Dodoma – Jumla ya Sh12.4 bilioni zimetolewa kwa zaidi ya wafanyabiashara 6,011 kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10, huku wanufaika wakipatiwa pia elimu ya fedha na uongozi ili kuimarisha usimamizi na uendelevu wa biashara zao.
Takwimu hizo zimetolewa na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB, Amanda Feruzi, wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Ukanda wa Ziwa Victoria (LVRLAC) unaoendelea katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma.
Fedha za Serikali Zilizotengwa kwa Makundi Maalum
Kwa mujibu wa Feruzi, fedha hizo ni sehemu ya Sh13 bilioni zilizotolewa na Serikali kwa NMB kwa ajili ya utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotengwa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Mpango huo unatekelezwa kwa mfumo wa majaribio katika Halmashauri sita ambazo ni:
- Jiji la Dar es Salaam
- Jiji la Dodoma
- Manispaa ya Songea
- Halmashauri ya Newala
- Halmashauri ya Bumbuli
- Halmashauri ya Itilima
Lengo la mfumo huo wa majaribio ni kupima ufanisi wa usimamizi wa mikopo hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya kifedha, huku ukilenga kuongeza uwazi, nidhamu ya matumizi na marejesho.
NMB Yajivunia Uzoefu wa Ufadhili wa Miradi
Feruzi amesema NMB ipo tayari kuendelea kushirikiana na Jumuiya hiyo kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kufadhili mikutano yao kila mwaka na kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya uwezeshaji wananchi.
Alieleza kuwa benki hiyo ina uzoefu katika mfumo wa Alternative Project Financing (APF), akibainisha kuwa imefanikiwa kutoa hati fungani, pamoja na taasisi nyingine, zenye thamani ya takribani trilioni moja.
.jpeg)




.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)









.jpeg)










