Msafara wa baiskeli ya Vodacom Twende Butiama ni msafara wenye malengo makubwa. Waendesha baiskeli wanavuka kutoka pwani hadi Kaskazini mwa Tanzania huku wakijihusisha na huduma za kijamii katika nyanja za elimu, utunzaji wa mazingira, na afya kwa wote.
Msafara wa mwaka huu unatarajia kuchangia madawati 1,500 kwa shule,ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa saidizi kwa shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum. Msafara huu pia utapanda miche 50,000 sambamba na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingita. Mwaka huu msafara huu utawezesha kutolewa kwa kambia za matibabu katika mikoa yote 12 watakapokatiza ambapo watu watapata huduma za ushauri, uchunguzi, na matibabu bure.
Msafara wa Twende Butiama, uliyoanzishwa mwaka 2018 na wapenzi wa baiskeli wakiongozwa na Gabriel Landa, umekua kwa kasi, ukigusa maisha ya Watanzania wengi. Akizungumza kabla ya kuondoka, Landa alisema, "Msafara huu ni Zaidi ya kuendesha baiskeli, unahusu kurudisha kwa jamii na kuendeleza maadili ambayo Mwalimu alituachia. Kila kilomita tunayoendesha, tunaenzi falsafa yake ya kuboresha elimu, afya, na mazingira. Ni mchezo, lakini pia ni wito kwa wote kuchukua hatua kwa Tanzania bora.”
Kile kilichoanza kama wito wa waendesha baiskeli wachache sasa kimekua kuwa jukwaa la kitaifa linalounganisha wadau tofauti chini ya lengo moja la maendeleo ya kijamii. Mbali na kusambaza vifaa vya shule, kupanda miti, na kutoa huduma za afya bure kwa maelfu, msafara wa mwaka 2024 wa Twende Butiama utaenda sambamba na Digi-Truck itakayotoa mafunzo ya ujuzi wa kidigitali bure, shukrani kwa ushirikiano kati ya Huawei na Vodacom Tanzania.
Annette Nkini meneja wa sustainability Stanbic Bank, alisisitiza kujitolea kwa benki hiyo kusaidia lengo hili muhimu, " Stanbic, tumejitolea kuwekeza katika miradi inayochochea maendeleo endelevu. Twende Butiama inaendana na lengo hili na inatoa fursa ya kuleta mabadiliko ya kudumu kwenye kuinua jamii, utunzaji wa kimazingira, kuchangia elimu na kuhakikisha kila mtu anapata huduma muhimu za afya."
Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, msafara wa Twende Butiama umetoa mchango Chanya kwa jamii ya Watanzania, kutoka kuboresha miundombinu ya shule hadi kukuza uendelevu wa mazingira. Waendesha baiskeli wanapoelekea Butiama, wataendelea kuenzi urithi wa Nyerere, kuhamasisha vizazi vijavyo, na kuimarisha roho ya umoja na fahari ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment