Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Friday, 21 August 2026

VODACOM YAKABIDHI MADARASA MAWILI KWA SHULE YA MSINGI MAHILO RUVUMA, KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania Plc, Abednego Mhagama, wakati alipowasili katika hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma, kupitia programu ya Vodacom Tanzania Foundation.

Madarasa hayo yanalenga kuwapatia wanafunzi na walimu mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, na ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa.

Katika awamu hii, shule tatu za msingi za umma katika mikoa ya Pwani, Ruvuma na Morogoro zimenufaika na mpango huo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Agosti 20, 2026, katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (katikati), akipokea maelezo kuhusu madarasa mawili yaliyokabidhiwa na Vodacom Tanzania Plc katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma, kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania Foundation za kuimarisha miundombinu ya elimu kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa.

Katika awamu hii, shule tatu za msingi za umma katika mikoa ya Pwani, Ruvuma na Morogoro zimenufaika. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Agosti 20, 2026, katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani Ruvuma. Wengine pichani ni Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa kampuni hiyo, Abednego Mhagama (kushoto), na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed (katikati, waliokaa), na Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania, Abednego Mhagama (wa tatu kushoto, waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali mkoani Ruvuma pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Mahilo, mkoani humo, kupitia programu ya Vodacom Tanzania Foundation.

No comments:

Post a Comment