Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 17 October 2024

SERIKALI NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA (IMF), ZAHITIMISHA TATHMINI

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kushoto), Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kushoto), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kulia), wakizungumza jambo wakati wa kikao kati ya Serikali na Ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), cha kuhitimisha tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya kwanza (1st Review) ya Program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akishiriki kikao cha kuhitimisha tathmini kati ya Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa njia ya mtandao, akiwa jijini Dodoma, ambapo timu hiyo ya IMF imefanya Tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya kwanza (1st Review) ya Program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF).
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kwa njia ya mtandao) na ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), wakiwa katika kikao cha kuhitimisha tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF).
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), akiagana na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Charalambos Tsangarides, baada ya kutamatika kwa kikao kati ya Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) aliyeshiriki kwa njia ya mtandao.
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati aliyeketi) na Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Charalambos Tsangarides (wa pili kushoto aliyeketi), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya kutamatika kwa kikao kati ya Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) aliyeshiriki kwa njia ya mtandao.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha kuhitimisha tathmini kati ya Serikali na Ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ulioongozwa na Bw. Charalambos Tsangarides, kwa njia ya mtandao, akiwa jijini Dodoma.

Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF imekuwa nchini kwa majuma kadhaa ikifanya Tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya kwanza (1st Review) ya Program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF).

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Manaibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Dkt. Yamungu Kayandabila, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali ambao walishiriki Mkutano huo wa kuhitimisha tathimini wakiwa Ukumbi wa Mikutano wa Mount Meru wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Wednesday 16 October 2024

IMF NA BENKI YA DUNIA ZAITEUA TANZANIA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza kikao cha Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ilitolewa taarifa kuwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), zimeitangaza Tanzania kuwa nchi ya pili, baada ya Madagascar, kunufaika na Mfumo wa Ushirikiano wa Kuimarisha Hali ya Hewa kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari mbaya za uharibifu wa mazingira.

Ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiongozwa na Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika hilo, Bw. Charalambos Tsangarides (kulia), ukiwa katika kikao na Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza kikao cha Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), zimeitangaza Tanzania kuwa nchi ya pili, baada ya Madagascar, kunufaika na Mfumo wa Ushirikiano wa Kuimarisha Hali ya Hewa kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari mbaya za uharibifu wa mazingira.

Kupitia Mfumo huo, IMF na WBG watafanya kazi kwa karibu na washirika wengine wa maendeleo, kuratibu juhudi zao za kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya sera ya Tanzania ili kukabiliana na vihatarishi na changamoto zinazohusiana na mabadiliko hayo ya tabianchi na kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa Tanzania.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa, Bw. Charalambos Tsangarides, alisema kuwa kupitia mpango huo, IMF itaunga mkono kuanzishwa kwa kanuni za uwekezaji wa umma zinazohimili mabadiliko ya tabianchi na utoaji taarifa, huku Benki ya Dunia itajikita katika kusaidia kutekeleza miradi katika sekta zitakazoimarisha uwezo wa Tanzania kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama vile nishati, maji, hifadhi ya jamii na kilimo.

Taasisi hizo mbili pia zitasaidia uboreshaji na utekelezaji wa sera ya Tanzania ya usimamizi wa hatari za maafa, ikiwa ni pamoja na kufadhili mfumo wa kukabiliana na hatari hizo na uimarishaji wa mtandao wa usalama wa kijamii ili kukabiliana na majanga ya hali ya hewa.

GOVERNMENT, AMSONS GROUP SIGN $320 MIL. DEAL TO BOOST CEMENT PRODUCTION


Dar es Salaam: The construction industry received a major boost on Tuesday as the government signed an agreement with the Amsons Group to invest 320 million US dollar (approximately 872bn/-) for the expansion of the Mbeya Cement plant and the construction of a new cement plant in Tanga.



The expansion of the Mbeya Cement plant will increase its clinker production capacity fivefold, from the current 1,000 tonnes to 5,000 tonnes per day.

Similarly, the new facility in Tanga will also produce 5,000 tonnes of clinker daily. This significant investment positions the company to better serve both domestic and international markets.



Mbeya Cement Company Limited is owned through a shareholding structure comprising the government, represented by the Treasury Registrar (25 per cent), the Amsons Group (65 per cent) and the National Social Security Fund (10 per cent).



Speaking at a press conference in Dar es Salaam, Treasury Registrar Nehemia Mchechu highlighted that the expansion and construction of new cement manufacturing plants underscores the importance of meeting the growing demand in local and international markets.



He noted that Tanzania is among the top 10 countries in Africa with a rapidly growing population, which increases the need for housing construction. Mr Mchechu emphasised that by 2100, Tanzania is expected to be among the top 10 nations globally with the fastest population growth. Currently, Tanzania’s population stands at 61 million.

“This population increase drives high demand for construction materials. We are confident that this expansion will meet the needs of the domestic market, especially in the Southern region and pave the way for new opportunities in neighbouring countries such as Zambia,” he said.

The expansion is expected to be completed within the next two years and once operational, it will significantly reduce cement prices due to increased supply, providing relief to citizens and construction stakeholders.

He also pointed out that ongoing major development projects, including the Julius Nyerere Hydro Power Plant (JNHPP), the electrified Standard Gauge Railway (SGR), the J.P. Magufuli Bridge and the construction of roads and ports, have driven a surge in cement demand.

VODACOM TWENDE BUTIAMA 2024 YAHITIMISHWA BUTIAMA KWA MAFANIKIO MAKUBWA


Dar es Salaam – Msafara wa kihistoria wa Vodacom Twende Butiama 2024 umekamilika rasmi mnamo tarehe 13 Oktoba kwa mafanikio makubwa, ukihitimishwa wilayani Butiama, kijijini kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere katika mkoa wa Mara. Msafara huo, uliowakutanisha waendesha baiskeli zaidi ya 100 kutoka Tanzania na nchi jirani, ulifanyika kuanzia tarehe 29 Septemba na kupita katika mikoa 12 ya Tanzania.


Mafanikio ya msafara huu ni pamoja na kutoa huduma za afya bure kwa maelfu ya wananchi katika kambi za matibabu zilizowekwa njiani. Zaidi ya madawati 1,000 yalichangwa kwa shule mbalimbali, zikiwemo shule zinazohudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum, huku miche 50,000 ya miti ikipandwa katika maeneo mbalimbali ambako msafara huu ulipita, lengo likiwa kuhifadhi mazingira.


Ubunifu huu wa Msafara wa Vodacom Twende Butiama, ulianzishwa mwaka 2018, umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kusaidia jamii kupitia utoaji wa huduma za kijamii katika nyanja za elimu, afya, na mazingira.






MBUNGI LA KITONGA KWA NGUVU YA BUKU 10 TU NDANI YA DStv!!!


Tuesday 15 October 2024

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UMOJA WA MABENKI TANZANIA (TBA)

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) akizungumza katika kikao chake na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), ofisini kwake jijini Dodoma, ambapo walijadili kuhusu mchango wa Sekta ya Benki katika uchumi wa nchi kupitia huduma za fedha jumuishi. Kushoto ni Mwenyekiti wa TBA, Bw. Theobald Sabi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Bw. Theobald Sabi, akizungumzia mchango wa Sekta ya Benki nchini katika kikao kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Taasisi hiyo, jijini Dodoma, ambapo walijadili kuhusu mchango wa Sekta ya Benki katika uchumi wa nchi kupitia huduma jumuishi za kifedha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiongoza kikao kati yake na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akifafanua jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, akielezea namna ambavyo Serikali kupitia Benki hiyo imekuwa ikisimamia Sekta ya Benki nchini wakati wa kikao kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
Na. Benny Mwaipaja, Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma, ambapo walijadili kuhusu mchango wa Sekta ya Benki katika uchumi wa nchi kupitia huduma jumuishi za kifedha. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, wakati ujumbe wa TBA uliongozwa Mwenyekiti wake, Bw. Theobald Sabi.

DKT. NCHEMBA ATETA NA MKUU WA KAMPUNI YA HEINEKEN JIJINI DODOMA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika picha na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya Vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford, baada ya kikao chao kilichofanyika Ofisini kwake -Treasury Square, jijini Dodoma. Katika kikao hicho walijadili kuhusu ukuaji wa Kampuni na namna ambavyo Kampuni hiyo inachangia mapato katika uchumi na maendeleo ya nchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiongoza kikao kati yake na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford, alipomtembela ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford aliyefika - Treasury Square, jijini Dodoma, kuzungumza na Mhe. Waziri kuhusu maendeleo ya Kampuni hiyo na namna inavyochangia katika uchumi wa nchi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kulia ni Kamishna Msaidizi, Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akifuatiwa na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Lilian Pascal.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya Vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford, aliyefika kumtembelea Ofisini kwake, Jengo la Treasury Square, Jijini Dodoma, ambapo walizungumzia kuhusu maendeleo ya Kampuni hiyo na mchango wake katika uchumi wa nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Mgeni wake, Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya Vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford na ujumbe wake, walipomtembelea Mhe. Wazir,i Ofisini kwake jijini Dodoma.
Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya Vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford na ujumbe wake, akifafanua jambo alipomtembelea Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), Ofisini kwake jijini Dodoma.

Na. Benny Mwaipaja, Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya vinywaji vya Heineken, Bw. Frank Ford, aliyemtembelea Ofisini kwake, Jengo la Treasury Square, jijini Dodoma, akiambatana na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo. Bi. Lilian Pascal, ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya kampuni hiyo iliyowekeza hapa nchini na namna inavyochangia katika pato la Taifa na Uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya na Kamishna Msaidizi, Idara ya Sera, Bw. William Mhoja, pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.

VODACOM YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUPELEKA HUDUMA MTAANI

Mteja wa muda mrefu wa Vodacom Tanzania Plc, George Nyamugali (wa nne kutoka kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaliyofanyika katika Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam. Ili kusherehekea wiki ya huduma kwa Wateja, Wafanyakazi wa kampuni hiyo wamewafuata wateja ili kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi papo hapo.

Dar es Salaam, Oktoba 07, 2024 – Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia Vodacom Tanzania imezindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 kwa kaulimbiu ya ‘Huduma Bora Kila Wakati’, ambapo kupitia program maalumu ya Huduma Kitaani imeanza kwa kutembelea Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la Wiki hii ya Huduma kwa Wateja ni kuimarisha mahusiano kati ya kampuni ya Vodacom na wateja wake, huku ikisisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora unaokidhi mahitaji ya mteja.


Akizungumza katika tukio hilo, Harriet Lwakatare, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, alisema, "Wiki hii ni fursa yetu ya kumshukuru kila mteja aliyekuwa nasi muda wote katika safari hii. Kupitia kaulimbiu yetu ‘Huduma Bora Kila Wakati,’ tunaleta huduma zetu moja kwa moja kwa wateja wetu, kuwasikiliza, na kuhakikisha tunawapatia huduma stahiki."


Mwaka huu, Vodacom Tanzania imeamua kuwasogezea wateja wake huduma kwa kuwafuata pale walipo kwenye shughuli zao za kila siku na kutatua changamoto zao pamoja na kupokea maoni yao kuhusu huduma za Vodacom. Harakati za huduma kitaani zitafanyika pia katika kanda za Vodacom mikoani na itaenda sambamba na utoaji wa msaada katika hospitali kadhaa ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Vodacom kuchangia damu.


Lwakatare aliendelea kusema, "Kwetu sisi huduma kwa wateja siyo tu suala la miamala au masuala ya kiufundi ila pia ni kule kujali wateja wetu na kuhakikisha wanapata huduma zinazowasaidia katika maisha yao ya kila siku. Tunataka wateja wetu watumie mtandao wetu na wafanye biashara zao kwa amani, wakijua kuwa Vodacom ipo kwa ajili yao."

NMB CEO CHIEF GUEST AT CHARLOTTE SEC. SCHOOL GRADUATION CEREMONY


With a few days left to the Fourth Form National Examinations scheduled to be held on November 11, 2024, form four candidates at Charlotte Secondary School located at Tungi Mkwajuni, Morogoro Municipality, have been urged to put God first, have discipline, work hard, have integrity and honest, if they are to achieve more success both academically and spiritually.


The call was made by the NMB Bank Chief Executive Officer (CEO), Ruth Zaipuna during the 12th graduation ceremony held in Morogoro over the weekend and attended by the bank’s management.


The graduation ceremony began with a holy mass presided by Father Isdory Ndekumanya who later joined the event’s chief guest, Ruth Zaipuna to cut a ribbon to inaugurate the school’s library.


Speaking during the event, Zaipuna commended the school’s board for the honor offered to her to officiate as guest of honor adding that the event reminded her of her form four graduation held 33 years ago at Kilakala Secondary School in Morogoro.


"Everyone has their own life journey, but the life journeys of others have something that you could learn from which can help you too. As you graduate form four today, remember that each of you has made a stride, so I take this opportunity to ask you to continue serving and trusting God but at the same time put an extra effort into everything you do.


"I have gone through various stages of education and then embarked on work life so as I said earlier, everyone has their own life journey, and sincerely speaking some of the things that helped me achieve success personally include putting God first in everything I do and every step I take.


"You also need a high level of discipline, and ensure to work hard in everything you do, be it small or big but you need to to continue learning every day," noted Zaipuna.


Zaipuna during the event lauded the Charlotte Secondary School Board under the chairperson Vidda-Joyce Makundi for spearheading the school’s success and congratulated parents and guardians for their efforts noting that she believes that behind every young child who believes in himself/herself, there is a parent who gives him/her that confidence.


Zaipuna used the opportunity to remind parents and students of the importance of creating a positive saving culture, urging them to join the NMB Youth Forum called ‘Go na NMB’ which comes with many benefits including financial literacy and other banking solutions including health insurance.


Earlier, the Principal of Charlotte Secondary School, Sister Monica Masaure lauded the parents for their cooperation in supporting their children's education since 2021 when they joined, while congratulating the teachers and non-teaching staff for supporting the well-being of the students.


Sister Monica reiterated that the mission of her school is to scrap second and third grades and remain with 'Division One' only.

CEO NMB AWAFUNDA WAHITIMU "FORM FOUR" CHARLOTTE SEKONDARI, MOROGORO


Kuelekea mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne itakayofanyika Novemba 11, 2024, wahitimu wa Shule ya Sekondari Charlotte iliyopo Tungi Mkwajuni, Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kumtanguliza Mungu, kuwa na nidhamu, bidii, uadilifu na uaminifu, ili kupata mafanikio zaidi kielimu, kimaisha na kiimani.


Wito huo umeetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, wakati wa Mahafali ya 12 ya shule hiyo inayomilikiwa na Shirika la Masista wa Kazi ya Roho Mtakatifu, yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 12, yaliyohudhuriwa pia na menejmenti ya benki hio.


Mahafali hayo yalitanguliwa na Misa Takatifu iliyoongozwa na Padre Isdory Ndekumanya wa Shirika la Mapdre wa Maisha ya Kitume wa Kazi ya Roho Mtakatifu, aliyemuongoza Mgeni Rasmi Bi. Zaipuna kukata utepe kuzindua Maktaba Mpya ya shule hiyo yenye usajili namba; S.4445.


Akizungumza wakati wa hotuba yake, Bi. Zaipuna aliishukuru Bodi ya Shule hiyo yenye wanafunzi 462 kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo, lililomrejeshea kumbukumbu za miaka 33 iliyopita alipokuwa akihitimu Kidato cha Nne katika Sekondari ya Kilakala mjini Morogoro.


“Kila mtu anayo safari yake ya kimaisha, lakini historia za maisha ya wengine zina kitu cha kujifunza kinachoweza kukusaidia nawe, kwa hiyo mnapohitimu kidato cha nne leo, kila mmoja wenu amepiga hatua, hivyo niwaombe muendelee kumtumikia na kumtumainia Mungu na kuweka juhudi katika kila mnachofanya.


“Nimepitia hatua mbalimbali za kielimu tangu hapo, baadaye maisha ya ajira na kama nilivyosema, kila mmoja ana safari yake, na katika safari yangu kielimu na kimaisha, vitu vilivyonisaidia kupata mafanikio ni pamoja na kumtegemea na kumtanguliza Mungu katika kila kitu, kila hatua.


“Pia, kuwa na nidhamu ya hali ya juu, bidii kwenye kila kitu ninachofanya kiwe kidogo au kikubwa, nafanya kwa bidii kubwa na maarifa makubwa, kuwa muadilifu, muaminifu, kuonesha na kusimamia ubora katika kazi ninayofanya na zaidi ni uamuzi wa kuendelea kujifunza kila siku,” alibainisha Bi. Zaipuna.


Aliupongeza uongozi wa Charlotte Sekondari na Bodi ya Shule chini ya Mwenyekiti Vidda-Joyce Makundi kwa kusimamia vema na kufanikisha elimu kwa wahitimu hao, huku akiwapongeza wazazi na walezi, akisema anaamini kuwa nyuma ya kila mtoto mdogo anayejiamini, kuna mzazi anayempa kujiamini huko.


Bi. Zaipuna alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wazazi na wanafunzi umuhimu wa kujenga utamaduni chanya wa kujiwekea akiba na kuwataka kujiunga na Jukwaa la Vijana la NMB liitwalo Go na NMB linalojumuisha elimu ya fedha, uwekaji akiba na suluhisho nyinginezo zikiwemo za bima ya afya.


Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Charlotte, Sista Monica Masaure, aliwashukuru wazazi kwa ushirikiano wao katika kujenga elimu ya watoto wao tangu mwaka 2021 walipojiunga, huku akiwapongeza walimu na wafanyakazi wasiokuwa waalimu kwa kusaidia ustawi wa taaluma shuleni kwake.


Sista Monica alibainisha kuwa dhamira yao kama shule ni kufuta ufaulu wa madaraja ya pili na tatu na kubaki na ‘Division One’ tu, msukumo unaopewa nguvu sio tu na ufundishaji wa walimu, bali misingi bora na imara iliyowekwa na wadau wa elimu wa shule hiyo ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia