ATM hizi zitawekwa katika viwanja vya ndege vikubwa nchini ambavyo ni uwanja wa Kimataifa vya Julius Nyerere, Uwanja wa Kilimanjaro na ule wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, ili ziweze kutumiwa na wasafiri wanaoingia na kutoka nchini wanaohitaji fedha za Tanzania au za nchi waendako.
Mwanamitindo na Mfanyabiashara, Nancy Sumari akifurahia huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kwenda shilingi za kitanzania katika mashine ya ATM ya Benki ya NMB. |
Mkuu wa Mauzo, Idara ya Hazina ya Benki ya NMB, Jeremiah Lyimo akifurahia huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kwenda shilingi za kitanzania katika mashine ya ATM ya Benki ya NMB. Naye Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania, Jerry Sabi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuwa wa kwanza kuleta huduma hii nchini ambayo imekuja kutoa suluhisho la upatikanaji wa huduma za fedha za kigeni kufuatia kufungwa kwa maduka ya kubadilishia fedha nchini. Alisema Serikali ilizitaka Benki za Biashara kusaidia na kuhakikisha kuwa huduma za kubadilisha fedha nchini zinapatikana kwa urahisi. Hii ina maana zoezi la kubadilisha fedha sasa litakuwa rahisi na haraka na hasa pindi mashine hizi zitakapowekwa kwenye viwanja hivi vya ndege. Benki ya NMB imelifanyia kazi hili kwa weledi na ubunifu mkubwa na sasa wamekuja na suluhu ya teknolojia kuongeza nguvu ya upatikanaji wa huduma hii ambayo imekuwa ikitolewa na matawi yao yote nchini. Hivyo basi, uwepo wa ATM za kubadilishia fedha kutasaidia kuhakikisha kwamba huduma hizo zinapatikana wakati wowote (Masaa 24) na kwa urahisi na usalama zaidi. |
No comments:
Post a Comment