Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 8 May 2021

BENKI YA CRDB YAKUSANYA WADAU KUJADILI UVUMBUZI KATIKA SEKTA YA FEDHA

Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe akiongoza Kongamano lililoandaliwa kwa kushirikiana kati ya Benki ya CRDB na Vodacom Tanzania na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma. Hii ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).

Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada wa Benki ya CRDB Ndugu Mangire Kibada akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.


Dodoma, Mei 06, 2021 – Benki ya CRDB imefanya kongamano lililobeba mada ya “Ni kwa namna gani sekta ya fedha inapaswa kuenenda kwa mwaka 2021?” ukizingatia dunia inapita katika changamoto ya janga la COVID-19 liloshika kasi mwaka 2020. Kongamano hilo lilioandliwa kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom liliongozwa na Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliasisiwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Akizungumza katika kongamano hilo, Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada za Benki ya CRDB, Mangire Kibada amaesema kuwa Benki ya CRDB imeamua kudhamini wiki ya uvumbuzi kwa kuwa inaamini katika kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja ambazo zinapatikana kwa njia ya kuwekeza katika uvumbuzi.

“Kwetu Benki ya CRDB tunaamini uvumbuzi ni kitu pekee ambacho kinaweza kututofautisha na wengine katika soko na hivyo kuifanya benki yetu kuendelea kuwa kinara sokoni kwa kuweza kutimiza mahitaji ya wateja wa makundi mbalimbali” alisema Kibanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuainisha na kupendekeza hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutengeneza na kutekeleza mipango ya uvumbuzi katika sekta ya fedha.



Kuhusu Benki ya CRDB


Benki ya CRDB ni moja benki zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, inatoa huduma kwa wateja wadogo, wakati na wakubwa ikiwamo huduma kwa wateja binafsi, huduma za hazina, huduma za bima, mikopo ya biashara, kilimo na uwezeshaji kwa wajasiriamali wadogo.

Benki ya CRDB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kuwa moja kati ya benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji. Moody’s imeipa Benki ya CRDB daraja la uimara la B1 ambapo ni daraja la juu zaidi kupatikana kwa mabenki na taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara. Benki ya CRDB imepata utambuzi wa Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UN Green Climate Fund) tangu mwaka 2019 na pia imetambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Global Finance kwa mwaka 2020.

Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania na Burundi kwa kuwahudumia wateja zaidi ya milioni 3 na kupitia mtandao mpana wa matawi 246, zaidi ya CRDB Wakala 19,000, 550 ATM, mashine za manunuzi 1,800 na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.

No comments:

Post a Comment