Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bi. Juliana Lukwaro (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) na kusindikizwa na msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja (kwa nyuma mwenye rasta) na George Venanty, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini (kwa nyuma mwenye miwani) katika viwanja vya Stendi Kuu mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo. |
No comments:
Post a Comment