Kipa wa Simba SC, Moussa Camara akifurahia na tuzo yake baada ya kuibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. |
Mechi hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na kuisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Wateja mbalimbali wa benki ya NBC walipata fursa ya kuutazama mchezo huo wakiwa katika jukwaa la VIP kupitia udhamini wa benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw. Abdul Karim Mkila aliiwakilisha benki hiyo katika kukabidhi tuzo na hundi ya fedha yenye thamani ya sh milioni moja, kwa mchezaji bora mwezi Agosti, ambae ni kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua huku Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya akikabidhi zawadi kama hizo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids ambae aliiibuka kocha bora kwa mwezi huo.
Katika mchezo huo wa jana ilishuhudiwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara akiibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa zawadi ya tuzo kutoka benki hiyo.
No comments:
Post a Comment