Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 30 July 2025

CRDB BANK FOUNDATION YAPONGEZWA KWA KUENDELEZA UJASIRIAMALI KUPITIA PROGRAMU YA IMBEJU

DAR ES SALAAM – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ameipongeza CRDB Bank Foundation kwa mchango wake mkubwa katika kukuza ujasiriamali na elimu ya fedha kwa vijana kupitia Programu ya Imbeju.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa shirika lisilo la kiserikali la National Enterprise Development Chamber (NEDC), Waziri Kikwete alisifu juhudi za CRDB Bank Foundation katika kuwawezesha vijana na kuwajumuisha kwenye mifumo rasmi ya kifedha.

“Taasisi ya CRDB Bank Foundation mnafanya kazi kubwa sana katika kuwainua vijana kupitia Programu yenu ya Imbeju. Mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya fedha mnayoitoa yanatoa fursa adhimu kwa jamii. Kujitoa kwenu kuilea NEDC nalo ni jambo muhimu litakalosaidia kuwajumuisha vijana wengi kwenye huduma rasmi za fedha,” alisema Waziri Kikwete.

CRDB Bank Foundation ndiyo mdhamini wa uzinduzi huo wa NEDC, taasisi inayolenga kuwaunganisha vijana wajasiriamali, wawekezaji, na taasisi mbalimbali ili kujenga mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Bi. Tully Esther Mwambapa, taasisi hiyo inafanya kazi kwa ukaribu na wadau kutoka sekta zote ili kuboresha maisha ya wananchi hasa kutoka jamii zilizotengwa kiuchumi na kifedha.

“Tunakusudia kuchochea ukuaji wa biashara changa kupitia mafunzo ya elimu ya fedha, ujasiriamali, usimamizi wa biashara, na mbinu za upatikanaji wa mitaji. Lengo letu ni kuwawezesha vijana na wanawake kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kifedha bila vizingiti,” alisema Tully.

Aidha, alisisitiza kuwa ushirikiano wa kimkakati kati ya serikali, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali ndio njia bora ya kuharakisha maendeleo ya wajasiriamali nchini.

Kwa upande wake, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NEDC, Bw. Jesse Madauda, alisema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya kuinua uchumi wa vijana kupitia ubunifu na biashara.

“Kwa kuunganisha nguvu, rasilimali na mikakati, tunaamini tunaweza kuharakisha ukuaji wa biashara changa zenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii,” alieleza Madauda.


Fuatilia Habari Zaidi Kama Hizi!

Kwa taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya kifedha, benki, ujasiriamali na fursa za kiuchumi nchini Tanzania na Afrika Mashariki, endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog — chanzo chako bora cha taarifa za kiuchumi na kifedha kwa zaidi ya miaka 11!






No comments:

Post a Comment