Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Friday, 24 July 2026

NMB YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 224 KATIKA MKOPO WA PAMOJA KWA MGODI WA DHAHABU WA GEITA

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna.

Benki ya NMB imewekeza takribani dola za Marekani milioni 100, sawa na Shilingi bilioni 224, katika mkopo wa pamoja wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita. Mkopo huo, ulioratibiwa na Nedbank Corporate and Investment Banking kwa niaba ya AngloGold Ashanti, unaifanya NMB kuwa benki kubwa zaidi kutoka Tanzania kushiriki katika muamala huo wa kimataifa.

Ushiriki wa NMB katika mkopo huo unaonesha uwezo unaoongezeka wa taasisi za fedha za ndani kuhamasisha mitaji kwa ajili ya uwekezaji mkubwa wa kimkakati. Fedha hizo zinatarajiwa kusaidia kuendeleza shughuli za uzalishaji katika mgodi huo, kuongeza mauzo ya dhahabu nje ya nchi, kuchochea ajira, kuimarisha ununuzi kutoka kwa wazabuni wa ndani na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMBBi. Ruth Zaipuna, amesema muamala huo ni uthibitisho wa utekelezaji wa Agenda 2030 ya benki kwa vitendo. Amesema NMB itaendelea kutumia mtaji wake, utaalamu na ushirikiano wa kimkakati kuelekeza fedha katika sekta zenye uwezo mkubwa wa kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi wa Tanzania.

Hadi sasa, Benki ya NMB imetoa mikopo yenye thamani ya takribani Shilingi bilioni 400 kwa sekta ya madini, hatua inayoendelea kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Uwekezaji huo pia unaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuimarisha mchango wa sekta binafsi, kuongeza mauzo ya nje, kukuza maendeleo ya viwanda, kuunda ajira na kuongeza ushiriki wa biashara za ndani katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.

No comments:

Post a Comment