Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 26 September 2024

VODACOM YAZINDUA VITUO VYA HUDUMA ZA MATENGENEZO KWA WATEJA WAKE

Meneja wa Maduka ya Rejareja wa Vodacom Tanzania Plc, Vanessa Mlawi (kati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vituo vya huduma za matengenezo ya simu kwa wateja wa Vodacom kwa kushirikiana na watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo. Kushoto kwake ni Mhandisi Emmanuel Maige, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Smash Technologies na George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika Vodashop ya Mlimani City, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 25 September 2024.

Dar es Salaam – 25th September 2024: Vodacom Tanzania Plc imezindua vituo vya huduma za matengenezo kwa ushirikiano na watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo. Lengo la ushirikiano huu ni kutoa huduma bora kwa wateja ikiwemo kupata matengenezo ya simu zao katika maduka ya Vodacom katika maeneo mbalimbali nchini huku duka la Vodacom Mlimani City ikiwa kama mfano wa huduma hizo.


Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji, George Lugata akisisitiza malengo ya kampuni hiyo alisema, "Kipaumbele chetu daima ni kutoa huduma bora kwa wateja wetu na huduma hii mpya ni mwendelezo wake. Kwa kushirikiana na washirika wetu hawa, tunaweza kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo tu, tunapanga kuongeza vituo zaidi ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka kote nchini."


Kwa sasa, Vodacom ina vituo 11 vya huduma za matengenezo katika sehemu kadhaa nchini. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya simu, kampuni hiyo inapanga kupanua mtandao wa vituo vyake vya matengenezo ili kusaidia wateja wengi zaidi. Kwa kuanzia kampuni hiyo itafanya matengenezo ya simu zilizotajwa huku ikiwa na mpango wa kukaribisha makampuni mengine ya simu kuungana nao ili kuongeza ujumuishwaji wa kidijitali nchini.

Naye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare, Meneja wa Maduka Rejareja, Vanessa Mlawi, alisisitiza umuhimu wa vituo hivyo, "huduma hizi za vituo vya matengenezo sio tu zinaongeza ujumuishi bila kubagua wateja bali pia zinaimarisha chapa ya kampuni yetu ya Vodacom. Inatusaidia kushughulikia changamoto za wateja huku pia ikitoa fursa ya kuuza bidhaa na huduma zingine za Vodacom. Zaidi, vituo hivi vinatupa mwangaza kujua mahitaji ya wateja wetu, na namna bora ya kuboresha huduma zetu."

Mbali na kuboresha huduma kwa wateja, ushirikiano huu unaendana na dhamira ya Vodacom ya kuwa kinara wa mabadiliko ya kidijitali kote nchini. Vituo vya matengenezo vitasaidia kuwahudumia wateja wa kampuni hiyo huku pia vikiongeza matumizi ya simu na uelewa wa kidijitali.

Kama kampuni inayoongoza katika sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania, ikiwa na wateja zaidi ya milioni 22, Vodacom inaendelea kuongoza katika utoaji wa huduma zinazomjali mteja huku zikikidhi mahitaji yanayoongezeka ya watumiaji wake.

Pamoja na kuwa na mpango wa kuongeza vituo vya matengenezo kwenye maeneo mengine, Vodacom inaendelea kujitolea kuhakikisha wateja wake wanapata huduma za matengenezo za kuaminika na hivyo kuridhika na huduma za kampuni hiyo. Mwisho

No comments:

Post a Comment