata 'Si Kikawaida' Indra Pratap ambaye ameshinda safari ya kutembelea Mbuga ya Serengeti pamoja na mwenza wake ikiwa imelipiwa kila kitu. Wengine ni Manfred Kayala (kulia) Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi na Donatus Richard (katikati mwenye tai) Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishuhudia tukio hilo. Shindano la MastaBata 'Si Kikawaida' lililenga kuhamasisha matumizi ya kadi kwenye manunuzi badala ya fedha taslimu.

Washindi 12 wa zawadi kuu ‘Grande Finale’ ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Siyo Kikawaida’ wamekabidhiwa zawadi zao mbalimbali, zikiwemo tiketi za ndege tayari kwa safari za utalii wa ndani katika Mbuga za Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar.

Hafla ya kukabidhi zawadi na tiketi hizo imefanyika jijini Dar es Salaam, ambako washindi wawili na wenza wao walikabidhiwa tiketi za safari ya utalii katika Hifadhi za Taifa za Serengeti na Ngorongoro, huku wengine 10 wakikabidhiwa zawadi mbadala zenye thamani ya Sh. Mil. 7 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, alisema Kampeni ya NMB MastaBata iliyozinduliwa Novemba 24 mwaka jana, imemalizika kwa mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya watumiaji wa kadi na kwamba jumla ya washindi 436 tayari wamekabidhiwa zawadi mbalimbali.