Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 25 November 2014

SERENGETI YATOA ZAWADI YA LIMO BAJAJ KWA MSHINDI WA KWANZA WA PROMOSHENI YA “TUTOKE NA SERENGETI”

Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Tutoke na Serengeti, ambapo Rukia Athuman Almas toka Morogoro ameibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia Limo Bajaji mpya yenye thamani ya tsh milioni tisa, kushoto ni mkaguzi toka bodi ya Michezo ya kubahatisha, Bakari Maulid. Haflahiyo ilkifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia), akiongea kwa njia ya simu ya mkononi na Rukia Athuman Almas ambaye ni mshindi wa kwanza wa promotion ya Tutoke na Serengeti, kushoto ni mkaguzi toka bodi ya Michezo ya kubahatisha, Bakari Maulid. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

25 Novemba 2014, Dar Es SalaamDroo ya kwanza ya kukuza mtaji, inayonjulikana kama “Tutoke na Serengeti” imefanyika leo 25th Nov. 2014 katika ofisi za Serengeti Breweries Chang’ombe  ambapo Bi. Rukia Athuman Almasi ameibuka mshindi wa kwanza wa Limo Bajaj.

Bi. Rukia Athuman kutoka Morogoro alipokea taarifa hizi kwa mshituko na bashasha baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Limo Bajaji. Akiongea kwa njia ya simu, Bi. Rukia Athuman Almasi alisema pamoja na kushiriki promosheni hiyo hakujihesabu kama mwenye bahati kati ya wenye bahati, hivyo basi ilimshangaza kuitwa mshindi.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kumtangaza mshindi, Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager, Bwana. Rugambo Rodney alisema “SBL inajivunia kwamba mashindano haya yamekuwa na mwanzo mzuri, shukrani kwa ushirikiano kati ya Serengeti Breweries na B-Pesa. Droo hii ya kwanza imeashiria kwamba kila mtu anaweza kushinda ili mradi tu ashiriki kwa kunywa  Serengeti Premium Lager”.

Kampeni hii inatoa fursa kwa kila mtanzania aliye na umri wa miaka 18 na zaidi kushiriki ambapo zaidi shilingi milioni 100 zinasubiri washindi na hii ni fursa ambayo kila mtu hapaswi kuikosa.”.

Ili kufanikisha kampeni hii, SBL imeungana na B-Pesa, wataalam wa teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha kwa washindi mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi. Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa masoko wa B-Pesa, Mr. Salil Abbas zilisema kuwa “kampeni imeanza vizuri na takwimu zinaonyesha kwamba watu wengi wameshiriki zaidi katika kampeni hii zaidi ya matarajio yetu ya awali. Aliitaja namba ya huduma kwa wateja ambayo ni 0225555000 ambayo itawasaidia wateja ni jinsi gani wataweza kujichukulia zawadi zao pia kuelezea kwa kina zaidi kwa wateja watakao kuwa na maswali.

“Tutoke na Serengeti” ni kampeni inayowazawadia wateja zawadi murua ya utalii wa ndani  kwa kuwapeleka washindi kufurahia mwisho wa wiki na wapenzi wao katika mbuga za taifa.

Kampeni hii ninawalenga wateja zaidi ya milioni 20 walio katika nafasi ya kushinda fedha taslim zenye thamani ya shilingi milioni 100 ambazo zimegawanywa katika mafungu ya shilingi 5,000, pia kuna bajaji sita aina ya Limo ambazo zinajulikana pia kama ‘Serengeti Bajaj’ zenye uwezo wa kubeba abiria  saba. . Pia kutakuwa na washindi wa bia za bure ambazo zitakuwa zikipatikana katika baa nchi nzima.

Promosheni hii ni kampeni ya kitaifa itakayoendeshwa kwa  miezi mitatu. Ili kuwa mshindi, unachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Serengeti Premium Lager na kuangalia chini ya kizibo kujua kama umeshinda. Namba ya kodi ambayo mteja atatumia baada ya kufungua kizibo ilitajwa kuwa ni 15317 na baada ya hapo utaingizwa kwenye droo ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Kwa taarifa zaidi :
Tembelea ukurasa wa facebook wa Serengeti Premium Lager na Twitter.

KUHUSU SERENGETI BREWERIES LIMITED 
Serengeti Breweries Limited ni kampuni ya bia ambayo huandaa, kuzalisha na kuuza vinywaji vilivyotengenezwa na shairi, ngano na mtamaa nchini Tanzania.

Kikiwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam, SBL hutengeneza vinywaji vifuatavyo:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®.

SBL pia husambaza vinywaji mbalimbali vikali vya kimataifa kama Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.


Serengeti Breweries Limited ni kampuni mwenza ya East African Breweries Limited/ DIAGEO PLC.

No comments:

Post a Comment