Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 23 April 2021

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPELEKA WANAFUNZI WA KILIMO SHAMBANI KUJIFUNZA KWA VITENDO

Meneja wa shamba la Siverlands lililopo Ifunda Mkoani Iringa, WayneTraves (aliyechuchumaa) akiwaelekeza jambo kuhusu udongo wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda pamoja na wafanyakazi wa SBL ikiwamo Mkurugenzi Mtendaji, Mark Ocitti (aliyevaa kofia) walipotembelea shamba hilo.
Wanafunzi Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni ya Bia ya Serengeti unaojulikana kama Kilimo Viwanda wakijifunza kwa vitendo juu ya ukulima wa kisasa walipotembelea shamba la Silverlands lilipo Ifunda Mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda katika muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara katika shamba la Silverlands lililopo Ifunda Mkoani Iringa. Wengine kwenye picha ni wafanyakazi wa shamba hilo na wafanyakazi wa SBL.

Wanafunzi wanufaika wa mpango wa ufadhili wa masomo ya kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) maarufu kama Kilimo Viwanda kutoka katika chuo cha Mt. Maria Goretti wamepata fursa ya kuembelea shamba la Silverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa na kujinza ukulima wa kisasa.

Wanafunzi hao ambao waliambatana na waalimu wao waliungana na baadhi ya wafanyakazi wa SBL akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mark Ocitti, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma John Wanyancha na wafanyakazi wengine.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kampuni ya SBL imedhamiria kuendelea kutengeneza maisha bora kwa vijana na wakulima nchini kupitia programu yake ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi wanaotoka familia masikini kwenye vyuo vinavyofundisha kilimo.

Programu hii iliyoanzishwa mwaka 2010 imesaidia wanafunzi 71 kusomea kozi za diploma katika ujuzi wa kilimo katika vyuo vinne kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Mark Ocitti.

Mkurugenzi huyo kuwa Kilimo Viwanda imelenga kusaidia wanafunzi kutoka familia masikini ili waweze kusomea masomo ya kilimo kwenye ngazi ya diploma katika vyuo vya ndani.

Wanafunzi wengine 43 chini ya programu hii wanapatikana Kaole Wazazi College of Agriculture (Bagamoyo), Kilacha Agriculture and Livestock Training Institute (Moshi) na Igabiro Training Insitute of Agriculture (Bukoba).

Ocitti alifafanua kuwa ufadhili huu unajumuisha malipo yote ya chuo na gharama zingine katika kipindi chao chote cha masomo. Vilevile, Kilimo Viwanda inalenga kuongeza nguvu jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa mashamba watakaowasaidia wakulima kuboresha mashamba yao. SBL inategemea kwa kiasi kikubwa mazao ya nafaka kama vile mtama, shayiri na mahindi katika uzalishaji wao.

Vilevile Ocitti alisema, ‘Programu hii ni fursa nzuri kwa wanafunzi kuongeza upeo wao kwa kujifunza kimatendo watakapotembelea mashamba makubwa ya wakulima wanaolima nafaka kama hizi pamoja na kutembelea viwanda vyetu vya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza ili kushuhudia namna kilimo na uzalishaji unavyotegemeana.’

No comments:

Post a Comment