| Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya mauzo iliyopewa jina la 'Mimi ni Shujaa' kwa Patrick Paul jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa wafanyakazi wa benki hiyo ina lengo la kuhamasisha utendaji kwa wafanyakazi wanohusika katika kitengo cha mauzo ndani ya benki hiyo. Wanaoangalia kutoka wa pili kushoto ni, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Andrew Lyimo, na Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Wateja Binafasi wa Absa Group, Nazim Mahmood. |
No comments:
Post a Comment