Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 2 July 2025

BENKI YA UCHUMI YAZIDI KUNG'AA MWAKA 2024 KWA ONGEZEKO LA FAIDA NA MALI

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Uchumi, Dkt. Heavenlight Kavishe, akisoma taarifa ya benki kwa wanahisa katika Mkutano Mkuu wa 19 wa Wanahisa wa Benki ya Uchumi.

Moshi, Kilimanjaro – Julai 1, 2025

Benki ya Uchumi, yenye makao yake makuu mjini Moshi, imeendelea kuonesha mafanikio makubwa katika mwaka wa fedha 2024, kwa kupata faida baada ya kodi ya Shilingi bilioni 1.507, ikilinganishwa na Shilingi bilioni 1.283 mwaka 2023, ambayo ni ongezeko la asilimia 17.46.


Mwenyekiti wa Bodi: Mafanikio Yamegusa Nyanja Nyingi

Akisoma taarifa ya benki hiyo, Mwenyekiti wa Bodi Dk. Heavenlight Kavishe alisema pamoja na ongezeko la faida, benki imepiga hatua katika maeneo mengine muhimu. Alieleza kuwa mali za benki, amana za wateja, mikopo, mtaji na idadi ya wateja wote vimeongezeka kwa kasi, hatua inayoonesha uimara wa taasisi hiyo katika soko la kifedha.


Kanisa Latoa Pongezi, Lahimiza Uwekezaji Zaidi

Mwakilishi wa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, ambaye pia ni Msaidizi wa Askofu, aliipongeza benki kwa mafanikio hayo ya mwaka 2024. Alisisitiza umuhimu wa wanahisa kuendelea kuongeza mtaji ili benki iweze kupanuwa huduma zake na kufikia malengo mapana zaidi.


Mtendaji Mkuu: Tunakua Licha ya Changamoto za Kiuchumi

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu CPA Samwel Wado, alieleza kuwa licha ya changamoto mbalimbali katika mazingira ya kifedha, benki imeweza kusonga mbele:

  • Amana za wateja zimeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 40.36 hadi Bilioni 51.19 (+26.83%)
  • Mali za benki zimefikia Shilingi Bilioni 69.42 kutoka Bilioni 55.08 (+26.03%)
  • Mikopo kwa wateja imepanda hadi Shilingi Bilioni 43.11 kutoka Bilioni 36.9 (+18.71%)
  • Mapato ya jumla yameongezeka hadi Shilingi Bilioni 9.34 kutoka Bilioni 8.32 (+12.26%)

Aliongeza kuwa ubora wa mali za benki (Asset Quality) umeimarika sana, huku kiwango cha mikopo chechefu kikishuka kutoka asilimia 11.02 hadi 9.4, na kufikia asilimia 5 ifikapo Machi 2025.


Dhamira ya Huduma Bora na Uwajibikaji wa Kijamii

CPA Wado alisisitiza kuwa dhamira ya benki ni kutoa huduma bora kwa wateja, kuendeleza ubunifu, na kusimamia masuala ya mazingira, jamii na utawala bora kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na wadau wote wa benki.


Wakaguzi wa Hesabu Wapongeza Hati Safi

CPA Baraka Moshi, mwakilishi wa kampuni ya ukaguzi ya Auditax International, aliipongeza benki ya Uchumi kwa kupata hati safi ya ukaguzi kwa mwaka 2024, na kuihimiza benki kuendelea kufuata taratibu, miongozo na sheria zinazohitajika kwa maendeleo endelevu.


Benki Kuu Yatambua Utawala Bora

Mwakilishi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bwana Lusungu, alitoa pongezi kwa benki ya Uchumi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, ambayo inawawezesha wanahisa na wadau wengine kutoa maoni yao kwa uwazi.


Wanahisa Waipongeza Menejimenti

Katika majadiliano ya mkutano huo, wanahisa waliipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi kwa kazi nzuri mwaka 2024, huku wakihimiza kuwekwa juhudi zaidi katika:

  • Kuimarisha mtaji
  • Kuongeza faida
  • Kusimamia mikopo kwa weledi


Endelea Kutembelea Blogu Yetu kwa Taarifa Zaidi Kuhusu Sekta ya Benki, Fedha na Uchumi.

No comments:

Post a Comment