Bagamoyo, January 29, 2020: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imezindua mpango wa ufadhili wa masomo utakaowanufaisha wanafunzi 30 kutoka katika jamii za wakulima hapa nchini kupata elimu ya ngazi ya chuo katika vyuo vya ndani vinavyofundisha masomo ya kilimo.
Ukijulikana kama Kilimo-Viwanda scholarship program, mpango huu unalenga kuongeza wataalamu wa kilimo watakaowasaidia wakulima nchini kuongeza uzalishaji, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti wakati wa uzinduzi wa program hiyo katika chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.
“Ni muhimu kwetu sisi kama SBL kuiunga mkono Serikali katika kuwajengea uwezo wakulima wetu kupitia kuwaongezea wataalamu wa kilimo watakaosadia kuwashauri na hivyo kuongeza tija katika kilimo,” alisema Ocitti.
Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ni moja kati ya vyuo vitatu ambavyo kampuni ya SBL inashirikiana navyo katika kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, programu hiyo inawalenga siyo tu wanafunzi wanaotoka katika familia zenye vipato duni lakini pia wanafunzi wanaotoka katika jamii za wakulima katika sehemu mbali mbali hapa nchini. Kila chuo kitapata nafasi ya kutoa wanafunzi 10 kila mwaka na watakaolipiwa ada na SBL mpaka watakapomaliza masomo yao.
Kwa mujibu wa Ocitti, programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama. Alisema, mwaka jana SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 za nafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka.
“Kampuni ya SBL inalengo la kuongeza kiasi cha malighafi inayonunua kutoka kwa wakulima wa ndani hadi asilimia 85 kufikia mwaka 2020 na ndiyo maana tumeona umuhimu wa kusaidia kusomesha wataalamu wa kilimo ili wakafanye kazi ya kuboresha kilimo chetu. Kwa sasa kampuni inanunua malighafi kutoka kwenye mtandao wenye wakulima 400 hapa nchini,”. alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture Sinani Simba aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuja na wazo la kutoa ufadhili wa masomo ya kilimo na kuongeza kuwa ili kilimo kiwe cha tija wataalamu wengi wanahitajika.
“Tunayo Furaha kwa kuwa ufadhili huu unawalenga wanafunzi wanaotokea katika familia zenye vipato duni ambao kama siyo msaada wa SBL, wasingeweza kupata fursa ya kuendelea na masomo,” alisema
Kwa taarifa zaidi wasiliana na;
John Wanyancha,
Mkgrugenzi wa Mahusino kwa Umma
Simu: 0692148857
E-mail: john.wanyancha@diageo.com
No comments:
Post a Comment