Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 24 October 2014

TASWIRA ZA UZINDUZI WA SAFARI ZA FLY DUBAI NCHINI

Ndege ya Shirika la Ndege la Fly Dubai ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere ikiwa katika uzinduzi wake uliofanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu, Ndege hiyo itafanya safari zake za moja kwa moja kutokea Dubai mpaka Dar es Salaa, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar.

Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu, na wapili kutoka kushoto ni Balozi mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga, wakwanza kushoto ni Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Pius Msekwa na wakwanza kulia ni Bajeti meneja wa Fly Dubai wa nchini Tanzania Bw. Riyaz Jamal wakiitazama Ndege ya Fly Dubai ilipokuwa inawasili. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu akisalimiana na Makamu wa Mkuu wa kampuni hiyo, Sudhir Screedharan mara baada ya kuwasili na Ndege hiyo. Katikati ni Bajeti meneja wa Fly Dubai Tanzania Bw. Riyaz Jamal. 

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahaya akisalimiana na Bw. Screedharan.

Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga akisalimiana na Bw. Screedharan.

Wakwanza kushoto ni Bw. Shabani Baraza akimwakilisha Balozi wa Tanzania UAE, wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara katika Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Bw. Cleophas Luhumbika Watatu kutoka Kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Hangi Mgaka pamoja na wajumbe wengine wakimsikiliza Mhe. Suluhu

Makamu wa Mkuu wa kampuni hiyo, Sudhir Screedharan akizungumza katika hafla hiyo mara baada ya uzinduzi wa safari za Ndege ya Shirika lake la Fly Dubai, alisema safari za ndege zao zinatumia ndege mpya za kisasa aina ya Boeing zipitazo 100.

Sehemu ya wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Mdogo.

Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai akizungumza na kuushukuru uongozi wa Fly Dubai kwakukubali kuanzisha safari za moja kwa moja kutokea Dar es salaam mpaka dubai, Mhe. Mjenga alisema kwa kuanza kwa safari ya ndege hiyo inategemewa kuongezeka kwa idadi ya Watalii nchini kutokea Milioni 1 kwa mwaka mpaka Milioni 2, fursa za ajira kwa Watanzania.

Mhe. Suluhu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ndege hiyo itakayoanzisha safari zake moja kwa moja kutokea Dar es salaam mpaka Dubai.

Makamu Mkuu Bw. Sudhir Screedharan (wakwanza kulia), wa kwanza kushoto Balozi Mdogo Mhe. Mjenga na (katikati) ni Bw. Riyaz Jamal wakimsikiliza Mhe. Waziri alipokuwa akizungumza.

Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza Bw. Screedharan alipokuwa akizungumza.

Picha ya pamoja (Picha na Reginald Philip)


No comments:

Post a Comment