Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 23 January 2023

NMB YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA SHILINGI MILIONI 26 ARUSHA


Sekta ya afya ni sekta muhimu kwa maendeleo ya jamii zetu na kwa kulitambua hilio, Benki ya NMB imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa Wilaya ya Arusha kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi 26,000,000 katika Vituo vya Afya - Mkonoo ambavyo ni;
  • Vitanda 10 vya kujifungulia kwa kina mama
  • Vitanda 10 vya kulazia wagonjwa wa kawaida

Huku, kwa Kituo cha Afya Levolosi waliwakabidhi mabenchi 20 ya kusubiri huduma na kukalia kwa wasindikizaji.


Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Mejooli alisema kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza Tanzania, wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.


Lakini pia, aliongezea kuwa Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi sana ya kuchangia katika miradi ya jamii, lakini benki imejikita zaidi katika maeneo ya elimu, afya, na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga na tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii.

kwa zaidi ya miaka kumi mfululizo, Benki ya NMB imekuwa ikitenga asilimia 1 ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka.

No comments:

Post a Comment