Dar es Salaam, Tanzania – 14 Agosti 2026
Vodacom Tanzania, kupitia Vodacom Tanzania Foundation, inaendelea kuchangia katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto nchini kupitia ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule tatu za msingi za umma zilizopo mikoa ya Pwani, Ruvuma na Morogoro.
Mpango huo unaotekelezwa kwa kuzingatia mahitaji yaliyobainika katika jamii, unalenga kuimarisha mazingira ya elimu, hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule za umma.
Kupitia mpango huo, jumla ya madarasa sita yameboreshwa katika Shule za Msingi Vikindu wilayani Mkuranga, Pwani; Mahilo mkoani Ruvuma; na Ihowanja mkoani Morogoro, ambapo kila shule imepatiwa madarasa mawili. Kati ya madarasa hayo, mawili yamekarabatiwa huku manne yakijengwa upya.
Maboresho hayo yanatarajiwa kunufaisha jumla ya wanafunzi 4,838, wakiwemo 117 wenye mahitaji maalum, pamoja na walimu 52. Aidha, Vodacom Tanzania imetoa jumla ya madawati 90 kwa shule hizo tatu.
VODACOM YAKABIDHI MADARASA VIKINDU
Hafla ya kwanza ya makabidhiano ilifanyika katika Shule ya Msingi Vikindu, Wilaya ya Mkuranga, ambapo Vodacom Tanzania ilikabidhi madarasa yaliyoboreshwa pamoja na madawati kwa uongozi wa shule.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, George Nyanda, Meneja Mauzo Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania, alisema uwekezaji huo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kufundishia kwa walimu.
“Katika Shule ya Msingi Vikindu, madarasa haya mawili yanalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na kufundishia kwa walimu. Kuitikia mahitaji ya jamii kunahitaji kuelewa mambo yanayoweza kuleta tofauti katika maisha ya kila siku ya watoto, hususan wale wenye mahitaji maalum,” alisema Nyanda.


.jpeg)




.jpeg)
.jpeg)























.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)





