Julai 28, 2026 | Dar es Salaam
Katika hatua inayotarajiwa kuongeza kasi ya matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali nchini, Selcom Microfinance Bank imezindua Selcom Business, akaunti mpya ya benki ya kidijitali inayolenga kuwapa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), kampuni na watengenezaji wa mifumo (developers) huduma za benki zenye gharama nafuu, uunganishaji wa mifumo kwa haraka na usimamizi bora wa fedha za biashara.
Uzinduzi huo unakuja wakati ambapo biashara nyingi nchini zinaendelea kutafuta njia za kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi kupitia teknolojia. Selcom Microfinance Bank inaeleza kuwa huduma hiyo imebuniwa kushughulikia changamoto mbili zinazowakabili wafanyabiashara wengi—gharama kubwa za kufanya miamala na muda mrefu unaochukuliwa kuunganisha mifumo yao na taasisi za kifedha.
Kupitia Selcom Business, biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwenda benki zote za ndani, mitandao ya simu na wafanyabiashara wanaotumia TanQR kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala. Vilevile, biashara zinaweza kujisajili na kupata REST APIs moja kwa moja kupitia dashboard ndani ya saa chache, bila kulazimika kupitia taratibu ndefu za makubaliano au kulipa ada za uunganishaji wa mifumo.
Mabando Matatu kwa Mahitaji Tofauti ya Biashara
Ili kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya biashara, Selcom Business imeanzisha mabando matatu ya kila mwezi yenye viwango tofauti vya gharama za miamala.
| Bando | Ada ya Mwezi (Siku 30) | Miamala hadi TZS 20 Milioni (Benki, Mitandao ya Simu na TanQR) | TZS 20–50 Milioni(Benki za Ndani) | Zaidi ya TZS 50 Milioni(Benki za Ndani) |
|---|---|---|---|---|
| Bando Poa | TZS 49,999 | TZS 250 | TZS 4,000 | TZS 8,000 |
| Bando Bomba | TZS 99,999 | TZS 150 | TZS 2,500 | TZS 5,000 |
| Bando Max | TZS 199,999 | TZS 100 | TZS 1,500 | TZS 3,000 |
Benki hiyo imeeleza kuwa hakuna kikomo cha idadi ya miamala inayoweza kufanywa ndani ya mwezi. Kadri biashara inavyochagua bando kubwa zaidi, ndivyo gharama ya kila muamala inavyopungua. Viwango vyote vinajumuisha VAT na ushuru wa bidhaa.
Ubunifu Unaolenga Kuongeza Ufanisi wa Biashara
Mbali na gharama nafuu za miamala, Selcom Business imejengwa juu ya huduma tatu kuu ambazo benki inaamini zitabadilisha namna biashara zinavyofanya shughuli zao za kifedha.
Kwanza ni bei nafuu za miamala, ambapo biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala kupitia Bando Max bila kikomo cha idadi ya miamala ndani ya mwezi.

.jpeg)




.jpeg)











.jpeg)

.png)








.jpeg)
.jpeg)