Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 30 September 2024
SMARTLAB & EIT CLIMATE-KIC PARTNER TO LAUNCH ADAPTATION AND RESILIENCE CLIMACCELERATOR PROGRAM
WAENDESHA BAISKELI 113 WAANZA SAFARI YA VODACOM TWENDE BUTIAMA 2024
BENKI YA EXIM YAFANYA TAMASHA KUSAIDIA WAGONJWA WA AFYA YA AKILI
NMB EMPHASIZES INCLUSIVE LEADERSHIP & MANAGEMENT TRAINING FOR WOMEN
Saturday, 28 September 2024
UDHAMINI WA NMB CDF TROPHY WAFIKIA MIL. 245/-, KIPUTE KUANZA OKTOBA 4, 2024
NMB CDF Trophy ni michuano maalum, ya wazi ya kimataifa ya mchezo wa gofu, inayotumika kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ), ambalo Septemba 1 mwaka huu limetimiza miaka 60, mashindano yakiratibiwa na Klabu ya Gofu Lugalo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutangaza michuano hiyo, Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo, aliishukuru NMB kwa kuendelea kuyabeba mashindano hayo kila mwaka wanaadhimisho ya Kuanzishwa kwa JWTZ Septemba 1, 1964.
Alibainisha kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana zawadi nono ya pesa Shilingi Milioni 4 kwa mshindi wa jumla kutoka NMB, pamoja na zawadi ya gari aina ya Toyota Harrier kwa mshindi wa pigo la ‘all in one’ linalotolewa na Kampuni ya Toyota Tanzania ambao ni wadhamini wenza.
“Ni mashindano ya wazi yatakayojumuisha kategori zote muhimu katika mchezo huu, ambazo ni wachezaji wa kulipwa ‘proffesional,’ wachezaji wa ridhaa ‘amature,’ wachezaji wakubwa ‘seniors,’ wachezaji wanawake ‘ladies’ na wachezaji watoto ‘juniors.’
“Hadi sasa tunao jumla ya watoto 45 wa timu zetu za vijana hapa ambao watashiriki, lakini kwa upande wa wachezaji wakubwa, waliojisajili hadi sasa wamefikia 185 na matarajio yetu ni kuona idadi ikiongezeka zaidi hadi Oktoba 4 mashindano yatakapoanza.
Akizungumza katika mkutano huo, Getrude Mallya ambaye ni Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum wa NMB, aliishukuru JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kuendeleza mashirikiano mema na taasisi yake na wao wanajivunia heshima ya kubaki kuwa wadhamini wakuu.
Friday, 27 September 2024
BENKI YA NMB YAPAMBA MASHINDANO YA SHIMIWI MOROGORO
NBC YAIPAMBA MZIZIMA DERBY ZANZIBAR, YAKABIDHI TUZO, FEDHA KWA MCHEZAJI NA KOCHA BORA MWEZI AGOSTI
Kipa wa Simba SC, Moussa Camara akifurahia na tuzo yake baada ya kuibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. |
Mechi hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na kuisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Wateja mbalimbali wa benki ya NBC walipata fursa ya kuutazama mchezo huo wakiwa katika jukwaa la VIP kupitia udhamini wa benki hiyo.
Thursday, 26 September 2024
EQUITY NA BAKHRESA KUWEZESHA WAFANYABIASHARA KUPATA MIKOPO KIDIGITALI
VODACOM YAZINDUA VITUO VYA HUDUMA ZA MATENGENEZO KWA WATEJA WAKE
Meneja wa Maduka ya Rejareja wa Vodacom Tanzania Plc, Vanessa Mlawi (kati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vituo vya huduma za matengenezo ya simu kwa wateja wa Vodacom kwa kushirikiana na watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo. Kushoto kwake ni Mhandisi Emmanuel Maige, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Smash Technologies na George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika Vodashop ya Mlimani City, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 25 September 2024.
Dar es Salaam – 25th September 2024: Vodacom Tanzania Plc imezindua vituo vya huduma za matengenezo kwa ushirikiano na watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo. Lengo la ushirikiano huu ni kutoa huduma bora kwa wateja ikiwemo kupata matengenezo ya simu zao katika maduka ya Vodacom katika maeneo mbalimbali nchini huku duka la Vodacom Mlimani City ikiwa kama mfano wa huduma hizo.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji, George Lugata akisisitiza malengo ya kampuni hiyo alisema, "Kipaumbele chetu daima ni kutoa huduma bora kwa wateja wetu na huduma hii mpya ni mwendelezo wake. Kwa kushirikiana na washirika wetu hawa, tunaweza kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo tu, tunapanga kuongeza vituo zaidi ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka kote nchini."
Kwa sasa, Vodacom ina vituo 11 vya huduma za matengenezo katika sehemu kadhaa nchini. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu, kampuni hiyo inapanga kupanua mtandao wa vituo vyake vya matengenezo ili kusaidia wateja wengi zaidi. Kwa kuanzia kampuni hiyo itafanya matengenezo ya simu zilizotajwa huku ikiwa na mpango wa kukaribisha makampuni mengine ya simu kuungana nao ili kuongeza ujumuishwaji wa kidijitali nchini.
Naye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare, Meneja wa Maduka Rejareja, Vanessa Mlawi, alisisitiza umuhimu wa vituo hivyo, "huduma hizi za vituo vya matengenezo sio tu zinaongeza ujumuishi bila kubagua wateja bali pia zinaimarisha chapa ya kampuni yetu ya Vodacom. Inatusaidia kushughulikia changamoto za wateja huku pia ikitoa fursa ya kuuza bidhaa na huduma zingine za Vodacom. Zaidi, vituo hivi vinatupa mwangaza kujua mahitaji ya wateja wetu, na namna bora ya kuboresha huduma zetu."
Naye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare, Meneja wa Maduka Rejareja, Vanessa Mlawi, alisisitiza umuhimu wa vituo hivyo, "huduma hizi za vituo vya matengenezo sio tu zinaongeza ujumuishi bila kubagua wateja bali pia zinaimarisha chapa ya kampuni yetu ya Vodacom. Inatusaidia kushughulikia changamoto za wateja huku pia ikitoa fursa ya kuuza bidhaa na huduma zingine za Vodacom. Zaidi, vituo hivi vinatupa mwangaza kujua mahitaji ya wateja wetu, na namna bora ya kuboresha huduma zetu."
THE DECK PRESENTS CHURRASCARIA BRAZILIAN BBQ EAT AS MUCH AS YOU CAN!!!
Saturday, 28th September 2024, from 6 pm.
Eat as much as you can!!!
Churrascaria Brazilian BBQ.
Reserve your seat by paying in advance through our M-Pesa LIPA Number 5948950. Call 0688 990 496 for more information.
The Deck Kitchen & Bar - Masaki Mwisho Jeshini.
NMB BANK LAUNCHES 4TH EDITION OF "BONGE LA MPANGO" CAMPAIGNS
Subscribe to:
Posts (Atom)