Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki hiyo unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Mei 22, 2021, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki. Kulia ni Mkurugeni wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na kushoto ni Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo.
Benki ya CRDB inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa siku ya Jumamosi tarehe 22/05/2021 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mkutano huo unafanyika kufuatana na Sheria ya Makampuni (Companies Act) namba 212 ya mwaka 2002, ambapo kila mwaka Benki ya CRDB imekuwa ikiandaa mkutano huo unaowapa Wanahisa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha au kuidhinisha maamuzi mbalimbali yenye maslahi kwa Benki.

Akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Mount Meru Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela amesema ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki mkutano huu muhimu, Benki ya CRDB imeandaa utaratibu kwa wanahisa ambao kwa namna moja au nyingine hawatoweza kufika Arusha waweze kushiriki mkutano wa kwa njia za kidigitali.
Mkutano Mkuu wa 26 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa yake ili kukuza uelewa wa masuala mbalimbali ya fedha na uwekezaji katika masoko ya mitaji. Semina hiyo itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 21/05/2022 kuanzia saa 3 asubuhi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Mgeni Rasmi katika semina hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Mwigulu Nchemba ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wa masuala ya fedha, sheria na uwekezaji katika masoko ya mitaji.
“Nachukua fursa hii kuwakaribisha wanahisa wote katika semina na mkutano mkuu na niwahakikishie wanahisa wote ambao watashiriki kwa njia ya mtandao kuwa tumejipanga vizuri katika kuhakikisha kila wanashiriki kama wanahisa ambao watakua AICC na tumeweka maelezo katika tovuti yetu ya Benki (www.crdbbank.co.tz) ya jinsi gani wanaweza kushiriki hatua kwa hatua” aliongeza Nsekela.
No comments:
Post a Comment