Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Sunday, 20 July 2025

VODACOM, JUBILEE ALLIANZ WAJIPANGA ‘KUINOGESHA’ NBC DODOMA MARATHON

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. Nguvu Kamando (katikati), pamoja na maofisa waandamizi wa taasisi hizo, akiwemo Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Bw. Godwin Semunyu (kulia), wakionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma, wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Julai 18, 2025 – Wadhamini wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz Tanzania, wamesisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ili kuhakikisha zinafikia malengo ya kijamii huku zikileta hamasa na furaha kwa washiriki.

Dhamira hiyo imeelezwa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya maofisa wa benki ya NBC, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha Bw Rayson Foya, waliotembelea makao makuu ya kampuni hizo kwa lengo la kukabidhi jezi maalum na vifaa vya mbio kwa washiriki – ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika msimu wa sita wa marathon hiyo.

Mbio za NBC Dodoma Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, 2025, jijini Dodoma, mwaka huu zinalenga kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili kwa wakunga 200, na kuanzisha mpango wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism).

Katika ziara yao, Bw Foya na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa NBC, Bw Godwin Semunyu, walikabidhi vifaa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jubilee Allianz Tanzania Bw Jaideep Goel, na kisha kuendelea na ziara kwa Vodacom Tanzania ambapo walipokelewa na maofisa waandamizi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara Bw Nguvu Kamando.

Akizungumza katika hafla hizo, Bw Foya alisema:

“NBC Dodoma Marathon sio tu tukio la kimichezo bali ni jukwaa la matumaini ya maisha kwa Watanzania. Ushiriki wa wadau hawa ni chachu muhimu katika kufanikisha dhamira yetu ya kurejesha kwa jamii kupitia afya na ustawi wa wananchi.”

Kwa upande wake, Bw Kamando wa Vodacom alisema:

“Tunawapongeza NBC kwa ubunifu na weledi wa hali ya juu katika maandalizi. Jezi hizi ni bora sana, na tumeridhishwa na uratibu wa mbio hizi. Tunaendelea kuwa washirika wa karibu – huu ukiwa ni mwaka wa pili mfululizo – na tunaahidi kuendelea kuwa sehemu ya safari hii ya mabadiliko ya kijamii.”

Usajili wa mbio hizo unaendelea kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz ambapo washiriki wanatakiwa kuchangia TZS 45,000 kwa mtu mmoja mmoja au TZS 42,000 kwa kila mshiriki wa kikundi chenye watu 30 au zaidi.


Endelea kufuatilia Blogu yetu kwa taarifa zaidi kuhusu matukio ya kijamii, miradi ya uwajibikaji wa kampuni, na habari za sekta ya fedha nchini.



No comments:

Post a Comment