Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfuko huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, Waziri Jenista amesema mfuko huo ni salama kwa uwekezaji kwani tangu uanzishwe hadi sasa umeonesha mafanikio makubwa kwenye sekta ya uwekezaji na uchumi.
Kwa upande wa Mtunza Amana wa Mfuko wa Faida (Faida Fund) ambaye ni Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela ameeleza kwamba mfuko huo ni wa kipekee, kwani umezingatia sera mahususi ya huduma jumuishi za kifedha zinazomjali mtanzania wa rika zote ikiwa ni pamoja na kuweza kununua vipande kwa shilingi elfu 10 jambo ambalo linaenda sambaba na sera ya benki hiyo ya kumsikiliza mteja.
Aidha amefafanua kwamba, Mfuko wa Faida unakuwa mfuko wa saba katika mifuko ya uwezazaji wa pamoja ambayo benki ya crdb inaisimamia na unatoa fursa pekee ya uwekezaji wa muda mfupi kwa watanzania kuweza kukuza mitaji yao kwa faida lakini pia ni faida kwa watumishi housing kukusanya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama (wanne kushoto) akiongoza zoezi la uzinduzi wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, Januari 14, 2023. Pamoja naye ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wapili kulia) pamoja na viongozi wengine. Picha zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment