Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 20 November 2020

DSTV YAJA NA OFA KABAMBE YA MSIMU WA SIKUKUU!

Katika kunogesha zaidi msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya, kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja wapya wa DStv yenye lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanapata huduma hiyo ili waweze kufurahia burudani elimu na habari wao na familia zao msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya DStv ya msimu wa sikukuu iliyopewa jina la ‘Vibe la sikukuu na DStv kama DStv’, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kama ilivyo ada kwa DStv, kila unapofika msimu wa sikukuu hutoa ofa maalum kwa wateja wake ili kuwapa uhakika wa kupata huduma za DStv kipindi hiki ambapo ni cha sikukuu na watu wengi wakiwemo watoto huwa likizo hivyo kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa burudani nyumbani.
Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akifafanua kuhusu kampeni ya msimu wa sikukuu ambapo DStv inatoa ofa maalum kwa wateja wake.

“Kwa wale ambao bado hawajajiunga na DStv, huu ndio wakati muafaka kwani kuna ofa maalum ya kujiunga ambapo mteja ataunganishwa na DStv kwa Sh 79,000 tu na zawadi ya kifurushi cha Family mwezi mmoja bila malipo” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa ofa hii inawapa uhakika wateja wapya kufurahia maudhui motomoto ndani ya DStv na itadumu hadi mwisho wa mwezi Desemba 2020.
Mkuu wa Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msimu wa sikukuu ambapo DStv imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake

Akifafanua zaidi kuhusu ofa hiyo inapatikana nchi nzima, Mkuu wa Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum amesema kuwa mawakala wa DStv wanapatikana kote nchini hivyo mteja atapata ofa hii na huduma ya kufungiwa DStv popote alipo kwa urahisi na haraka. “Tunafahamu kuwa kipindi hiki cha sikukuu watu wengi husafiri kuungana na familia zao maeneo mbalimbali mijini na vijijini na kwa kulitambua hili tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinapatikana kirahisi kila mahali”

Amewashauri wateja wote ambao wanahitaji huduma za DStv, mbali na kwenda kwenye vituo au mawakala wa DStv, wanaweza pia kupata huduma hiyo kwa kupiga simu 0659 07 07 07 au kwa kutembelea kurasa za DStv Tanzania za mitandao ya kijamii Instagram @dstvtanzania, Twitter @DStv_Tz na Facebook @DStv(tz) ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali za DStv kama vile kuunganishwa, kulipia vifurushi, kubadili kifurushi na huduma nyinginezo.

Kwa wateja wa DStv, Salum amesema wataendelea kupata maudhui kemkem kuanzia michezo, burudani, vipindi vya elimu, chaneli za watoto, sinema na tamthilia za ndani na nje bila kusahau chaneli za habari zitakazowahakikishia taarifa mbalimbali kutoka pande zote za dunia.

Kwa wale wanaosafiri, amewakumbusha kupakua App ya DStv Now inayowawezesha kuendelea kufurahia huduma za DStv kwenye vifaa mbalimbali kama simu janja bila gharama yaziada. “kwa wale wanaosafiri na wangehitaji kuendelea kuburudika na DStv, ni vyema wakatumua huduma yetu ya DStv Now kwa kupakua app yetu na hivyo kuweza kutumia akaunti zao katika vifaa zaidi ya vine popote walipo nchini bila kulazimika kulipia malipo yoyote ya ziada” alisisitiza Salum.
Waigizaji maarufu katika tamthilia ya Karma Ford (kulia) na Misa (katikati) wakiwa pamoja na maafisa wa DStv Tanzania – Mkuu wa Masoko Ronald Shelukindo (wa pili kulia), Mkuu wa Mauzo Salum Salum (wa pili kushoto) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msimu wa sikukuu.

Hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya DStv ilihudhuriwa na baadhi ya wasanii maarufu wa Bongo Movie wanaoigiza katika tamthilia na filamu mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo ndani ya DStv akiwemo kinara wa tamthilia maarufu ya Karma Wema Sepetu.

Kufahamu zaidi kuhusu maudhui motomoto msimu huu wa sikukuu tembelea https://www.dstvafrica.com/en-tz

No comments:

Post a Comment