Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 10 May 2021

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA MIFUKO 500 YA SARUJI MKOA WA KIGOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi (wanne kulia) akikabidhi msaada wa mifuko mia tano 500 ya saruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule mkoani humo. Mifuko hiyo ilipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchatta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Nd Thobias Adengenye. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma.

Benki ya Taifa ya Biashara imekabidhi mifuko 500 ya seruji kwa Mkoa wa Kigoma kusaidia juhudi za serikali za ujenzi wa madarasa mkoani humo. Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchata akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Thobias Andengeye pamoja na kuishukuru Benki ya NBC alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa kutokana na muamko wa wazazi wa Kigoma kupeleka watoto shule kufuatia maamuzi ya serikali kutoa elimu bure.

“Tunategemea wanafunzi wapatao 40,771 kuhitimu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 kuepelekea uhitaji wa madarasa ziaidi ya 1,010 huku mkoa wetu ukiwa na madarasa 405, hivyo mchango wa Benki ya NBC wa mifuko 500 ya saruji utaisaidia kusukuma malengo serikali yetu ya mkoa kukamilisha ujenzi wa madarasa zaidi ya 605.” Alisema Nd Mchata.

Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd Theobald Sami alisema kuwa msaada huo wa mifuko 500 ya seruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 ni kielelezo kidogo tu cha dhamira ya dhati ya kurudisha kwa jamii kiasi cha faida inayopatikana kutokana na kuwahudumia Watanzania.

“Sera yetu ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii inayotuzunguka inaangalia maeneo ya elimu, afya na ustawi wa jamii kama nguzo kuu. Ni kweli mchango wetu huu haitamaliza changamoto ya vyumba vya madarasa lakini nia yetu kama taasisi ya biashara ni kuendelea kurudisha sehemu ya faida kwa jamii hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali ya mkoa katika juhudi mbali mbali za kutatua changamoto katika jamii, huu si mwanzo bali ni muendelezo.” Alisema Nd Theobald Sabi.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Nd Joseph K Rwiza ambaye wilaya yake ni moja kati wa wilaya nufaika wa msaada huo ameishukuru Benki ya NBC kwa mchango wao. Pia alieleza kwamba serikali ya wilaya yake itaunganisha nguvu za bajeti pamoja wananchi na wadau wengine kuhakikisha kwamba changamoto ya uhaba wa madarasa inakuwa historia katika wilaya yake.

No comments:

Post a Comment