Dar es Salaam, Tanzania — Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imewakutanisha wadau kutoka tasnia mbalimbali ikiwemo ulimbwende, mavazi, ubunifu, ujasiriamali na taaluma nyingine katika mkakati maalum unaolenga kujiandaa kwa uzinduzi mkubwa wa kinywaji chake kipya, Serengeti Premium Apple, kinachozalishwa hapa nchini.
Kikao hicho kilifanyika katika mgahawa wa hadhi ya juu wa Upper Deck jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa SBL wa kuhakikisha wadau muhimu wanaelewa kwa kina mwelekeo wa chapa kabla ya uzinduzi rasmi. Kupitia jukwaa hilo, washiriki walipata maelezo ya kina kuhusu historia ya chapa, nafasi yake sokoni, pamoja na maono ya Serengeti Premium Apple na kile inachowakilisha kwa mlaji wa kisasa wa Kitanzania.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Wema Mugofwa alieleza kuwa bidhaa hiyo mpya inaashiria hatua nyingine muhimu katika safari ya ubunifu wa kampuni hiyo:
“Serengeti Premium Apple ni ishara mpya ya dhamira yetu ya kuendeleza ubunifu na ubora wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini. Kama kinywaji chenye ladha ya kipekee na hadhi ya juu kilichotengenezwa Tanzania, kinaakisi mabadiliko ya ladha na mahitaji ya wateja wa kisasa wanaothamini ubora, mtindo wa maisha na uhalisia wa mazingira wanayoishi. Tunapojiandaa kwa uzinduzi rasmi, tunafurahia kushirikiana na wabunifu wa maudhui watakaosaidia kusimulia hadithi hii kwa njia halisi na yenye kuvutia,” alisema.
Mbali na uwasilishaji wa taarifa, kikao hicho kilitoa nafasi ya majadiliano ya wazi kati ya wadau na timu ya masoko ya SBL. Washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni, na kupata uelewa wa kina kuhusu mikakati ya uzinduzi pamoja na shughuli mbalimbali zitakazoandamana na tukio hilo.
Wadau wengi waliohudhuria walionesha shauku kubwa ya kuwa sehemu ya uzinduzi huo, wakivutiwa na ubunifu uliotumika katika maandalizi pamoja na maudhui yaliyowasilishwa wakati wa kikao hicho.
Huku maandalizi yakifikia hatua za mwisho, matarajio yanaendelea kuongezeka kuelekea tukio hilo linalotarajiwa kuwa la kipekee na tofauti na yaliyowahi kushuhudiwa nchini. Kwa dalili zote, uzinduzi wa Serengeti Premium Apple unaelekea kuwa sio tu tukio la bidhaa mpya, bali pia jukwaa la kuandika historia mpya katika tasnia ya vinywaji nchini Tanzania.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment