Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 21 July 2023

NBC YASAINI MKATABA NA WIZARA YA ELIMU KUTOA UFADHILI WA MASOMO YA UFUNDI

Waziri wa wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda (wa tatu kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) akisaini mkataba pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. James Mdoe (kulia). Kupitia mkataba huo uliosainiwa jijini Dodoma, Benki ya NBC itatoa ufadhili wa masomo ya ufundi kwa wanafunzi 1,000. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Benki ya NBC.

Waziri wa wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda (katikati) akishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. James Mdoe (kulia) wakibadilishana nakala za mikataba. Kupitia mkataba huo uliosainiwa jijini Dodoma, Benki ya NBC itatoa ufadhili wa masomo ya ufundi kwa wanafunzi 1,000. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Benki ya NBC.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano kati ya Benki hiyo na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kupitia mkataba huo uliosainiwa jijini Dodoma, Benki ya NBC itatoa ufadhili wa masomo ya ufundi kwa wanafunzi 1,000.

Dodoma, Julai 20, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini mkataba wa makubaliano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknalojia kwa ajili ya kutoa ufadhili wa masomo ya ufundi kwa vijana wa Kitanzania.

Katika makubaliano hayo, NBC itaanza kutoa udhamini wa masomo kuanzia mwaka huu 2023 na imetenga jumla ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya programu hiyo mpya.

Wanufaika wa programu watakuwa ni vijana wa Kitanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na ambao wanatoka katika familia zenye vipato duni. Programu itasimamiwa na Wizara Elimu, Sayansi na Teknalojia na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wataitekeleza.

Ufadhili huo wa masomo unaojulikana kama NBC Wajibika Scholarship, unalenga kuwapatia vijana ujuzi katika fani mbali mbali ikiwa ni jitihada za kuwafanya waweze kujiajiri na kuajiriwa. Mafunzo yatakuwa yakitolewa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA).

Akiongea wakati ya hafla ya makubaliano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknalojia, Profesa Adolf Mkenda alisema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaweza kutatuliwa kwa kuwasaidia vijana kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri.

“Watanzania wengi wana umri kati ya miaka 15 na 45 na Serikali peke yake haiwezi kuwapatia ajira wote. Hata hivyo, kama kundi hili linapatiwa ujuzi sahihi wa kiufundi wanaweza kujiajiri wenyewe na kuwaajiri vijana wengine,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema Benki hiyo inaendelea kuwekeza kwa jamii. “Tunayofuraha kuwa ushirikianio wetu huu na Serikali kupitia wizara ya elimu utawezesha vijana 1,000 kupata mafunzo ya ufundi na hivyo kuweza kujiajiri”

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, NBC inajivunia kupata fursa ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao. “Tuna wajibu wa pamoja wa kuhakisha tunaliingiza kundi hili kubwa kwenye soko la ajira na kwa msingi huo benki ya NBC inafurahia kuanzisha programu ya ufadhili wa masomo maarufu kama Wajibika Scholarship ambayo itatoa mafunzo ya muda mfupi na kuwapatia vijana ujuzi utakaowasidia kujiajiri,” alisema.

Sabi alifafanua kuwa wanufaika pia watafaidika na programu mbali mbali za benki hiyo zitazowasaidia kukua ikiwa ni pamoja na, NBC Kuanasi, Klabu za kibiashara za NBC, ushauri wa kifedha, mikopo na kuunganishwa na masoko.

No comments:

Post a Comment