Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 30 July 2025

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA BAMMATA KUELEKEA MICHEZO YA MAJESHI ZANZIBAR

ZANZIBAR – Benki ya NMB imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuunga mkono sekta ya michezo nchini kwa kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ya majeshi inayotarajiwa kuanza tarehe 6 Septemba mwaka huu visiwani Zanzibar.

Msaada huo umekabidhiwa na Meneja Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame, kwa Mwenyekiti wa BAMMATA, Brigedia Jenerali Saidi Hamis Saidi, katika hafla fupi iliyofanyika Zanzibar.

Walioshuhudia tukio hilo ni pamoja na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite, pamoja na maafisa wa jeshi Kanali Robert Mbuba na Luteni Kanali Said Shamhuna.

“Msaada huu ni sehemu ya mchango wetu wa kuunga mkono sekta ya michezo na afya, na kuimarisha mshikamano miongoni mwa askari wetu kupitia michezo,” ilieleza Benki ya NMB kupitia uongozi wake.

NMB imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali nchini, ikiwemo afya, elimu, michezo na ustawi wa jamii, kwa kuendelea kushirikiana na taasisi za umma na binafsi kuleta matokeo chanya kwa jamii.


Fuatilia Zaidi Habari Kama Hizi

Kwa taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya sekta ya michezo, benki, fedha na uwajibikaji wa taasisi za kifedha kwa jamii, endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog – blogu mahiri ya kifedha inayokuletea habari za uhakika kwa zaidi ya muongo mmoja!






No comments:

Post a Comment