Salamu hizo za shukrani zimetolewa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo wakati wa hafla iliyofanyika katika tawi la Benki hiyo lililopo Oysterbay, Jijini Dar es Salaam. Nshekanabo alisema wateja wamekuwa msingi mkubwa kwa Benki ya CRDB kufikia mafanikio ambayo imekuwa ikiyapata kufikia kuwa ‘Benki Bora zaidi Tanzania’.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo amesema pamoja na kuwashukuru wateja, katika Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu wamedhamiria kuwasherekea wale wote walio mstari wa mbele kuiwezesha benki hiyo kutoa huduma bora”.
Uriyo alisema Benki ya CRDB itaitumia wiki hii kuwashkuru na kuwasherehekea wateja ambao wamekuwa chachu ya huduma bora zinazotolewa na benki hiyo. Aidha, watakuwa wakiwasherekea wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa huduma bora kwa weledi na ubunifu mkubwa.
Benki ya CRDB inatajwa kuwa benki inayoongoza kwa huduma bora kwa wateja. Mwaka huu benki hiyo imetunukiwa tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ na jarida maarufu duniani la nchini Uingereza la Euromoney. Mwaka jana mwishoni benki hiyo ilitunukiwa ‘Tuzo ya Ubora’ na Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya (European Society for Quality Research).
Uwekezaji huu pia umeongeza ufanisi katika njia mbadala za utoaji huduma; CRDB Wakala zaidi ya 22,000, ATMs zaidi ya 550, na huduma za SimBanking, SimAccount, na Internet banking. “Benki pia imewekeza katika mafunzo kwa wafanyakazi ili kuwawezesha kupata weledi pindi wanapowahudumia wateja. Hii imeenda sambamba na uboreshaji wa taratibu zetu za utoaji huduma (processes) ili ziendane na mahitaji ya wateja,” alisema Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.
Baadhi wa Wateja wa Benki ya CRDB wakishiriki shidano fupi la kupamba Keki ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli mbiu "Sherehekea Huduma" iliyofanyika leo kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Shampeni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda baada ya kushiriki shidano fupi la kupamba Keki ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli mbiu "Sherehekea Huduma" iliyofanyika hivi karibuni kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Oysterbay, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (wapili kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo.
No comments:
Post a Comment