Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 2 August 2023

NBC, TIRA WATANGAZA USHIRIKIANO UENDESHAJI WA AKAUNTI YA DHAMANA

Kamishna wa Bima nchini ambae pia ni Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware (wa tatu kushoto) sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa tatu kulia) wakizindua ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA. Ushirikiano huo umetangazwa rasmi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi iliyokwenda sambamba na semina kwa wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini. Wengine ni maofisa waandamizi kutoka taasisi hizo mbili.
Kamishna wa Bima nchini ambae pia ni Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware (kushoto) sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) wakijipongeza kufuatia uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na wageni waalikwa wakati wa semina iliyoambatana na uzinduzi wa ushirikiano baina ya TIRA na Benki ya NBC katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa semina iliyoambatana na uzinduzi wa ushirikiano baina ya benki hiyo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa TIRA Bw. Abubakar Ndwata akizungumza na wageni waalikwa wakati wa semina iliyoambatana na uzinduzi wa ushirikiano baina ya TIRA na Benki ya NBC katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.
Kamishna wa Bima nchini ambae pia ni Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware (kushoto) sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta bima nchini wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini hatua inayolengea kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia semina hiyo.
Dar es Salaam, 01 Agosti 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza ushirikiano wetu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) katika uendeshaji wa Akaunti ya dhamana (Trust Account) kwa kampuni za bima nchini. Hatua hiyo kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima nchini ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.

Ushirikiano huo umetangazwa rasmi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi iliyokwenda sambamba na semina kwa wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakiwemo viongozi waandamizi kutoka TIRA, Benki ya NBC pamoja na wawakilishi wa makampuni ya bima nchini wakiwemo wakurugenzi na maofisa wa fedha wa kampuni hizo.

Akizungumzia hatua hiyo Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo A. Saqware ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TIRA ameipongeza benki ya NBC kwa kuanzisha akaunyo hiyo huku akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia sekta hiyo kuachana na utaratibu wa awali uliokuwa na mapungufu kadhaa.

"Awali changamoto ilikuwa ni kwamba kampuni nyingi za bima zilikuwa zikitumia fedha za amana ya Akiba katika matumizi mengine, pasipo kupata idhini ya TIRA hivyo kupelekea kuingia katika changamoto ya ukwasi, na wakati mwingine kushindwa kulipa fidia kwa wateja kutokana na fedha kuwekezwa katika miradi mingine." Alibainisha.

Aidha, alibainisha kuwa uamuzi wa kufungua Akaunti ya Dhamana ya Bima katika benki za biashara ni suluhisho la changamoto hiyo, kwakuwa sasa TIRA itaweza kusimamia moja kwa moja fedha hizo za amana za akiba, jambo ambalo si tu litaimarisha usimamizi, bali pia litaboresha maendeleo ya sekta ya bima nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi ameishukuru TIRA kwa kuipa fursa Benki ya NBC kushiriki katika uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Bima kwani uamuzi wa uanzishwaji wa akaunti hiyo utakuza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya bima.

Sabi alipongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa akaunti hiyo na kusisitiza kuwa ina mchango mkubwa katika kukuza uwazi zaidi na uwajibikaji katika sekta ya bima, na kwamba itasaidia pia kujenga imani kwa wadau wa sekta hiyo.

“Benki ya NBC imejipanga vyema katika kutoa ushauri wa uwekezaji kupitia Idara yetu ya Hazina na Masoko ya Mitaji” alisema Bw Sabi huku akitoa wito kwa makampuni ya bima nchini kutumia Akaunti ya dhamana (Trust Account) ili kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.

Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa TIRA Bw. Abubakar Ndwata amesema chimbuko la Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni Kanuni ya Bima ya mwaka 2009 inayozitaka Kampuni za Bima kuweka Amana za Usalama angalau 50% ya kiwango cha chini cha mtaji halisi wa kampuni husika ya bima.

Ndwata amesema TIRA kwa kushirikiana na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI), walikubaliana kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji wa Usimamizi wa Ukwasi ambao pia ulielekeza uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Akiba kupitia benki za biashara ili kuondokana na tatizo la changamoto ya kimtaji au kushindwa kulipa fidia za madai ya wateja wake.

No comments:

Post a Comment