Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926

Absa Banner_170926

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Thursday, 20 May 2021

TIGO HOST INNOVATION WEEK PANEL DISCUSSION ON HOW TECHNOLOGICAL ADVANCEMENT CAN ENHANCE BUSINESS EFFICIENCY


Emmanuel Mallya - Chief Technical Officer at Tigo Tanzania explains how technical innovation has transformed our customer's businesses during a panel discussion on How Technological Advancement can Enhance Business Efficiency.
DIGITAL LIFESTYLE: "Technology has changed our lives, adoption of mobile money is very huge in Tanzania" Josina Njambi-Head of Innovation & Development @NMBTanzania during the panel discussion on how technological advancement can enhance business efficiency #IWTz2021 @innovationweektz
"Tigo are enablers for commerce/economy grow" Sameer Hirji - CEO @SelcomTanzania during the panel discussion on how technological advancement can enhance business efficiency.#IWTz2021 @innovationweektz
LIVING DIGITAL LIFE: "We are happy to work with Tigo ensuring that our community who have small saving & lending groups are able to access an app to enable them to operate in a better way" Marianna Balampama - Country Director PACT #BusinessEnhance#IWTz2021 @innovationweektz
"We have very strong, innovative and remarkable products and service" @SimonAKarikari Managing Director
#UbunifuNdioJadiYetu#MaishaKidigitaliNaTigo #TigoPesa#TigoBusiness#IWTz2021 @innovationweektz


ZANTEL YAJIZATITI KUBORESHA MTANDAO WA 4G ZANZIBAR

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Zantel, Aneth Muga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Zantel, Emmanuel Swai (kushoto) na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Zantel Kanda ya Pemba, Said Masoud Ali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Pasua Anga Ki Zantel 4G uliofanyika katika viwanja vya Gombani Kongwe visiwani Pemba. Kampeni hiyo imelenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.
  • Ni kupitia kampeni yake ya Pasua Anga Ki Zantel 4G inayotoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa 4G
Pemba, Mei 19, 2021 - Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, imeeleza mpango wake wa kueneza na kuboresha zaidi mtandao wa 4G katika kila kona ya visiwa vya Zanzibar ili kutoa fursa kwa watumiaji kunufaika na mtandao huo hasa kujiendeleza na shughuli za kiuchumi mtandaoni.

Mkakati huo ni sehemu ya kampeni yake mpya ijulikanayo kama ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ yenye lengo la kutoa elimu juu ya matumizi yenye tija ya mtandao wa 4G hususan kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika viwanja vya Gombani Kongwe visiwani Pemba, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Zantel, Aneth Muga alisema lengo kubwa ni kuhakikisha wateja wananufaika zaidi na matumizi ya intaneti mbali na matumizi ya mitandao ya kijamii.

“Leo tunafuraha kuwajulisha wateja wetu kuwa tumerudi tena na kampeni yetu hii mahsusi ili kuendelea kutoa elimu kwa wateja wetu juu ya manufaa mbalimbali yatokanayo na mtandao ulioboreshwa wa Zantel 4G,” alisema Muga.

ABSA BANK TANZANIA LAUNCHES THE FIRST VIRTUAL BRANCH ENGAGEMENT SOLUTION IN THE MARKET

Absa Bank Tanzania Finance Director, Obedi Laiser (left), cuts a ribbon to inaugurate the bank’s first virtual branch engagement solution to be hosted on WhatsApp. The event took place at Absa Mikocheni Branch in Dar es Salaam. Looking on from right are Absa Tanzania Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and bank’s Head of Customer Experience, Samuel Mkuyu.
Absa Bank Tanzania Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi, addresses attendees during the launching ceremony.
A cross-section of attendees watch the screen as Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed, speaks using teleconferencing facility.
Absa Mikocheni Branch Manager, Prisca Daudi, demonstrates how to use the just-launched Absa's virtual branch engagement solution in Dar es Salaam.
Absa Bank Tanzania Finance Director, Obedi Laiser (left), the bank’s Head of Customer Experience, Samuel Mkuyu, and Absa Tanzania Head of Retail Oscar Mwamfwagasi, in a buoyant mood during the official launch of the bank’s first virtual branch engagement solution to be hosted on WhatsApp.

Absa Bank Tanzania has launched its first ever virtual branch engagement solution to all customers. The new engagement solution is hosted on WhatsApp and will enable its customers to book their banking services and know the turnaround time per service prior to being attended to. The solution is aimed to fit into customers lifestyles and enhance their experience while at the branch.

Addressing the press to announce the system launch, the bank’s Managing Director, Abdi Mohamed said, “Absa’s aim is to become a digitally led bank while providing solutions which caters for our customers convenience and lifestyles. Our customers no longer need to wait aimless at the branch lobby, we are now in a position to engage them before they even arrive through their mobile phones.”

“We chose WhatsApp because it makes interacting with customers easy, private and personalized. Based off our market research at least 68% of WhatsApp users think using the platform is the easiest and most private way to connect. This system will also enable customers to share their feedback on their experience which will put more emphasis on how we can better improve our products and services. As a bank we are truly tapping into our customers lifestyles, by partnering with Fintech companies such as FastHub Solutions to provide more meaningful personalized moments for our customers”, said the Head of Customer Experience (CX) & Digital, Samuel Mkuyu.

Wednesday, 19 May 2021

DStv INAKULETEA RUMBLE IN DAR SECOND EDITION

 

Moja ya michongo ambayo inapaswa kuwepo kwenye ratiba yako mwezi huu ni hii ya pambano la #RumbleInDAR ambapo Mei 28, 2021 pale Next Door Arena ndipo pambano litafanyika.

Hakikisha umelipia kifurushi cha Bomba TShs 19,900 tu kwenye king'amuzi cha @dstvtanzania ili uweze kutazama pambano LIVE hapa @plustvtz kupitia DStv Channel namba 294 kuanzia saa 2 kamili usiku.

Piga *150*53# kulipia kifurushi chako mapema.

#vyanyumbanihuanziadstv

Tuesday, 18 May 2021

MKUTANO MKUU WA 26 WA WANAHISA WA BENKI YA CRDB KUWEKA HISTORIA MPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki hiyo unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Mei 22, 2021, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki. Kulia ni Mkurugeni wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na kushoto ni Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo.

Benki ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa siku ya Jumamosi tarehe 22/05/2021 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mkutano huo unafanyika kufuatana na Sheria ya Makampuni (Companies Act) namba 212 ya mwaka 2002, ambapo kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki.


Akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Mount Meru Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela amesema ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki mkutano huu muhimu, Benki ya CRDB imeandaa utaratibu kwa wanahisa ambao kwa namna moja au nyingine hawatoweza kufika Arusha waweze kushiriki mkutano wa kwa njia za kidigitali.


“Kwa kuzingatia uzoefu tulioupata kwa kufanya mkutano wa 25 kwa njia ya mtandao, wanahisa walipitisha pia azimio la mkutano wa 26 kufanyika kwa njia zote mbili kwa maana ya kuruhusu wanahisa wanaoweza kushiriki kwa kufika Arusha lakini pia kuruhusu wanahisa wanaoweza kushiriki kwa njia ya mtandao kutumia njia hiyo ambapo itakua ni historia kwa mkutano mkuu wetu kufanyika nama hii” alisema Nsekela.

Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa yake ili kukuza uelewa wa masuala mbalimbali ya fedha na uwekezaji katika masoko ya mitaji. Semina hiyo itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 21/05/2022 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mgeni Rasmi katika semina hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Mwigulu Nchemba ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wa masuala ya fedha, sheria na uwekezaji katika masoko ya mitaji.


Kwa mujibu wa Nsekela hii itakua ni mara ya kwanza kwa Mkutano wa Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB kufanyika kwa njia zote mbili ambapo mkutano wa mwaka jana ulikuwa wa kwanza kwa Benki kutumia njia za kidigitali ili kukabiliana na changamoto ya COVID-19. Zaidi ya wanahisa 1,400 waliweza kushiriki mkutano wa mwaka jana idadi ambayo haijawahi kufikiwa katika mikutano ya kawaida ambayo hufanyika jijini Arusha kwa miaka yote.

“Nachukua fursa hii kuwakaribisha wanahisa wote katika semina na mkutano mkuu na niwahakikishie wanahisa wote ambao watashiriki kwa njia ya mtandao kuwa tumejipanga vizuri katika kuhakikisha kila wanashiriki kama wanahisa ambao watakua AICC na tumeweka maelezo katika tovuti yetu ya Benki (www.crdbbank.co.tz) ya jinsi gani wanaweza kushiriki hatua kwa hatua” aliongeza Nsekela.


Pamoja na mambo mengine yatakayojadiliwa katika mkutano mkuu huo ikiwemo maboresho ya katiba ya kampuni, shauku kubwa kwa wanahisa ni kufahamu juu ya pendekezo la gawio kwa wanahisa kwa mwaka uliopita ukizingatia kuwa Benki ya CRDB imeendelea kupata matokeo mazuri sokoni ambapo katika hesabu za mwaka wa fedha ulioisha Benki iliweza kupata faida kabla ya kodi ya Shilingi Bilioni 236 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 kutoka Shilingi Bilioni 175 iliyopatikana mwaka 2019.

Monday, 17 May 2021

BENKI YA NMB KUFUNGUA FURSA KWA WATEJA KUPITIA WIKI YA UBUNIFU

Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu wa Benki ya NMB, Josina Njambi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi rasmi wa tamasha la Wiki ya Ubunifu (Innovation Week) iliyoanzishwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) na wadau mbalimbali. Benki ya NMB ni mdhamini wa wiki hiyo ya ubunifu.

Benki ya NMB imeazimia kufungua fursa zaidi kwa wateja wake kupitia huduma mbalimbali zinazoendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kurahisisha upatikanaji huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya wiki ya ubunifu ambapo NMB ni sehemu ya wadhamini jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Ubunifu kutoka benki hiyo, Bi. Josina Njambi alisema lengo la kuwa sehemu ya tukio hilo ni kutaka kujivuta karibu zaidi na wadau wanaojihusisha na ubunifu.

Alisema, Benki ya NMB ni miongoni mwa benki kubwa nchini iliyokuwa ya mwanzoni kutumia ubunifu kuwapa wateja huduma wanazostahiki ikiwemo huduma ya NMB Mkononi.

“Tulipunguza mlolongo wa wateja kupanga foleni kwenye matawi yetu kwa kutoa huduma ya benki kwa simu za mkononi, tulipunguza mlolongo kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) kwa kuanzisha NMB Wakala nchi nzima, huu ni ubunifu wa kipekee tuliopata kuufanya,” alisema Bi. Njambi.

Thursday, 13 May 2021

DStv INAKULETEA JUA KALI NDANI YA MAISHA MAGIC BONGO

 

Leo kwenye Jua Kali, Stella anaendelea kumuwashia moto Thomas kisa Maria, Mrs Bill aonyesha wazi kumtaka Dr Temba kimapenzi, huku Sophia akipokea taarifa mbaya ya ugonjwa wa mama yake!

Ni ndani ya @maishamagicbongo kupitia @dstvtanzania pekee saa 3:30 usiku!

Piga *150*53# kulipia kifurushi Bomba TShs 19,900 tu.

#vyanyumbanihuanziadstv

DStv INAKULETEA KAIZER CHIEFS VS SIMBA FC LIVE

 

Ni mwendo wa bandika bandua kupitia #SokaLisilopimika pekee!

Tazama Kaizer Chiefs vs Simba FC kupitia chaneli 270.

WAKAZI WA KATAVI WAIPOKEA BENKI YA NBC KWA SHANGWE

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, Meneja wa Huduma za NBC Wakala, Robert Madaki, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya hiyo, Elibariki Masuke, na kulia ni Wakala wa ofisi hiyo Emmanuel Atimili.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera (katikati), akikata keki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Wakala Mkuu wa huduma ya NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, pamoja na Maofisa wengine kutoka Benki hiyo na Wakala wa Ofisi hiyo Emmanuel Atimili.

Taarifa kwa Umma Mei mwaka huu 2021 Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Benki ya NBC kwa kuzindua NBC Wakala Plus katika Manispaa ya Mpanda kwani kwa kuwepo kwa wakala mkuu huyo kutafungua fursa za kiuchumi, kuziendeleza pamoja na kuinua uchumi wa wafanyabiashara katika Mkoa huo.

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo la NBC Wakala Plus, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera ameupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu ambapo watu zaidi ya elfu moja wamefungua akaunti katika tawi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Komredi Homera aliupongeza uongozi wa Benki ya NBC kwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Katavi. Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda. Komredi Homera pia aliusihi uongozi wa Benki ya NBC kutoa mikopo kwa wajasiriamli wa Katavi ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwa haraka.

Aidha Homera ameishukuru Benki ya NBC kwa kutoa msaada mifuko 300 ya saruji, Bati 60 sambasamba na ndoo 5 za rangi katika Cho Cha Afya huku benki hiyo ikiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa mawili katika chuo hicho.

Tuesday, 11 May 2021

DStv INAKULETEA MPALI KILA JUMATATU - ALHAMISI


Mpali inazidi kuwa 🔥🔥🔥

Tazama visa hivi vya Nguzu na familia yake kila siku ya Jumatatu - Alhamisi saa 12:00 jioni kupitia @maishamagicbongo, Chaneli 160.

Piga *150*53# kulipia kifurushi Bomba sh 19,900 tu.

#vyanyumbanihuanziadstv

KCB GROUP TO SPEND SH6BN IN BUYING RWANDAN, TANZANIAN BANKS

KCB Group CEO Joshua Oigara (right) Chairman Andrew Kairu (centre) and Group CFO Lawrence Kimathi during the release of the full-year results.

KCB Group will spend a total of Sh6 billion to acquire two banks in Rwanda and Tanzania from London-listed Atlas Mara limited.

The Nairobi Securities Exchange-listed firm had earlier estimated it would acquire a 62 percent stake in Banque Populaire du Rwanda Plc (BPR) and a 100 percent ownership in African Banking Corporation Tanzania Limited at a cost of $40 million (Sh4.2 billion).

The amount has increased after KCB sought to make a full buyout of the Rwandan bank by making an offer to its minority shareholders who hold a combined 38 percent stake.

“The group has made an offer to the remaining shareholders of BPR for the acquisition of the remaining stock at the same terms as Atlas Mara's to raise its ownership to 100 percent,” KCB says in its latest annual report.

“Once approved, the aggregate completion consideration that would be payable by KCB for acquisition of the combined assets is estimated at current values and exchange rates to be $56.9 million (Sh6 billion).”

Atlas Mara is selling its African banks to KCB and other lenders to raise funds to pay its creditors, some of whom have launched liquidation proceedings against the multinational that was the brainchild of former Barclays Plc’s chief executive Bob Diamond.

I&M BANK COMPLETES ACQUISITION OF UGANDAN LENDER


I&M Holdings Plc. has completed the acquisition of 90 percent shareholding in Uganda’s privately-owned lender Orient Bank Ltd (OBL) as part of its regional expansion plan.

In a statement Monday, I&M said the acquisition was completed on April 30, 2021 after the transaction received the necessary approvals from the Central Bank of Kenya, Bank of Uganda, Capital Markets Authority of Kenya and the Common Market for Eastern and Southern Africa (Comesa).

The agreement for the deal priced at Ush96.75 billion ($26.93 million) was made in July last year.

“I&M Group aspires to be Eastern Africa’s leading financial partner for growth. The acquisition of OBL will place I&M Bank in an advantageous position to capitalise on the growth in the Eastern African economies and thereby ultimately increasing shareholder value,” said Sarit Raja Shah, I&M’s Group Executive Director.

Continue Reading > > >

CLYDE & CO UPDATER - TANZANIA ISSUES NEW MINING RULES ON DISPUTE RESOLUTION


Tanzania recently issued new Mining (Disputes Resolution) Rules, directly impacting companies and individuals operating in the mining sector and revoking the previous rules in effect. In this article, we provide an overview of the new rules and the key implications to consider.

Background

The Mining (Disputes Resolution) Rules (the Rules) which are made under section 122 of the Mining Act Cap 123 Revised Edition 2019 (the Mining Act), were published in the Government Gazette dated 16 April 2021 and repeal the Mining (Disputes Resolution) Rules Government Notice No. 224 of 1999.

Application of the Rules

The Rules will directly affect persons engaged in prospecting or mining operations and any third parties but not the Government. This means that the Executive Secretary of the Mining Commission (the Commission) will have power to inquire into and decide disputes between the abovementioned persons. The law permits this power to be delegated to any officer of the Commission who holds - at a minimum - the rank of a director.

Section 119(1)(a)-(d) of the Mining Act provides that the Commission will decide disputes in connection with:
  • boundaries of areas subject to mineral rights;
  • claims by any persons entitled to erect, cut, construct or use any pump, line of pipes, flume, race, drain, dam or reservoir for mining purposes, or to have priority of water taken, diverted, used or delivered, as against any other person claiming the same;
  • assessment and payment of compensation in line with the Mining Act; and
  • any other matter which may be prescribed by law.

The Commission

The Commission is managed by the Executive Secretary who is the Chief Executive Officer. The Executive Secretary is appointed, for a term of five years, by the President of the United Republic of Tanzania to oversee the management of the Commission. After the five year tenure, the Executive Secretary will be eligible for re-appointment.

Monday, 10 May 2021

BENKI YA NMB YADHAMINI MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya thamani ya sh milioni 15 kutoka kwa Mhazini Mkuu wa Benki ya NMB, Azizi Chacha jana kwa ajili ya udhamini wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliyoanza jana uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri Elimu, Omari Kipanga na watatu ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo.

Dodoma - Benki ya NMB imekabidhi kitita cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya udhamini wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) yaliyofunguliwa rasmi jana Jijini Dodoma.

Akizungumza jana Mhazini Mkuu wa Beniki ya NMB, Azizi Chacha alisema benki hiyo imetoa fedha hizo ikiwa ni udhamini wa mashindano hayo yanayoandaliwa na Serikali kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Chacha alibainisha kuwa lengo la NMB kutoa fedha hizo ni kuisaidia Serikali katika kufanikisha mashindano hayo ya Kitaifa ambayo yamekuwa na malengo ya kuibua wabunifu wapya kila mwaka.

BENKI YA NBC YAZINDUA KLABU YA WAFANYABIASHARA MKOANI KIGOMA

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta (wapili kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi wakifurahia baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa wa Kigoma uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika wenye lengo la kuwakutanisha wateja wake wafanya biashara na wenye viwanda na wadau wengine. Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanayabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya NBC, Mussa Mwinyidaho pamojana Mteja wa Benki hiyo, Marietha Patrick.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta (wa sita kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa saba kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma baada ya uzinduzi rasmi wa NBC Biashara Club kwa Mkoa huo uliofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Benki ya NBC imezindua klabu ya wafanyabiashara wa benki hiyo mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya mipango ya benki hiyo kusogeza huduma kwa wateja wake sambamba na kujenga mtandao ambao utawasaidia wafanyabiashara wateja wa benki hiyo kufanya biashara zao kwa tija.

Theobald Sabi ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC,Theobald Sabi akizungumz kwenye uzinduzi wa klabu hiyo ya wafanyabiashara kwa mkoa Kigoma alisema kuwa lengo kubwa la klabu hiyo kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kwenye sekta ya biashara kuzungumza kwa pamoja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao na kuzitatua.

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA MIFUKO 500 YA SARUJI MKOA WA KIGOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi (wanne kulia) akikabidhi msaada wa mifuko mia tano 500 ya saruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule mkoani humo. Mifuko hiyo ilipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchatta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Nd Thobias Adengenye. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma.

Benki ya Taifa ya Biashara imekabidhi mifuko 500 ya seruji kwa Mkoa wa Kigoma kusaidia juhudi za serikali za ujenzi wa madarasa mkoani humo. Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma, Nd Rashid Mchata akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Thobias Andengeye pamoja na kuishukuru Benki ya NBC alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa kutokana na muamko wa wazazi wa Kigoma kupeleka watoto shule kufuatia maamuzi ya serikali kutoa elimu bure.

“Tunategemea wanafunzi wapatao 40,771 kuhitimu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 kuepelekea uhitaji wa madarasa ziaidi ya 1,010 huku mkoa wetu ukiwa na madarasa 405, hivyo mchango wa Benki ya NBC wa mifuko 500 ya saruji utaisaidia kusukuma malengo serikali yetu ya mkoa kukamilisha ujenzi wa madarasa zaidi ya 605.” Alisema Nd Mchata.

ABSA BANK TANZANIA CO-SPONSORS FINTECH & HEALTHTECH YOUTH ENTREPRENEURS IN THE INAUGURAL WAZO CHALLENGE TANZANIA DEMO DAY


Absa Bank Tanzania announced youth entrepreneurial winners of the Wazo Challenge Tanzania Demo Day. The program was managed and organized by Startup Réseau; an India-headquartered startup accelerator which kick-started its East Africa expansion with the inaugural edition of the "Wazo Challenge Tanzania", announced in February 2021.

Wazo Challenge Tanzania focussed on 5 thematic areas - Financial Services, Healthcare, Agriculture, Energy / Utility and Education. As a part of the program, Startup Réseau hosted a Venture Bootcamp, wherein 10 high-potential founders were selected for a 4-week venture mentorship and leadership development bootcamp, that was delivered by successful founders, industry leaders, domain experts and investors from Startup Réseau’s global network. The Venture Bootcamp also had a parallel track of “Office Hours” wherein 15 more startups from the application pool were mentored.

This one-month long venture development bootcamp operated from March - April 2021 having winners compete for a cash grant of USD 10,000 determined by the stage of startups, the founders’ vision, uniqueness, market opportunities and clarity of business model. The grant money was disbursed as Top-3 prizes of USD 5,000 (Kikoba App), USD 3,000 (Mipango App) and USD 2,000 (MedPack)

Saturday, 8 May 2021

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKABIDHI MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 220 MACHOCHWE

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Nurdin Babu, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Machochwe, Martha Marwa baada ya kuzindua kisima kilichochimbwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika kijiji hicho. Mradi huo una thamani ya Shilingi 220 milioni ambapo wakazi 12,000 watanufaika. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL, John Wanyancha.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, Nurdin Babu, akizungumza kwenye uzinduzi wa kisima kilichochimbwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika kijiji cha Machochwe. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Water Aid, Anna Mzinga na Mkurugenzi wa Mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha(kulia).
Viongozi wa kimila wa Machochwe Wilayani Serengeti (walioshika fimbo) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha mji chenye thamani ya shilingi milioni 220 kilichochimbwa kwa uafadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kinaweza kuhudumia watu 12,000.
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), John Wanyancha akizungumza wakati wa kukabidhi kisima katika kijiji cha Machochwe Mkoa Mara.

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi 220m/- katika Kijiji cha Machochwe kilichopo wilayani Serengeti Mkoani Mara ikiwa ni jitihada zake za kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji salama kwa wananchi wa eneo hilo.

Mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia watu 12,000, unahusisha uchimbaji wa kisima,ununuzi wa tanki la maji na pampu yenye uwezo wa kuvuta lita 7,500 kwa saa.

Akizungumza wakati wa kukabidi kisima hicho, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL John Wanyancha alisema kampuni hiyo kupitia mradi wa ‘Maji ni Uhai’ imesaidia uchimbaji wa visima vilivyosaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ikiwamo Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa zaidi ya watu milioni moja.

BENKI YA CRDB YAKUSANYA WADAU KUJADILI UVUMBUZI KATIKA SEKTA YA FEDHA

Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe akiongoza Kongamano lililoandaliwa kwa kushirikiana kati ya Benki ya CRDB na Vodacom Tanzania na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma. Hii ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).

Meneja Mwandamizi wa Huduma za Ziada wa Benki ya CRDB Ndugu Mangire Kibada akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.


Dodoma, Mei 06, 2021 – Benki ya CRDB imefanya kongamano lililobeba mada ya “Ni kwa namna gani sekta ya fedha inapaswa kuenenda kwa mwaka 2021?” ukizingatia dunia inapita katika changamoto ya janga la COVID-19 liloshika kasi mwaka 2020. Kongamano hilo lilioandliwa kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom liliongozwa na Mkurugenzi wa FSDT, Sosthenes Kewe na kuhudhuriwa na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya uvumbuzi “Innovation Week” ambayo yataambatana na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliasisiwa mwaka 2019 kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Friday, 7 May 2021

NCBA BANK TANZANIA APPOINTS JULIUS KONYANI AS AN EXECUTIVE DIRECTOR


NCBA Bank Tanzania Limited has appointed Julius Konyani to the Board of Directors as an Executive Director following the redeployment of Gift Shoko to NCBA Bank Kenya as the Group Director, Regional Subsidiaries. This appointment has also been approved by Bank of Tanzania (BOT).

Konyani brings to the board over 17 years of extensive experience and expertise in Banking and Management having served in an array of leadership roles in banks locally, including CRDB Bank PLC, NMB Bank PLC, United Bank of Africa (T) LTD the Defunct Commercial Bank of Africa Tanzania among others.

Konyani is currently the NCBA Tanzania, Head of Retail and Business Banking where he has been instrumental in strengthening and growing its retail business following the merger of NIC and Commercial bank of Africa (CBA) in 2019. He was also the country project lead for the successful integration of the two banks which gave birth to NCBA effective July 2020.

BENKI YA NMB YABORESHA BIMA YA FARAJA, YATAMBULISHA BIMA YA VIKUNDI

Mkuu wa Kitengo cha Bima (Head of NMB Bancassurance Department) cha Benki ya NMB, Martine Massawe (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Bima ya Maisha. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Life (CEO), Amani Boma na kulia ni Meneja Mkuu wa Biashara ya Makampuni Sanlam, Nura Masood.

Kwa mara nyingine Benki ya NMB imedhihirisha kauli mbiu yake kuwa ipo karibu na wateja, imekuja na maboresho ya huduma zake za bima ili kuhakikisha Watanzania wanapata faraja wakati wa matatizo.

Benki hiyo inashirikana na kampuni mbili za bima, Metropolitan Life na Sanlam Life ambapo watakuwa na utaratibu wa kutoa bima za maisha na vikundi kwa wateja na wasio wa NMB, katika kuangalia matarajio ya wateja wao baadae ikitokea hatari katika maisha yao na hivyo kusaidia malengo ya wateja kufikiwa hata kama wao hawapo au wamepata ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Bima NMB, Martine Massawe alisema wameiboresha huduma ya bima ya NMB Faraja kwa kuongezea kiasi cha fedha kinachotolewa lakini pia kuongeza kpengele cha ulemavu wa kudumu atakaopata mteja pia atalipwa lakini pia wamekuja na hudma mpya ya bima kwa vikundi.

WANUFAIKA WA KILIMO - VIWANDA WATEMBELEA KIWANDA CHA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI MWANZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries, Mark Ocitti, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, wakati wanafunzi ambao ni wanufaika wa programu ya Kilimo-Viwanda kutoka Chuo cha kilimo cha Igabiro Wilayani Muleba, Mkoani Kagera walipotembelea kiwanda cha Mwanza kujionea uzalishaji wa bia. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Sadock Stefano.

Mpishi wa bia wa zamu (Shift Brewer) Christina Machaka akiwaeleza namna bia inavyopikwa kwenye mitungi maalum wanafunzi wa Chuo cha Kilimo lgabiro walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Serengeti Tawi la Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo kupitia wa programu ya Kilimo-Viwanda inayoendeshwa na Kampuni ya Serengeti.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo lgabiro cha Mkoani Kagera, Neema Michael, akizungumza jinsi alivyonuifa kwa kulipiwa ada na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia programu ya Kilimo-Viwanda, ambapo wanafunzi wa Chuo hicho walitembelea Kiwanda cha Mwanza. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries, Mark Ocitti na anayefuatia ni Mkuu wa Chuo hicho, Sadock Stephano.
Wanafunzi wa Chuo cha Kilimo Igabiro kilichopo Muleba Mkoani Kagera ambao ni wanufaika wa programu ya ufadhili wa mosomo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti inayojulikana kama Kilimo-Viwanda wakiwa lkatika ziara ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Mwanza.

Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imejidhatiti kuwapa wanafunzi nyenzo na mafunzo zaidi ya kivitendo kama njia mojawapo ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kilimo nchin Tanzania.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti katika tukio la kuwapongeza wananfunzi 17 waliopata nafasi za ufadhili kupitia programu hii kutoka chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture kilichopo mkoa wa Kagera. SBL imelenga kufanya haya kupitia program hii maarufu inayojulikana kama Kilimo Viwanda inayolenga kusaidia wanafunzi kutoka familia masikini ili waweze kusomea masomo ya kilimo kwenye ngazi ya diploma katika vyuo vya ndani.

Wednesday, 5 May 2021

BENKI YA NMB YAENDESHA DROO YA 'BONGE LA MPANGO'

Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akibofya kitufe kumpigia mmoja wa washindi kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.

Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbezi Louis, Nestory Mwombeki (kushoto) akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo tawini hapo. Wa pili kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo wakiwa kwenye hafla hiyo.

Tuesday, 4 May 2021

TAZAMA NUSU FAINALI ZA UEFA LIVE NDANI YA DStv

 

Ule muda uliokuwa ukisubiriwa sasa umewadia!

Nusu fainali za UEFA zitakazoamua timu zitakazoingia fainali.

Je wewe utabiri wako unautupia wapi...?

Piga *150*53# kulipia sasa kifurushi chako cha Compact Plus TShs 89,000 tu ili usikose mechi hizi.

#SokaLisiloPimika