Blog Rebranding Teaser_030826
Stanbic Bank Banner_070826
Absa Loan Campaign_160426
Wednesday, 22 May 2019
FARMING GETS 127BN/- IFAD BOOST
The International Fund for Agricultural Development (IFAD) has allocated over 127bn/- to support agricultural projects in the country for the three-year period effective next year.
Read More >>
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SERIKALI KIASI CHA SHILINGI BILIONI MBILI (2.1) KUTOKA SHIRIKA LA MAWASILIANO TANZANIA TTCL JIJINI DAR ES SALAAM MEI, 21 2019
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu uzalendo na kuunga mkono Shirika la Mawasiliano TTCL jijini Dar es Salaam. |
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA MAENDELEO WA SWEDEN MHE PETER ERIKKSON IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 20, 2019
Ikulu Blog
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA DKT. MPOKI ULISUBISYA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MEI 20, 2019
Bofya hapa kwa picha zaidi
AGRICULTURE BANK PROVING A BOON TO FARMING SECTOR
![]() |
| Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), Managing Director, Mr. Japhet Justine. |
Read More >>
BARCLAYS BANK TANZANIA ORGANISES AN IFTAR DINNER FOR CUSTOMERS IN DAR ES SALAAM
| Dar es Salaam Regional Sheikh, Alhad Mussa Salum addresses invited guests during an iftar hosted by Barclays Bank Tanzania for its customers in Dar es Salaam over the weekend. |
| Barclays Bank Citizenship Manager, Hellen Siria (right) serves an iftar meal to some invitees at a function hosted by the bank for its customers in Dar es Salaam. |
| Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (centre), together with some invited guests, breaking the fast at an occasion hosted by the bank for its customers in Dar es Salaam recently. |
| Some invite guests breaking the fast at an occasion hosted by Barclays Bank Tanzania in Dar es Salaam recently. |
TANZANIA NA UHOLANZI ZAZINDUA MRADI WA KUKUA NA KUKU
![]() |
| Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (pichani juu) na Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Bibi Lianne Houben (pichani chini) wakitoa hotuba fupi wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Kukua Na Kuku huko Kilacha, Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Bofya hapa kwa picha zaidi |
Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Uholanzi na Africa (Netherlands – Africa Business Council - NABC) hivi karibuni waliongoza ujumbe wa Makampuni 7 kutoka Uholanzi yaliyobobea katika Sekta ya Ufugaji wa Kuku kwenda Mkoani Kilimanjaro kuzindua Mradi maalum wa ufugaji utakaoendeshwa na Makampuni hayo nchini Tanzania maarufu kama “Kukua Na Kuku (Growing with Chicken) Impact Cluster”.
Mradi wa “Kukua Na Kuku” ni matokeo ya makubaliano ya kuanzisha ubia kati ya Tanzania na Uholanzi yanayolenga kuboresha Sekta ya Ufugaji Kuku nchini Tanzania na kuifanya kuwa endelevu kwa kutumia teknolojia ya kisasa kutoka Uholanzi. Makampuni hayo yatatoa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo wafugaji wazawa kwa kuboresha usimamizi wa kilimo cha ufugaji, afya ya wanyama, upatikanaji wa chakula (lishe) bora kwa ajili ya mifugo, vifaa muhimu vya kufugia, na hata utafutaji masoko.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Chuo cha Kilimo na Ufugaji wa Mifugo Kilacha, Mkoani Kilimanjaro kwa kusaini Makubaliano ya Ushirikiano, na ukawa ndio mwanzo wa ushirikiano wa miaka 3 kati ya makampuni hayo 7, Serikali ya Uholanzi na wadau wazawa wa Tanzania. Chuo cha Kilimo na Ufugaji wa Mifugo cha Kilacha kinasimamiwa na Kituo cha Uzalishaji na Mafunzo kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Mkoani humo.
Mgeni rasmi wakati wa sherehe za uzinduzi huo alikuwa Mhe. Anna Mgwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju,Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bibi Lianne Houben, na Mkurugenzi wa Biashara na Kilimo wa NABC, Bw. Mackenzie Masaki.
Makampuni hayo kutoka Uholanzi ni pamoja na: Aeres University of Applied Sciences; Ebit+/I Grow Chicken; GD Animal Health; Impex; Hendrix Genetics; Koudijs de Heus; na Vencomatic Group.
|
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Monday, 20 May 2019
CRDB BANK HOLDS A SHAREHOLDERS SEMINAR IN ARUSHA
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA SEMINA YA WANAHISA WA BENKI YA CRDB, JIJINI ARUSHA
![]() |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. |
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. |
Bofya hapa kwa picha zaidi
Sunday, 19 May 2019
Saturday, 18 May 2019
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFRICAN DEVELOPMENT BANK - AfDB) DKT. AKINWUMI ADESINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, 15 MEI 2019
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhe. Dkt. Akinwumi Adesina ameipongeza Tanzania kwa ukuaji mzuri wa uchumi wa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka na hivyo kuendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kubwa Duniani.
Mhe. Dkt. Adesina ametoa pongezi hizo tarehe 15 Mei, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ushirikiano kati ya benki hiyo na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.
Mhe. Dkt. Adesina amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa dhamira yake njema na msimamo wake wa kuwapigania Watanzania na amemtaka kuendelea na mwelekeo huo ambao umeendelea kuimarisha uchumi kwa ukuaji wa wastani wa asilimia 7 ikilinganishwa na wastani wa ukuaji wa uchumi wa dunia wa asilimia 3.5.
Halikadhalika amempongeza kwa ushirikiano na nchi jirani kama vile Uganda na hivyo kufanikisha ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi lenye urefu wa kilometa 1,443 kati ya Hoima nchini Uganda na bandari ya Tanga nchini Tanzania kwa kushirikisha sekta binafsi.
Aidha, Mhe. Dkt. Adesina amesema wamezungumzia kuhusu kilimo na kwamba AfDB ipo tayari kusaidia kutatua tatizo la masoko ya mazao yanayozalishwa katika kanda mbalimbali za Tanzania na kuongeza thamani.
Kuhusu miradi mingine ya maendeleo amesema kwa hivi sasa AfDB imetoa ufadhili kwa miradi yenye thamani ya shilingi Trilioni 4.55 na kwamba hivi karibuni benki hiyo imeidhinisha ufadhili kwa miradi ya ujenzi wa barabara za mzunguko (ring road) za Jiji la Dodoma zenye urefu wa kilometa 110, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato Mkoani Dodoma, na pia ameipongeza Tanzania kwa kuanza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa kati ya Dar es Salaam na Dodoma kwa kutumia fedha zake na ameahidi kuwa benki hiyo itaunga mkono mradi huo hasa kwa ujenzi wa kuanzia Isaka kwenda Kigali nchini Rwanda na hivyo kunufaisha nchi nyingine za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa upande wake, Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Dkt. Adesina kwa ushirikiano mkubwa ambao AfDB inautoa kwa Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania itahakikishia fedha zinazotolewa na benki hiyo zinatekeleza miradi iliyokusudiwa kwa uhakika na inaleta matokeo yanayotarajiwa.
Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na miradi hiyo AfDB pia imekubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ya Mpanda – Tabora yenye urefu wa kilometa 359, kujenga awamu ya pili ya mradi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) kati ya Kariakoo na Mbagala Jijini Dar es Salaam na kujenga njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 400 kati ya Sumbawanga – Mpanda – Kigoma – Nyakanazi.
Kuhusu AfDB kusaidia ujenzi wa reli ya kati kwa kipande cha kuanzia Isaka mpaka Kigali Mhe. Rais Magufuli amesema ufadhili huo utasaidia kuharakisha usafirishaji wa madini yaliyopo katika kanda ya kati na magharibi mwa Tanzania.

Subscribe to:
Posts (Atom)