Puma Energy imemtangaza Boaz Aywayo kuwa mshindi wa droo ya kampeni ya vilainishi, akiibuka na Elite Card yenye thamani ya Shilingi milioni 5, itakayomwezesha kufanya manunuzi ya vilainishi au gesi katika kituo chochote cha Puma nchini.
Mbali na zawadi hiyo kubwa, droo hiyo pia iliwapatia washindi wengine zawadi mbalimbali ikiwemo vilainishi na fedha taslimu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kampuni kuwashukuru na kuwazawadia wateja wake kwa uaminifu wao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Kitengo cha Oili wa Puma Energy, Matiko Bugumia, alisema droo hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni kuongeza thamani kwa wateja wake pamoja na kuhamasisha matumizi ya vilainishi halisi.
“Soko limekua kwa kasi, lakini changamoto ya bidhaa bandia bado ipo. Ndiyo maana Puma Energy inaendelea kutoa bidhaa bora na salama ili kulinda magari na vifaa vya wateja wetu,” alisema Bugumia.
Puma Energy imeendelea kuwekeza katika upanuzi wa huduma zake nchini, sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia vilainishi halisi vinavyotolewa kwenye vituo rasmi, ili kuepuka athari za bidhaa bandia ambazo zimekuwa zikiongezeka sokoni.
Kwa upande wake, mshindi wa droo, Boaz Aywayo, aliishukuru Puma Energy kwa kampeni hiyo na kuwataka watumiaji wengine kuhakikisha wanapatia bidhaa kwenye vituo vinavyoaminika.
“Bidhaa bandia ni changamoto, lakini Puma Energy imethibitisha kuwa chanzo cha bidhaa salama na zilizothibitishwa,” alisema Boaz.
.jpeg)
.jpeg)


No comments:
Post a Comment