Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amefungua tawi jipya la Tanzania Commercial Bank (TCB) mkoani humo ikiwa ni katika harakati za kupanua wigo wa biashara na kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, Shigella alisema kuwa kufunguliwa kwa tawi hilo kutawezesha kupatikana kwa ajira za kudumu katika tawi hilo.
Shigella aliongeza kuwa benki hiyo itawezesha wafanyabiashara wadogo wakati na wale wakubwa na vikundi vidogovidogo kuendelea kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kuendelea kukuza mitaji yao.
“Sisi wana Geita tutafaidika na mikopo hii, na riba yake ni miongoni mwa benki inayotoa riba nzuri kuliko benki zingine, utapewa riba nzuri na muda wa kutosha kuzalisha fedha zako na kuirudisha”, Alisema Shigella.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 10 benki imeongeza mali za benki hiyo kutoka bilioni 121 hadi kufikia trillion 1 na bilioni 400 na kuongeza idadi ya matawi kutoka 30 hadi kufikia matawi 80 hivyo kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 400 hadi kufikia wafanyakazi 1,200.
Kwa upande wake Meneja wa Tanzania Commercial Bank, Andrew Mziray alisema kuwa Benki hiyo imejipanga kutoa fursa kwa wachimbaji wadogowadogo kwa kuwapa mikopo kwa ajili ya vifaa vya kufanyia shughuli za uchimbaiji.

No comments:
Post a Comment