Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kwenye kongamano la 28 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (Institution of Engineers Tanzania – IET) juu ya mchango wa sekta ya fedha na mikopo ya nyumba katika kuimarisha sekta ya ujenzi wa nyumba endelevu za gharama nafuu nchini. Kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam lilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mwishoni mwa wiki iliyopita. IET ni Taasisi inayojitegemea iliyoundwa mwaka 1977, ikiwa na lengo la kuimarisha fani ya Uhandisi hapa nchini. Taasisi hii tayari ina jumla ya wanachama 3,000 kutoka katika sekta mbalimbali hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment