Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 8 December 2015

TAASISI YA SEKTA BINAFSI, BOT, BENKI YA DUNIA WAJADILI MFUMO WA MIRADI YA PPP

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda akihojiwa na waandishi wa habari katika hafla ya ufungaji wa semina ya siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia.
Mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, Jeffrey Delmon (kulia) akizungumza na washiriki semina ya siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda (kulia) akizungumza katika hafla ya ufungaji wa semina ya siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Kamisha wa PPP kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu.
Kamishna wa Sera ya Ushirikiano wa Sekta Binafsi ya Umma (PPP) kutoka Wizara ya Fedha, Dk. Francis Mhilu (kulia) akiagana na Mtaalamu wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, Jeffrey Delmon baada ya kumalizika kwa semina ya siku mbili kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ikishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Benki ya Dunia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Gideon Kaunda.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo kutoka Benki ya Maendeleo, George Wandwalo (kushoto) akiuliza swali.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo iliyokuwa ikijadili ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma (PPP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment