Dar es Salaam, Desemba 11, 2015: Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Reach for Change (R4C) wametangaza washiriki 15 wenye vipaji vya ujasiriamali wa kijamii wamechaguliwa katika shindano la “Tigo Digital Change Makers’ ambapo washindi wawili watatangazwa wiki ijayo.
Shindano hili lilioanza Septemba, limepokea mamia ya maombi kutoka kwa washiriki wenye ubunifu wa kiteknologia katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, ukulima na afya kwa mujibu wa Afisa wa Huduma kwa Jamii wa Tigo, May Thomas
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salam leo, May amesema, wajasiriamali wa kidijitali 15 waliochaguliwa kila mmoja wao alileta suluhisho la kidijitali lenye ubunifu lilokusudia kuboresha maisha ya watoto nchini Tanzania, na ndio kigezo kilicho wafanya wafuzu kushiriki katika shindano hilo.
May alisema: wengi katika hawa waombaji fikra zao ubunifu zimeenda sambamba na mkakati wetu wa kuleta mabadiliko ya kidijitali maishani. Hali imesababisha changamoto kubwa katika zoezi la kuchagua washindimda,” alisema, huku akiongeza kuwa washindi hao wawili watapokea dola za kimarekani 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kutekeleza miradi yao.
Tigo na Reach for Change wameendesha shindano hili la Digital Change-Makers nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, ambapo wajasiriamila wa kijamii saba wameshinda fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi yao. Kwa mujibu wa May, miradi ya wajasiriamali wa kijamii hao saba kwa pamoja imesaidia ya zaidi ya watoto 10,000 nchini katika kipindi hicho.
Shindano la Tigo Digital –Makers lina malengo ya kuwaendeleza na kuwatia moyo wajasiriamali wa kijamii kutumia teknolojia za kidijitali kusuluhisha baadhi ya matatizo sugu nchini Tanzania
Kuhusu Reach for Change
Reach for Change ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Sweden na lilianzishwa na Kinnevik, mwanzilishi wa kapuni ya Millicom. Dira ya Reach for Change ni kuhamasisha harakati za kimataifa za ubora, ujasiri na shauku kwa mawakala wa mabadiliko, kujenga dunia iliyo bora kwa watoto. Reach for Change inabainisha na kusaidia wajasiriamali wa kijamii barani Ulaya, Afrika na Asia.
Kuhusu Tigo
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania , ikijulikana kama “nembo ya maisha ya kidijitali yanayojitosheleza”. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo mapya 500 yenye mtandao wa Tigo na kufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini. Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 9 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni la Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 12 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na amerika ya Kusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani. Pamoja na ujuzi Fulani walionao ambao unawafanya kubuni mara kwa mara na kuwafanya wawe juu, Millicom anaendelea kujenga thamani kubwa kwa mbia; kutumia dhana yao ya "mahitaji zaidi" hivi ndivyo wanafanya biashara na kurejesha nafasi yao kama viongozi wa maisha ya kidijitale hasa katika masoko zaidi ya kipekee na yenye changamoto.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz or wasiliana na:
John Wanyancha – Meneja Mawasiliano
Mobile: 0658 123 089
john.wanyancha@tigo.co.tz
No comments:
Post a Comment