Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 3 October 2015

UZINDUZI WA MAUZO YA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZINAZOJENGWA ENEO LA MOROCCO SQUARE, JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
 Wageni waalikwa.
Wageni waalikwa.
Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
Burudani ya muziki.

Burudani ya muziki.
Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya makazi na biashara.

Waziri Kairuki aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua mauzo ya nyumba za biashara na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na wenzake kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kiasi kikubwa katika kuleta uhai na taswira nzuri ya shirika hilo.

Alisema kuwa serikali inatambua kuwa makazi ni jambo muhimu kwa maendeleo ya taifa, ndiyo maana imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kuwezersha sekta ya nyumba kuwa endelevu na yenye tija kwa wananchi na uchumi wa nchi.

Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza sekta hii ni kuwa na Sheria ya Mikopo ya nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya mwaka 2008, iliyoanzishwa kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa nyumba na taasisi za fedha kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta hii muhimu.

Aidha , alisema tangu kuwapo kwa sheria hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya zaidi ya benki 50 zilizopo nchini zikitoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania, 16 kati ya hizo zikiwa zimesaini makubaliano na na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.

Naibu waziri huyo alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya riba kubwa ya mikopo ya nyumbva inayotozwa na benki mbalimbali ambayo ni kati ya asilimia 18 na 25, serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya kuewezesha benki kupunguza riba katika mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua nyumba.

Aliwahimiza Watanzania kutumia fursa zilizopo za mikopo ya Benki kununua nyumba zinazojengwa na NHC, ikiwamo kujitokeza kwa wingi kununua nyumba hizo za za mradi wa Morocco Square ambao una nyumba za ofisi hoteli, makzi na maduka makubwa.

No comments:

Post a Comment