Katika kuwezesha urahisi wa malipo:
- Mteja ataweza kulipa kianzio cha Tsh 20,000 kisha kulipa kuanzia Tsh 900 tu kwa siku.
- Mteja anaweza kuchagua pia kufanya malipo kwa wiki au mwezi.
- Mteja anaweza kujiunga na huduma hii kupitia menu ya M-Pesa, kisha kufika kwenye duka lolote la Vodacom kuchukua simu yake.
- Kwa mwaka huu zitatolewa simu milioni moja kwa wateja ambao watakidhi vigezo vya kukopeshwa.
“Ubia huu una tija kwani utafungua uchumi wa kidijitali na kutengeneza fursa za ziada kwa Watanzania.”
“Ushirikiano huu utaongeza kasi ya kuleta huduma za kifedha nchini, na unaenda kuongeza nguvu kwenye kampeni yetu ya "Teleza Kidijitali" inayolenga kuwafikia watu wengi nchini na huduma jumuishi za kifedha,” aliongeza.
Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku alisema: “Maoni yetu daima ni kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali na kubadilish maisha kupitia teknolojia. Hivyo, ushirikiano huu unaenda sambamba na azma yetu ya kuwafungulia wateja wetu fursa zinazobadilisha maisha.”
No comments:
Post a Comment