Wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakiwa katika picha ya pamoja, katika halfa ya sherehe ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NCBA katika halfa ya wiki ya huduma kwa wateja, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
Meneja Masoko wa benki ya NCBA akisema jambo na wafanyakazi na wateja wa benki hiyo katika hafla ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA, Julius Konyani akiongea katika hafla ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wateja wa benki ya NCBA, Amina Aly (kulia) akisalimia na mteja mwenzie pamoja na Dennis Chacha pembeni kulia. |
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA, Julius Konyani, akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Mbaraka Kihame, Amina Aly, Dennis Chacha na Serphin Lusala. |
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA, Julius Konyani, wakati wa Hafla ya wiki ya huduma kwa wateja iliyohudhuriwa na wafanyakazi na wateja wa NCBA katika jengoi la makao makuu lililopo jijini Dar es Salaam.
Konyani alisema, “Kupitia mbinu yetu ya kwanza ya kidijitali, tutaendelea kubuni na kutumia nyenzo bora za kiteknolojia katika huduma kwa wateja, ili kuendelea kutoa huduma za kipekee za kifedha na bidhaa zinazozidi matarajio ya wateja, na viwango vinavyokubalika kimataifa,”
Aliendelea kwa kusema ”Ukubwa na kiwango katika biashara ni muhimu na vinatupa NCBA nafasi ya kuwapa wateja uchaguzi mpana wa bidhaa na mbinu za utoaji huduma hizo. Teknolojia yetu imara inatengeneza mawasiliano imara kurhusu huduma safi kwa wateja watumiapo bidhaa na huduma zetu katika matawi mbalimbali”.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, aliwataka watumishi wa NCBA kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuwafurahisha wateja kwa kuwapa huduma za daraja la kwanza Pamoja na kuhudumia wateja kwa ufanisi usio wa kawaida, uthabiti, na usikivu.
Amina Ally mmoja wa wateja wa NCBA alionyesha dhamira yake kali na furaha kuelekea huduma za kibenki za NCBA.
Alisema "Huduma zao nazifurahia, watu wao ni wasikivu. Nikiwa na tatizo lolote kama nihitaji mkopo Napata ushauri, wananipa mwongozo mzuri katika jambo lolote lile nalotaka kufanya".
Kwa upande mwingine, Seraphin Lusala mteja mwingine wa NCBA, alibainisha kuwa " Huduma za kadi ya mkopo ya NCBA ni nzuri kwangu. Ninathamini sana huduma zao za msaada kwa wateja,"
Nukuu hizo zina thibisha nia ya kweli ya NCBA kwa wateja wake na kufuatia hatua ya hivi karibuni ya benki hiyo kuzawadia katika tuzo za Global Banking & Finance kutoka Global Finance Review.
Mwaka huu, benki hiyo iliadhimisha wiki yake ya huduma kwa wateja kwa kuwatembelea wateja wao na kusikiliza maoni kutoka kwao ili kujifunza changamoto zao za kuboresha huduma za benki na msukumo wa ukuaji kwa wateja.
No comments:
Post a Comment