Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Grooveback Advert_210725

Grooveback Advert_210725

Tuesday, 22 July 2025

CRDB BANK TARGETS 40% GROWTH IN ONLINE ENTREPRENEUR TRAINING THROUGH INSTAPRENYUA SEMINAR

CRDB’s Acting Director of Retail and SME Banking, Muhumuliza Buberwa (left) and Head of Marketing, Joseline Kamuhanda, speak at a press conference in Dar es Salaam yesterday.

DAR ES SALAAM: CRDB Bank is aiming for a 40 per cent increase in the number of online entrepreneurs trained through its flagship Instaprenyua seminar, as part of its broader mission to equip digital business owners with critical skills and growth opportunities.

The bank, one of Tanzania’s leading financial institutions, announced that the fourth season of the seminar targets training 700 online entrepreneurs—up from 500 trained during the third season.

CRDB’s Acting Director of Retail and SME Banking, Muhumuliza Buberwa, said the program will focus on key areas such as online business information security and the adoption of modern digital payment solutions.

“Today, thousands of Tanzanians are earning an income through online businesses. Transactions worth billions of shillings are completed daily through digital platforms,” Mr Buberwa told reporters on Monday.

Launched in 2022, the Instaprenyua seminar has already empowered over 3,000 entrepreneurs with skills in leveraging social media platforms, securing digital transactions, and accessing modern payment systems.

Mr Buberwa emphasized that CRDB recognises the growing importance of online business in Tanzania’s economy and sees it as crucial to support these entrepreneurs with both knowledge and access to banking and social opportunities.

“The seminar is designed to equip participants with practical digital business skills and link them to new markets and funding opportunities,” he said.

This year’s edition has been refreshed to reflect the evolving landscape of online business. Participants will benefit from interactive sessions led by experts in digital commerce, fintech, and e-marketing.

Monday, 21 July 2025

ABSA GROUP CEO VISITS TANZANIA TO DEEPEN CUSTOMER-CENTRIC GROWTH STRATEGY

Absa Group Chief Executive Officer, Kenny Fihla (third from left), is pictured with (from left): Obedi S. Laiser – Managing Director, Absa Bank Tanzania; Savior Chibiya – Chief Executive, Absa Regional Operations; and Nicholous Mukanya – Branch Manager, Ohio Branch, in Dar es Salaam today.

Dar es Salaam, Tanzania – 21 July 2025 – The Group Chief Executive Officer of Absa, Kenny Fihla, has concluded a significant visit to Tanzania, marking a major step in the bank’s broader East African engagement strategy. His tour reflects Absa’s commitment to regional growth, sustainable financial inclusion, and placing customers at the heart of its operations.

The visit reaffirms Tanzania’s growing importance within Absa’s regional network. With the country’s GDP projected to grow at 6.1% in 2025, and notable momentum in sectors like ICT, energy, and mining, Absa views Tanzania as a key driver of its inclusive and digital banking agenda.

During his time in Tanzania, Mr. Fihla met with an array of stakeholders – from customers and clients to regulators and staff – focusing on enhancing customer experience, strategic capital deployment, and aligning with Tanzania’s national development priorities.

“Tanzania is a market of immense potential, and our presence here must reflect more than just financial services – it must reflect partnership, purpose, and progress,” said Mr. Fihla. “We are here to build lasting relationships and grow with the communities we serve.”

This visit marks the first leg of Mr. Fihla’s regional roadshow since assuming the role of Group CEO on 17 June 2025. It also supports Absa’s Pan-African growth strategy, focusing on digital innovation, small business support, and sustainability.

Stakeholder Confidence and Strategic Alignment

Absa’s leadership team used the visit to deepen conversations around financial innovation, trade finance, youth empowerment, and the role of fintech in Tanzania’s economic transformation. Internal engagements also emphasized the Group’s values and long-term priorities.

Mr. Obedi Laiser, Managing Director of Absa Bank Tanzania, noted:
“His visit reaffirms the strategic importance of the Tanzanian market within Absa Group’s pan-African footprint. At Absa Bank Tanzania, we are deeply committed to making a real impact through innovation, inclusion, and stakeholder partnerships.”

BENKI YA NBC YAKUTANA NA WATEJA WAKE WAKUBWA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bw. Elvis Ndunguru (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo maofisa na wateja jijini Arusha, wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbalimbali (corporates). Hafla hiyo ililenga kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya, pamoja na kuwaongezea wateja uelewa kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Tukio hilo liliandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo na kufanyika jana jioni jijini Arusha.

Arusha, Julai 21, 2025 — Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa kutoka mashirika binafsi, taasisi mbalimbali, na wateja wa kawaida (corporates) jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kuwasilisha huduma mpya za benki hiyo, na kuwajengea wateja uelewa mpana juu ya faida na manufaa ya huduma hizo. Aidha, benki hiyo ilitumia fursa hiyo kupata mrejesho wa moja kwa moja kuhusu jinsi ya kuendelea kuboresha huduma zake ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja wake.

Katika kufanikisha hilo, NBC kupitia kitengo chake cha Biashara na Uwekezaji (CIB) iliandaa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa NBC, Bw. Elvis Ndunguru, akiwa ameambatana na maofisa waandamizi kutoka makao makuu na matawi ya benki hiyo jijini Arusha.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw. Ndunguru alisema tukio hilo ni sehemu ya jitihada endelevu za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja wake, hasa kwa kutambulisha huduma mpya kama NBC Connect, ambayo imelenga kuleta suluhisho la kifedha kwa kundi hilo la wateja.

“Tukiwa kama muhimili muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayoletwa na ubunifu wa kiteknolojia tunaoendelea kuufanya kila siku,” alisema Bw. Ndunguru.

Aliongeza kuwa kupitia hafla hiyo, benki ilielezea maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye huduma zake pamoja na kuzindua huduma mpya zilizo rahisi na za kidigitali, zinazokidhi mahitaji ya wateja wakubwa wa taasisi hiyo.

Huduma ya NBC Connect ilielezwa kuwa ni sehemu ya mpango mpana wa benki hiyo wa kuwasogezea huduma karibu zaidi wateja wa kada ya juu, wakiwemo mashirika binafsi, taasisi za serikali, na makampuni makubwa.

VISA EXPANDS PRESENCE IN EAST AFRICA WITH NEW OFFICE IN TANZANIA

Visa’s General Manager for Southern and Eastern Africa, Michael Berner (right), presents a gift to the Governor of the Bank of Tanzania, Emmanuel Tutuba, during the inauguration ceremony of the company’s office held in Dar es Salaam on July 16, 2025.
The Governor of the Bank of Tanzania, Emmanuel Tutuba (right), and Visa’s General Manager for Southern and Eastern Africa, Michael Berner (left), arrive at the venue to attend the inauguration ceremony of the company’s office held in Dar es Salaam on July 16, 2025.

Visa Day event held to mark crucial regional growth milestone

Dar es Salaam, 16 July 2025 - Visa (NYSE: V), a global leader in digital payments has officially opened its new office in Tanzania, marking a significant milestone in its commitment to advancing financial inclusion and digital transformation across East Africa.

The announcement coincided with the inaugural Visa Day Tanzania, event themed “Shaping the Future of Payments in Tanzania”, held in Dar es Salaam.

The new office will serve as a regional hub, supporting operations in Tanzania, Uganda, Burundi, and Rwanda, and will be led by recently appointed Country Manager Victor Makere, a Tanzanian national with deep expertise in the region’s financial landscape. 

Tanzania is one of the most dynamic and promising markets in Africa when it comes to digital payments,” said Michael Berner, Head of Southern and Eastern Africa at Visa. “With increasing mobile and internet penetration, a vibrant SME sector, and a strong push for financial inclusion, we see tremendous opportunity to partner with local stakeholders to shape a more inclusive and innovative payments ecosystem.” 

Sunday, 20 July 2025

EUROMONEY YAITANGAZA BENKI YA STANBIC KUWA BENKI BORA YA UWEKEZAJI

🏆 Tuzo ya heshima kwa mchango wa Benki ya Stanbic katika uchumi wa Taifa

Dar es Salaam, 18 Julai 2025 – Benki ya Stanbic Tanzania imetangazwa kuwa Benki Bora ya Uwekezaji Tanzania katika Tuzo za Ubora za Euromoney 2025, tukio linalotambua juhudi zake katika kuchochea uwekezaji, ajira, na ukuaji wa uchumi wa muda mrefu.

Tuzo hii inaonesha mafanikio ya benki hiyo katika:

  • Kuwezesha miradi mikubwa ya maendeleo
  • Kukuza viwanda vya ndani
  • Kuongeza fursa za ajira na mauzo nje ya nchi

“Tuzo hii si kwa ajili ya kutambulika tu, bali kwa thamani tunayoileta kwa Taifa,”
— Manzi Rwegasira, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Stanbic Tanzania


💼 Miradi ya Uwekezaji Yenye Mvuto Mkubwa

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Benki ya Stanbic:

  • Ilishiriki katika miamala ya kimkakati iliyosaidia viwanda kupanua uzalishaji
  • Ilichangia mitaji kwa wawekezaji wa muda mrefu
  • Iliimarisha miundombinu ya kifedha kwa kusaidia taasisi nyeti

VODACOM, JUBILEE ALLIANZ WAJIPANGA ‘KUINOGESHA’ NBC DODOMA MARATHON

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. Nguvu Kamando (katikati), pamoja na maofisa waandamizi wa taasisi hizo, akiwemo Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Bw. Godwin Semunyu (kulia), wakionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma, wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Julai 18, 2025 – Wadhamini wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania, wamesisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ili kuhakikisha zinafikia malengo ya kijamii huku zikileta hamasa na furaha kwa washiriki.

Dhamira hiyo imeelezwa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya maofisa wa benki ya NBC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha Bw Rayson Foya, waliotembelea makao makuu ya kampuni hizo kwa lengo la kukabidhi jezi maalum na vifaa vya mbio kwa washiriki – ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika msimu wa sita wa marathon hiyo.

Mbio za NBC Dodoma Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, 2025, jijini Dodoma, mwaka huu zinalenga kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili kwa wakunga 200, na kuanzisha mpango wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism).

Katika ziara yao, Bw Foya na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa NBC, Bw Godwin Semunyu, walikabidhi vifaa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Allianz Tanzania Bw Jaideep Goel, na kisha kuendelea na ziara kwa Vodacom Tanzania ambapo walipokelewa na maofisa waandamizi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara Bw Nguvu Kamando.

CRDB BANK YATWAA TUZO TATU KUBWA ZA EUROMONEY 2025 JIJINI LONDON

 

London / Dar es Salaam, 20 Julai 2025 – Benki ya CRDB imetangazwa kuwa Benki Bora TanzaniaBenki Bora kwa Masuala ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG), na Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati (SME) na jarida la kifedha la kimataifa la Euromoney. Tuzo hizi zilitolewa wakati wa hafla ya Tuzo za Ubora za Euromoney iliyofanyika jijini London, Julai 17, 2025.

Kutwaa tuzo hizi tatu ni uthibitisho wa dhamira ya Benki ya CRDB kukuza maendeleo jumuishi, uwajibikaji wa kifedha, na maendeleo endelevu kwa kipindi cha miaka 30 ya utendaji wake sokoni.

Tuzo hizo zilipokelewa na Bi. Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, kwa niaba ya benki katika hafla iliyohudhuriwa na zaidi ya wataalamu 500 wa sekta ya fedha duniani. Aliongozana na maofisa waandamizi wa CRDB pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Tuzo hizi zimejumuishwa na ile ya hivi karibuni ambapo Benki ya CRDB ilitambuliwa na Euromoney kuwa Benki Bora kwa huduma za benki za Kiislamu nchini Tanzania kupitia huduma zake za CRDB Al Barakah Banking (Dubai, Mei 20, 2025).

Kwa pamoja, tuzo hizi nne zinaonyesha mtazamo mpana wa kimkakati wa Benki ya CRDB katika:

  • Uwezeshaji wa upatikanaji wa fedha;
  • Kukuza biashara endelevu;
  • Kuwezesha wananchi katika masoko inayohudumia.

Zimekuja wakati muhimu ambapo Benki ya CRDB inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, ikiendelea kuwa kiungo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

Kauli ya Bi. Tully Esther Mwambapa

"Heshima hii ya tuzo nne kutoka Euromoney inadhihirisha dhamira ya msingi ya Benki yetu ya kuwa mshirika wa kweli wa maendeleo kwa watu binafsi, wafanyabiashara, na jamii kwa ujumla. Tunapoendelea na kuadhimisha miaka 30 ya Benki ya CRDB, tuzo hizi zinatupa chachu ya kuendelea kusimamia kusudi letu la kuboresha maisha na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu katika uendeshaji wetu."

Friday, 18 July 2025

STANBIC YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MKOPO WA KIDIJITALI "JIWEZESHE" KWA WATANZANIA WOTE

Mkuu wa Kitengo cha Kidijitali na Biashara Mtandao wa Benki ya Stanbic, Edward Balandya, akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa huduma ya mkopo wa kidijitali "Cash Advance", inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Benki kwa Wateja Binafsi, Emmanuel Mahodanga, na kulia ni Meneja wa Mifumo ya Kidijitali wa benki hiyo, Godlisten Shirima.

📍 Dar es Salaam, Tanzania – 16 Julai 2025
Na Mwandishi Wetu

Katika jitihada za kuendeleza ujumuishaji wa kifedha na matumizi ya teknolojia, Stanbic Bank Tanzania imezindua rasmi huduma ya mkopo wa kidijitali inayojulikana kama JIWEZESHE, ikiwa ni suluhisho jipya la kifedha linalowalenga Watanzania wa kada mbalimbali, hususan wale wasio na ajira rasmi lakini wenye kipato cha uhakika.

💳 Mikopo Kupitia Simu Bila Dhamana

Huduma hii mpya inatoa fursa ya kupata mikopo kuanzia TZS 50,000 hadi TZS 5,000,000 kwa wateja wa mishahara na hadi TZS 2,500,000 kwa wale wasio na ajira rasmi, kulingana na historia ya mapato inayoingia kwenye akaunti zao za Stanbic kwa miezi sita mfululizo.

“JIWEZESHE inamuwezesha mteja kupata fedha papo kwa papo, bila dhamana, na kwa usalama wa hali ya juu kupitia mfumo wetu wa kidijitali,” alisema Edward Balandya, Mkuu wa Kitengo cha Kidijitali na Biashara Mtandao.

Mfumo huu umetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayochambua mwenendo wa mapato ya mteja, hivyo kufanya mchakato wa uidhinishaji wa mkopo kuwa wa haraka na bila urasimu.

👥 Kila Mtanzania Anaweza Kufikiwa

Kwa mujibu wa Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Kitengo cha Benki kwa Wateja Binafsi, JIWEZESHE ni sehemu ya dhamira ya Stanbic Bank kujenga jukwaa la kifedha jumuishi.

“Kupitia JIWEZESHE, tunasema sasa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma. Watu wanaofanya kazi halali na kupata kipato, lakini wamekuwa nje ya mfumo rasmi wa kifedha, sasa wanapata nafasi ya kujikwamua,” alisema Mahodanga.

Huduma hii inalenga kuwasaidia watu kukabiliana na changamoto za kifedha za dharura kama ada za shule, gharama za afya, au mtaji wa kuendeleza biashara ndogo.

📲 Rahisi, Haraka, na Salama

Kwa mujibu wa Godlisten Shirima, Meneja wa Mifumo ya Kidijitali, huduma ya JIWEZESHE inaweza kupatikana moja kwa moja kupitia Stanbic Bank App au tovuti rasmi ya benki, bila kutembelea tawi, bila dhamana, wala mdhamini.

“Hii ni huduma ya kisasa inayozingatia kasi ya maisha ya sasa. Wateja wanaweza kufungua akaunti na kuomba mkopo papo hapo,” alisema Shirima.

Thursday, 17 July 2025

NBC YAKABIDHI ‘KITS’ ZA NBC DODOMA MARATHON KWA UONGOZI WA GSM GROUP

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (wa pili kushoto), sambamba na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Group, Bw. Gharib Said Mohamed (GSM) (katikati), Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM Group, Mhandisi Hersi Said (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya GSM Group, Bi. Chenedzo Mupukuta, na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa NBC, Bw. Godwin Semunyu (kulia), wakionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma, wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Julai 18, 2025 – Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambao ndio waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, leo imeendelea na maandalizi ya kuelekea mbio hizo kwa kukabidhi rasmi jezi na vifaa maalum kwa mmoja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo, kampuni ya GSM Group.

Kupitia kampuni tanzu ya GSM Beverages, GSM Group inadhamini huduma ya maji na vinywaji baridi kwa washiriki wa mbio hizo za sita ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 27 Julai 2025, jijini Dodoma.

Mbali na udhamini wa maji, GSM Foundation—taasisi ya kijamii ya GSM Group—ni mfadhili mkuu wa ajenda tatu muhimu za kijamii zinazoratibiwa na mbio hizi mwaka huu:

  • Kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake,
  • Kufadhili wakunga hadi kufikia idadi ya wakunga 200,
  • Kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 watakaotoa huduma kwa watoto wenye changamoto ya usonji (autism).

Ujumbe kutoka NBC uliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Rayson Foya, akiambatana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Bw. Godwin Semunyu, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bi. Tatiana Massimba.

Walipokelewa katika makao makuu ya GSM Group jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa GSM Group, Bw. Gharib Said Mohamed (GSM), pamoja na viongozi wengine waandamizi akiwemo Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mhandisi Hersi Said, Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Chenedzo Mupukuta, na maofisa wengine wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bw. Foya aliishukuru kampuni ya GSM Group kwa kuwa mdau muhimu wa mbio hizo, akisisitiza mchango wao mkubwa katika kufanikisha malengo ya kijamii kupitia mbio hizi.

“Tupo hapa kukabidhi vifaa hivi kama ishara ya kutambua na kuthamini mchango wa GSM Group kwenye mafanikio ya NBC Dodoma Marathon. Mbali na kutoa maji na vinywaji kwa washiriki zaidi ya 12,000, GSM kupitia Foundation yao wamechukua jukumu kubwa zaidi katika kufanikisha ajenda zetu tatu kuu zinazogusa afya ya mama na mtoto na changamoto za watoto wenye usonji,” alisema Bw. Foya.

NMB BANK EXECUTIVES ATTEND LAUNCH OF TANZANIA DEVELOPMENT VISION 2050

DODOMA, July 17, 2025 – Senior leaders from NMB Bank Plc, led by the Chairman of the Board of Directors, CPA David Carol Nchimbi (right), attended the official launch of the Tanzania Development Vision 2050, held at the Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) in Dodoma.

The launch event was presided over by Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, and brought together high-ranking government officials, private sector leaders, and development partners from both within and outside the country.

As a key player in Tanzania’s economic development, NMB Bank reaffirmed its commitment to supporting the successful implementation of this long-term national strategy, which aims to transform Tanzania into an inclusive, competitive, and sustainable upper-middle-income country by the year 2050.

“We recognize the importance of aligning with national priorities and remain steadfast in playing our role in driving inclusive growth, innovation, and financial empowerment,” said a representative from the Bank.


📌 Follow our blog for more updates on policy developments, economic milestones, and NMB Bank’s continued contribution to Tanzania’s progress.


NMB YAKUTANA NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU KUIMARISHA UBORA WA HUDUMA KWA WATEJA

Dar es Salaam, Tanzania – Benki ya NMB kwa mara nyingine imeonyesha dhamira yake ya kushirikiana na taasisi za serikali katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, baada ya kuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAG), ulioongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno.

Katika kikao kilichofanyika katika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, ujumbe wa OAG ulipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, pamoja na viongozi waandamizi wa benki hiyo. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili, hasa katika maeneo ya kubadilishana uzoefu, mbinu bora za utoaji huduma kwa wateja, na matumizi ya TEHAMA katika sekta ya huduma.

Ujumbe wa OAG ulihusisha pia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo:

  • Bw. Ipyana Mlilo – Mkurugenzi Msaidizi, Uratibu
  • Bi. Leila Muhaji – Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Bw. Juma Mziray – Afisa TEHAMA Mwandamizi
  • Bw. Nyamhanga Nyamhanga – Wakili wa Serikali

Katika mazungumzo yao, viongozi wa pande zote walisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuongeza ufanisi wa utoaji huduma na kuchochea maendeleo jumuishi kwa jamii nzima.

“Ushirikiano kama huu unasaidia kuimarisha utawala bora, kuongeza uwazi, na kutumia teknolojia kuharakisha huduma kwa wananchi,” ilielezwa na mmoja wa washiriki wa kikao hicho.

CRDB BANK SHARES CROSS 1,000/- MARK IN HISTORIC MARKET MILESTONE

Dar es Salaam, Tanzania – CRDB Bank Plc has made history by surpassing the 1,000/- share price mark on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) for the first time—representing a tenfold increase from its price just six years ago.

To many investors, this milestone is more than just psychological; it signals a strategic triumph rooted in sound execution, resilience, and long-term vision.

“This is not just a psychological mark. It’s a strategic landmark that reflects six years of solid fundamentals, investor trust, and Tanzania’s maturing banking sector,” said Isaac Lubeja, Advisory and Research Manager at Zan Securities.


From 100/- to 1,000/-: The Numbers Behind the Surge

In 2019, CRDB’s share traded at 100/-, with a market capitalisation of TZS 261.18 billion and an annual profit of TZS 120.1 billion.

Fast forward to today, the share price stands at 1,000/-, up from 670/- in January, propelling the bank’s market cap to TZS 2.611 trillion. The bank also reported a 2024 profit of TZS 551.8 billion—an almost fivefold increase.

So far in 2025 alone, the stock has gained 49% in price appreciation and delivered a total return of 58.9%, including dividends.

“This performance reflects not short-term volatility, but rather sustained consistency driven by strong operational results,” Mr. Lubeja noted.


Consistent Growth Driven by Fundamentals

Between 2020 and 2024, CRDB posted an impressive 30% compound annual growth rate (CAGR) in profits. Last year alone, it achieved:

  • Return on Equity (ROE): 27.7%
  • Return on Assets (ROA): 5.1%
  • Cost-to-Income Ratio: Improved to 45.9% from 49.5%

These gains are largely attributed to the bank’s digital transformation, cost efficiency, and expansion scale.

CRDB’s diversification strategy is also bearing fruit, with nearly one-third of its income now derived from non-interest sources such as fees, commissions, and foreign exchange—a vital buffer in fluctuating interest rate environments.

AKIBA COMMERCIAL BANK STRENGTHENS CUSTOMER ENGAGEMENT IN MOSHI

Akiba Commercial Bank Managing Director, Mr. Silvest Arumasi, opens the Customer Engagement Forum in Moshi.

Date: 16th July 2025
Location: Moshi, Tanzania

Akiba Commercial Bank Plc (ACB) continues to affirm its commitment to being a customer-centric institution by hosting a special engagement forum with its customers in Moshi on 16th July 2025. The event, held in the heart of Kilimanjaro region, was graced by the Bank’s Managing Director, Mr. Silvest Arumasi.

Ms. Florentina Manyilunzi, the new ACB Branch Manager of Moshi, was officially introduced to customers during the meeting.

The customer forum served as an important platform for open dialogue between the Bank and its clients. It brought together a cross-section of customers from the Moshi area, creating a space where they could offer feedback, learn about recent bank initiatives, and gain financial education—all under one roof.

In his address, Mr. Arumasi underscored the importance of customer feedback in shaping the Bank’s services:

“At ACB, being customer-centric is not just a principle—it’s a practice. We value your feedback, and we are committed to translating it into real action,” he emphasized.

Participants shared personal success stories of their journeys with ACB, citing how the Bank’s support had contributed to their financial growth. They also offered constructive suggestions to enhance service delivery, which the Bank welcomed as part of its continuous improvement strategy.

CRDB BANK GROUP APPOINTS PROF. NEEMA MUNISI MORI AS BOARD CHAIRPERSON

Dar es Salaam, 15 July 2025 – The Board of Directors of CRDB Bank Plc is pleased to announce the appointment of Prof. Neema Munisi Mori as Board Chairperson, and Dr. Donald Eliapenda Mmari as Vice Chairperson of the Board of CRDB Bank Group.

These appointments reaffirm the Bank’s ongoing commitment to exemplary corporate governanceinclusive leadership, and sustainable growth across the region.


Prof. Neema Munisi Mori – Board Chairperson

Prof. Mori is a seasoned academic, visionary leader, and corporate governance expert with over 20 years of experience in finance, banking, entrepreneurship, and leadership development. She currently serves as an Associate Professor of Finance and Director of Public Services at the University of Dar es Salaam.

Her contribution to CRDB Bank has been instrumental, having previously served as:

  • Vice Chairperson of the Board
  • Chairperson of the Credit Committee
  • Member of the Risk Committee
  • Member of the Governance, Nomination and Human Resources Committee

Beyond CRDB, Prof. Mori also serves as Chairperson of the Board for BRELA and Air Tanzania Company Ltd, and is a founding member of several programs aimed at empowering youth and women in leadership and business. She is a widely published researcher in international journals and is highly regarded as a mentor in business, finance, and entrepreneurship.

Her academic credentials include:

  • PhD in International Business – University of Agder, Norway
  • MBA and Bachelor’s in Finance – University of Dar es Salaam
  • Certification in Company Direction – Institute of Directors (UK)

Prof. Mori brings to the role a unique blend of scholarly depth, governance acumen, and a passion for sustainable development in Africa’s financial sector.


Dr. Donald Eliapenda Mmari – Vice Chairperson

Dr. Mmari is a distinguished economist and institutional strategist with over 30 years of experience in economic researchpolicy development, and corporate leadership. He currently serves as the Executive Director of REPOA, a leading Tanzanian think tank focused on socio-economic transformation.

Wednesday, 16 July 2025

NBC YAZINDUA RASMI JEZI ZA NBC DODOMA MARATHON 2025, YAKABIDHI KWA WADHAMINI

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (wa tatu kushoto), akikabidhi moja ya jezi maalum za mbio za NBC Dodoma Marathon kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw. Julius Magabe (wa tatu kulia), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini muhimu wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma. Wengine katika picha ni maofisa waandamizi wa kampuni hizo.

Dar es Salaam, Julai 16, 2025 – Katika kuendeleza maandalizi ya NBC Dodoma Marathon 2025, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), waandaaji wa tukio hilo kubwa la kimichezo na kijamii, wameanza rasmi utambulisho wa jezi maalum na vifaa vya washiriki kwa kuvikabidhi kwa wadau mbalimbali, akiwemo mmoja wa wadhamini wakuu – Sanlam Insurance.

Mbio hizo, zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, 2025 jijini Dodoma, zimeendelea kuvutia ushiriki mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi, huku zikiweka mkazo kwenye dhamira yake kuu ya kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kuongeza ufadhili wa wakunga, na kuanzisha mpango wa masomo kwa wauguzi wa watoto wenye changamoto za usonji (autism).

Kabidhiano rasmi kwa wadhamini

Zoezi la makabidhiano ya jezi na vifaa limezinduliwa jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Bw. Rayson Foya, aliyeambatana na maofisa mbalimbali wa benki hiyo, akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Bw. Godwin Semunyu. Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya Sanlam, ambapo walipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam, Bw. Julius Magabe, pamoja na maofisa waandamizi wa kampuni hiyo.

NBC: Marathon inayochangia maisha

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Foya aliishukuru Sanlam kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya NBC Dodoma Marathon tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020. Alieleza kuwa michango ya wadhamini kama Sanlam imekuwa chachu katika kufanikisha dhamira ya marathon hiyo, si tu kama tukio la michezo, bali pia kama jukwaa la matumaini kwa Watanzania.

VODACOM, VIVO ENERGY WAUNGANA KUENDELEZA MALIPO YA KIDIJITALI KWA WATUMIAJI WA MAFUTA

Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy, Mohamed Bougriba, wakisaini hati ya makubaliano ya kukuza na kuongeza matumizi ya malipo ya kidijitali kwa wateja wanaonunua mafuta katika vituo vya Engen kupitia huduma ya Lipa kwa Simu. Hafla hii imefanyika tarehe 15 Julai 2025, jijini Dar es Salaam, katika kituo cha mafuta cha Engen Mikocheni.

Dar es Salaam, 15 Julai 2025 – Ikiadhimisha miaka 25 ya kutoa huduma kwa Watanzania, Vodacom Tanzania imezindua ushirikiano rasmi na Vivo Energy Tanzania, kampuni inayosambaza mafuta kupitia vituo vya Engen, kwa lengo la kuimarisha matumizi ya malipo ya kidijitali kote nchini.

Uzinduzi wa ushirikiano huo umefanyika katika kituo cha Engen Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka sekta ya mafuta, usafirishaji pamoja na wateja wa huduma ya M-Pesa. Ushirikiano huu unalenga kuleta mapinduzi katika sekta ya mafuta kwa kuhimiza malipo kwa njia ya simu na kupanua huduma za kifedha kwa Watanzania.

Mageuzi Kupitia Teknolojia: Lipa kwa Simu na Mikopo ya Chomoka

Kupitia mpango huu, madereva wa magari binafsi, daladala, bajaji na bodaboda watanufaika kwa njia mbalimbali, ikiwemo:

  • Malipo kwa njia ya simu (Lipa kwa Simu)
  • Upatikanaji wa mikopo ya mafuta kupitia huduma ya Chomoka
  • Fursa ya kukopa simu janja na kulipa kwa awamu kupitia Vodacom

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Bw. Epimack Mbeteni, alisema:

“Tunajivunia kushirikiana na Vivo Energy Tanzania, kampuni inayoamini katika uvumbuzi na maendeleo ya jamii. Ushirikiano huu si tu unarahisisha maisha ya wateja wetu, bali pia unatoa fursa ya kukuza kipato kupitia huduma salama, rahisi na za kisasa.”

Tuesday, 15 July 2025

NBC YAENDELEZA MAPINDUZI YA KILIMO RUVUMA KUPITIA MSIMU WA PILI WA KAMPENI YA ‘NBC SHAMBANI’

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Bw. Kisare Makori (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’, inayoratibiwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wakulima wa zao la kahawa katika wilaya za Mbinga na Nyasa, mkoani Ruvuma. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC, Bw. Msafiri Shayo (wa nne kulia), Meneja wa NBC Kanda ya Pwani, Bi Zubeider Haroun (wa tatu kushoto), maofisa wengine wa benki hiyo, pamoja na wadau wa kilimo mkoani Ruvuma wakiwemo wakulima.

Mbinga, Ruvuma – Julai 14, 2025

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi msimu wa pili wa kampeni yake ya ‘Shinda Mechi Zako Kinamna Yako na NBC Shambani’ katika Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuchochea kasi ya uzalishaji wa zao la kahawa hususan katika Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Kampeni hii ya kipekee inalenga kuwawezesha wakulima kwa kuwaletea huduma maalum na zenye masharti nafuu, sambamba na elimu ya kifedha kupitia mafunzo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NBC, ikiwa ni pamoja na:

  • Bima ya mazao na afya
  • Huduma za uwakala na kidigitali
  • Mikopo ya pembejeo na zana za kisasa za kilimo
  • Ujenzi wa maghala
  • Msaada katika maandalizi ya masoko na uzalishaji


Mkuu wa Wilaya: “Ni Ukombozi kwa Wakulima wa Kahawa”

Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Mbinga, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya, Bw. Kisare Makori, aliyeipongeza NBC kwa kutoa kipaumbele kwa wakulima kupitia kampeni hii ya kijamii na kiuchumi.

“Zaidi nimefurahi kusikia kupitia kampeni hii wakulima wanaweza kupata mikopo ya vitendea kazi kama matrekta, pembejeo na hata malipo ya awali. Hii ni hatua kubwa kwa wakulima wetu,” alisema DC Makori.

EAST AFRICA POISED TO LEAD AS AFRICA UNLOCKED 2025 CHAMPIONS INCLUSIVE GROWTH

By Our Reporter | Cape Town, South Africa

Cape Town played host to Africa Unlocked 2025, a landmark two-day summit that convened some of the continent’s foremost entrepreneurs, investors, and policymakers to discuss strategies for accelerating inclusive economic growth across Africa.

Organised by Standard Bank Group, the parent company of Stanbic Bank Tanzania, the forum centred on critical enablers of growth — regional trade, infrastructure, energy, and access to capital — with particular emphasis on the unique opportunities emerging across East Africa.


A Shift in Tone: From Constraints to Collaboration

The summit’s conversations touched on familiar regional issues — port congestion, energy access, and trade inefficiencies — but the overarching tone was one of optimism and proactive collaboration. Rather than focusing on what’s missing, Africa Unlocked urged stakeholders to act on what is possible.

The message was clear: Africa’s future lies in leveraging its strengths through coordinated action, innovation, and regional integration.


Trade Integration: Unlocking Borderless Opportunity

Trade featured prominently throughout the discussions. East Africa, through the East African Community (EAC) and its active role in the African Continental Free Trade Area (AfCFTA), has made commendable progress. But the region must go further to enhance the smooth flow of goods and services across borders.

Speakers highlighted ongoing investments in trade corridors, modern port systems, and digital customs platforms as game changers for local producers, logistics players, and cross-border entrepreneurs.

A case in point is Tanzania’s Dar es Salaam Port, a vital regional trade hub. Enhancing its capacity and efficiency stands to benefit not only Tanzania but also its land-linked neighbours — Rwanda, Uganda, and the Democratic Republic of Congo. Conversations reinforced the need for infrastructure projects to be regional in scope, aligned with long-term trade goals.


Powering Progress: The East African Energy Advantage

Energy access was another focal point. East Africa is emerging as a leader in renewable and decentralised energy solutions, with countries like Kenya and Tanzania expanding rural electrification through solar and mini-grid projects.

Sunday, 13 July 2025

VODACOM NA STANBIC WAGUSWA NA JAMII: WATOA MSAADA KWA WALEMAVU, SHULE YA MSINGI SIMIYU

Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Ziwa, Straton Mchau (wa pili kushoto), pamoja na Meneja wa Benki ya Stanbic Tanzania Tawi la Mwanza, Geoffrey Makondo, wakikabidhi moja ya viti mwendo kwa Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Rutherford Magayane (kulia), na Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A, Mwl. Adalbert Chambia (wa pili kulia), katika Shule ya Msingi Sima A, wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

Bariadi, Simiyu – Julai 12, 2025

Katika kuendeleza dhamira yao ya uwajibikaji kwa jamii, Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania wamekabidhi msaada muhimu kwa Shule ya Msingi Sima A, iliyoko Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Hafla hiyo ilihusisha viongozi waandamizi kutoka taasisi hizo mbili, wakiongozwa na Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Bw. Straton Mchau, na Meneja wa Stanbic Bank Tanzania Tawi la Mwanza, Bw. Geoffrey Makondo.


Msaada kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Katika hafla hiyo, viongozi hao walimkabidhi Afisa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Rutherford Magayane, na Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A, Mwl. Adalbert Chambia, msaada wa vifaa mbalimbali vya kusaidia wanafunzi wenye ulemavu pamoja na vifaa vya kuimarisha mazingira ya shule.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na:

  • Viti mwendo (wheelchairs) 4
  • Magongo ya kutembelea (walking sticks) 5
  • Magongo ya mabega (crutches) 5
  • Magongo ya kiwiko (elbow crutches) 5


Kuboresha Miundombinu na Mazingira ya Kujifunzia

Zaidi ya msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Vodacom na Stanbic pia walikabidhi:

  • Miche 100 ya miti kwa ajili ya upandaji wa mazingira ya shule
  • Matundu 10 ya vyoo
  • Magodoro 40 na vitanda 20 kwa matumizi ya wanafunzi

Hatua hii inalenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji, afya na ustawi wa wanafunzi, na kuongeza motisha kwa walimu na jamii inayozunguka shule hiyo.


Safari ya Kijamii Itakayohitimishwa Butiama

Msaada huu umetolewa kama sehemu ya msafara maalum wa kijamii unaodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania.

Msafara huo unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2025 katika Mkoa wa Mara, wilayani Butiama — nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Friday, 11 July 2025

BANK OF TANZANIA MONTHLY ECONOMIC REVIEW, JUNE 2025

MAKAMU WA RAIS DR. MPANGO AIPONGEZA NMB KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI

Arusha – Julai 10, 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ameipongeza Benki ya NMB kwa ushirikiano wake wa karibu na Serikali katika kufanikisha matukio mbalimbali ya kijamii na kiuchumi nchini.

Akizungumza jijini Arusha alipotembelea banda la maonyesho la NMB kabla ya kufungua Mkutano wa 14 wa Watunga Sera wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika, unaofanyika katika ukumbi wa AICC, Dkt. Mpango alieleza kufurahishwa kwake na mchango wa benki hiyo kwa taifa.

“Kila ninapoiona NMB ikishiriki katika matukio mbalimbali yanayoandaliwa na Serikali kama mshirika wa karibu, roho yangu inasuuzika kwa sababu najua kazi wanazofanya na uwezo walionao,” alisema Dkt. Mpango.


WITO WA KUWEKEZA ZAIDI VIJIJINI

Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuitaka NMB kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya benki vijijini, ili kuhakikisha Watanzania wanaoishi maeneo ya pembezoni wanapata huduma sawa na wale wa mijini.

“Ni muhimu benki kama NMB kuhakikisha kuwa huduma zake zinafika kila kona ya nchi, ili kila Mtanzania apate haki ya kifedha bila kujali eneo analoishi,” alisisitiza.


NMB YATOA ZAIDI YA BILIONI 6.4 KUISAIDIA JAMII

Akiwasilisha taarifa ya huduma za kijamii, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB, Baraka Ladislaus, alisema benki hiyo hutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kwa ajili ya kuisaidia jamii.

“Kwa mwaka huu pekee, tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 6.4 kusaidia sekta ya Afya, Elimu na Mazingira. Lengo letu ni kurejesha faida kwa jamii inayotuzunguka na kushirikiana na serikali kuhudumia wananchi,” alisema Baraka.


NMB YAUNGA MKONO MIFUKO YA JAMII

Baraka aliongeza kuwa NMB inaendesha kampeni maalum ya kuunga mkono kazi za mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuimarisha uchumi wa wanachama, kupunguza utegemezi na kuinua maisha ya wazee.

“Tuna bidhaa maalum kama NMB Hekima Plan, inayolenga wastaafu na wale wanaotarajia kustaafu. Kupitia mpango huu, tunatoa elimu ya kifedha ikiwemo uwekezaji na utunzaji wa mafao ili yawasaidie kwa muda mrefu,” alieleza.

NMB YAZINDUA HUDUMA YA KIDIJITALI YA UNUNUZI NA UUZAJI WA HISA KUPITIA NMB MKONONI

Dar es Salaam – Julai 10, 2025

Benki ya NMB kwa kushirikiana na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wamezindua rasmi ushirikiano wa kimkakati na wa kidijitali wa ununuzi na uuzaji wa hisa za kampuni mbalimbali zilizoorodheshwa DSE, kupitia huduma mpya inayopatikana ndani ya aplikesheni ya NMB Mkononi.

Huduma hiyo mpya, matokeo ya ubunifu wa muda mrefu kati ya NMB na DSE, inahusisha uunganishaji wa mifumo ya kidijitali ya NMB Mkononi na Hisa Kiganjani, hatua inayowezesha wateja wa NMB kununua, kuuza hisa, kupata taarifa za soko na thamani ya uwekezaji wao kwa urahisi zaidi kupitia simu zao.


TEKNOLOJIA YA KISASA KUWEZESHA USHIRIKI WA KIFEDHA

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema kuwa huduma hiyo ni hatua kubwa katika kujumuisha Watanzania kwenye masoko ya mitaji kwa njia salama, rahisi na ya kisasa.

“Huduma hii ni matokeo ya ubunifu na ushirikiano baina ya wataalamu wa TEHAMA kutoka NMB na DSE. Wateja sasa wataweza kujisajili, kununua na kuuza hisa, kufanya malipo moja kwa moja kupitia akaunti zao za NMB na kupata taarifa za mwenendo wa soko kwa wakati halisi,” alisema Zaipuna.

Aliongeza kuwa huduma hiyo inathibitisha dhamira ya NMB katika kukuza ushirikishwaji wa kifedha kupitia teknolojia, na inatarajiwa kuongeza kasi ya ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya masoko ya mitaji.


SERIKALI YAIPONGEZA NMB NA DSE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, aliizindua rasmi huduma hiyo na kupongeza mashirika hayo kwa ubunifu unaoenda sambamba na malengo ya Taifa ya kuimarisha huduma kwa wananchi.

“Huduma hii inachangia moja kwa moja katika maeneo manne muhimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa: kuimarisha upatikanaji wa huduma, kubadili mitazamo ya wananchi, kuelimisha jamii kuhusu uwekezaji na kuchochea ushirikiano miongoni mwa taasisi za ndani,” alisema Prof. Mkumbo.

Alisisitiza kuwa huduma hii ni hatua muhimu ya kuhamasisha utamaduni wa kuwekeza miongoni mwa Watanzania, hasa vijana, na kuongeza uelewa kuwa utajiri unaweza pia kupatikana kupitia umiliki wa hisa.


DSE: HATUA MUHIMU KATIKA KUJENGA KESHO BORA

Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Peter Nalitolela, alisema huduma hiyo inapanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji, na kwamba DSE inajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya kidijitali.